Mungu huwapenda wasemao ukweli lakini huwavumilia wasemao uongo! Ukweli lazima ubaki kuwa ukweli na uongo vivyo hivyo.
Kama taifa, tunahitaji ukweli ushamiri ili tuweze kuyafikia na kuyatekeleza malengo yetu pendwa ya maendeleo ya nchi. Ikiwa tutaukumbatia uongo na kuufanya uwe ndio ukweli basi tutabaki maskini daima na ikibidi tutarudi nyuma kimaendeleo.
Mazingira yaliyopo kwa sasa hayana afya kustawisha taifa katika misingi ya uwazi na ukweli ili kujenga mazingira ya uwajibikaji kwa manufaa ya taifa na si watu wachache wenye nafasi za uongozi. Tukisema ukweli na wenye dhamana wakauzingatia tutasonga mbele tukiwa pamoja kama taifa kinyume chake wenye dhamana tutatumia nguvu kubwa kuwaaminisha wananchi kuwa taifa lipo vizuri na linapiga hatua ilihali hali halisi inaonyesha tunarudi nyuma.
Ukweli ni upi ambao tunapaswa kujuzana?
Biashara za ndani na nje zimevurugwa zikavurugika
Mapato ya ndani na ya nje yameshuka
Uwezo wa taifa kujiendesha upo shakani
Hali ya kisiasa haina afya kwa mustakabali wa taifa
Sekta ya elimu inadorora
Umaskini unakithiri
Ari ya kufanya kazi miongoni mwa watumishi imeshuka
Matumizi ya nguvu ya dola yameshamiri
Ubaguzi kwa misingi ya kisiasa imeshamiri
Umoja wa kitaifa upo rehani
Kuaminiana hakupo tena
Utawala ni wa mtu mmoja (Autocratic)
Uvunjaji wa katiba umeshamiri
Uvunjaji wa haki za binadamu imekuwa jadi
Watawala hawapo tayari kuonywa na hata kukosolewa
Utekelezaji wa miradi ambayo haijaidhinishwa na mhimili husika
Ukosefu wa ajira umeongezeka
Tunaaminishana uongo kuwa ukweli kwa yafuatayo:
Mapato yameongezeka
Nidhamu ya kazi miongoni wa watumishi wa umma imeongezeka
Mhimili wa kuidhinisha mapato na matumizi kwa shughuli mbalimbali za maendeleo ya nchi upo vizuri
Demokrasia imeshamiri
Nchi imejaa amani na utulivu
Umaskini unapungua kwa kasi
Kiwango cha elimu kinapanda kwa kasi
Utawala wa sheria unazingatiwa
Kila mhimili unafanya kazi yake kwa uhuru pasipo kuingiliwa na mhimili mwingine
Haki za binadamu zinazingatiwa
Huduma za kiafya zimeimarishwa
Kwa ujumla nchi inapiga hatua kimaendeleo
''Asemaye ukweli ampendeza mmumba wake maana muongo anavumiliwa tu''