Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,300
- 25,920
Ulaghai na utapeli wa elimu ni wa kupigwa vita na kila mpenda maendeleo ya nchi yetu. Kila mtanzania anayo fursa ya kupata elimu kadiri ya uwezo wake. Hilo linatamkwa katika Ibara ya 11 ya Katiba yetu. Watanzania husoma katika mazingira tofauti. Wapo wanaosoma kwa raha na wale wanaosoma kwa mbinde. Lakini, kikubwa ni kupata elimu.
Elimu yetu hushuhudiwa na cheti. Cheti hubeba,pamoja na matokeo na ngazi ya elimu husika, jina la mwenye cheti hicho na sifa hiyo ya elimu. Mwenye cheti ndiye mwenye fursa ya kupata kazi, mafunzo na nafasi kulingana na cheti chake. Kitendo cha mtu mwingine kujifanya yeye ndiye mwenye cheti na kulaghai watu kuwa ndiye hakivumiliki.
Narudia tena, utapeli na ulaghai wa elimu unapaswa kupingwa kwa nguvu zote. Matapeli na walaghai wa elimu ni watumiao vyeti vya wengine kupata fursa za kimaisha na kujifanya wao ndio wenye hivyo vyeti. Tunakubaliana kuwa elimu yetu ni pyramidal in shape,yaani huanza na wengi na kumaliza na wachache katika ngazi za juu. Huo ndio ukweli wa elimu yetu.
Kitendo cha kutumia cheti cha ngazi yoyote ya elimu cha marehemu au mtu mwingine yeyote hakivumiliki. Tunaoguswa hasa na mapambano haya dhidi ya matapeli na walaghai wa elimu ni sisi tuliofanyiwa uhakiki takribani mara tatu na Serikali. Uhakiki wa Serikali ndiyo kielelezo cha vita dhidi ya utapeli wa elimu na kukerwa kwetu kama nchi katika hilo.
Tafadhali, kama ulifeli na unatumia cheti kisicho chako, hata kama umebadili jina, jitokeze mwenyewe na ukiri. Ukijificha utafichuliwa kwa aibu kubwa. Ni lazima matapeli na walaghai wa elimu wapigwe vita. Hawapaswi kuachwa watambe wakiwa na sifa wasizozistahili. Kila mtanzania anamjua wa karibu yake. Tuambiane ukweli kulinda elimu yetu.