Bank Officer-Mama aliyeshindwa kulipa ada ya mtoto shule anakuja kukopa pesa Bank ili alipe ada ya mtoto wewe afisa mikopo,unaomba rushwa kwa mwanamke mjane ,mwenye shida.
Mama mjane anakuahidi kuwa atakupa pesa mkopo ukikamilika,mkopo unatoka kisha anakupa kwa simanzi na masikitiko makubwa pesa ya mkopo ambao atakuwa anakatwa kila mwisho wa mwezi.
Pesa unayopewa unaenda kununua tairi LA gari, -hii ni laana ambayo unarithisha kizazi chako.
Bank Teller- Mzee asiyejua kusoma na kuandika ,ameandikiwa deposit receipt 30,000/= kwa tarakimu na maneno lakini amekukabidhi Tsh 300,000/= kwa tamaa yako unampoka 270,000/= na kuweka 30,000/= pesa ya manung'uniko ina laana ,na utavuna laana.
Doctor- Unatambua watu wanakesha wakiomba Mungu ,awajalie kupata watoto ,wewe ni bingwa was kutoa mimba ,wakati utungo wa mimba ni kazi ya Mungu,laana ya mauaji inakutesa daima mpaka ufanye toba.
Nurse-Mgonjwa masikini aliyeuza ng'ombe ili aweze kupata tiba wewe unachukua rushwa kwa ajili ya manufaa yako wewe,unapanda mbegu ya kizazi cha laana.
HR-mtoto wa masikini amekidhi vigezo katika nafasi husika ,wewe kwa tamaa zako ,unaomba rushwa ya ngono kwa asiye na vigezo unafanya naye mapenzi na kumpa ajira mtu ambaye hastahili ,Mungu anaona laana yako.
Police - Unapoka Mali za masikini kwa sababu ya nafasi uliyonayo ,unatumia cheo chako kumwaga damu isiyo na hatia,nakukumbusha tu Mungu ni was haki,deni la damu hulipwa kwa damu.
Mwanafunzi wa chuo kikuu,unaiba mume wa mtu na haujaolewa ,mkewe na watoto wanaishi maisha magumu sababu yako wewe ,laana inakungojea kwenye ndoa yako.
Wewe mwanaume ambaye unaingilia kinyume na maumbile watoto wa kiume ,Kwenye familia na kizazi chako mbegu ya ushoga ndio umefunga nayo agano tayari.
Mwalimu- kazi yako kubwa ni kubebesha mimba watoto wa masikini ,ndio maana mikono yako imetoboka sababu mishahara haikai kwako juu ya manung'uniko ya watu.
Kiongozi wa serikali, mnatumia rasilamali za masikini kwa faida yenu ,na utajiri wenu umejaa damu za walalahoi na wakesha hoi,laana imetamalaki kwenye viuono vya uzao wenu. .
Natamani kuandika karatasi lenye urefu wa Metre 100 mapungufu yetu ili atakayesoma Leo Ijumaa kuu afanye toba na tuishi maisha ya haki na uadirifu ili tutufuke na BWANA Yesu na kuisha maisha mapya.
Who ever is cares with the truth in small matters cannot be trusted with important matters.