Ukweli nyuma ya kupendwa na kila mtu

Ukweli nyuma ya kupendwa na kila mtu

one one chief

Member
Joined
Jan 22, 2014
Posts
37
Reaction score
99
Nadharia ya kimarx inayozungumzia juu ya maendeleo ya kijamii, inasisitiza Zaidi juu ya mvutano wa kijamii, nadharia hii inaeleza kuwa ili jamii iendelee ni lazima kuwapo na mvutano kati ya pande mbili zinazokinzana, upande mmoja uwe na mawazo na mwingine uwe na mawazo mbadala kisha mawazo hayo mawili yavutane na kuibuke mawazo bora Zaidi, hapo ndipo maendeleo hutokea baada ya mawazo kushindwa na mawazo yaliyobora Zaidi.

Nadharia hii ya kimarx ndiyo inayofanya kazi katika jamii, jamii haiendelei kwa mawazo ya aina moja ila kwa mawazo bora yaliyoshindana na mawazo mengi kisha mawazo bora kuchaguliwa. Mifumo ya kidemokrasia inayoongoza katika nchi nyingi, mabunge, mabaraza na mikutano ya kimashauliano ni zao la nadharia za kimarks zilizolenga kuboresha maisha ya jamii nzima. Ubaguzi, upendeleo na ukandamizwaji wa haki za kiraia ni adui wa nadharia ya kimarkx.

Amri iliyo kuu katika vitabu vitakatifu ni upendo, mungu anatuagiza binadamu wote tupendane tena kama vile sisi tuzipendavyo nafsi zetu ndivyo tunatakiwa kuwapenda wenzetu, Bila shaka hii ni amri njema kwa wanadamu wote. Pamoja na kwamba hii ndiyo amri iliyo kubwa lakini kuna walakini katika kupendwa na kila mtu, binadamu aliyekamilika, mwenye maono, na mpambanaji haiwezekani kupendwa na watu wote, kama katika jamii unayoishi watu wote wanakupenda kwa dhati basi ipo shida kubwa kwenye maisha yako.

Kupendwa na kila mtu pengine ili ni tamanio la kila mmoja wetu, ili kila mtu akupende ni lazima kumlizisha kila mmoja wao jambo ambalo ni gumu kutekelezeka katika miili hii ya nyama, kila mtu anayo mahitaji yake katika jamii ambayo ni tofauti na mahitaji ya mtu mwingine, kila mtu anavipaumbele vyake ambavyo ni tofauti na binadamu wenzake, kila mtu ananafasi ya kutekeleza mambo yeke amabayo ni tofauti na wenzake, lakini Zaidi kila mtu aliumbwa na kupewa jukumu lake ambalo ni tofauti hata na la wazazi wake. Katika mazingira kama haya amabapo kila mtu hujitahidi kutekeleza kulingana na utofauti alio nao na wenzake ni ngumu kupendwa na kila mtu.

Kama utafanikiwa kupendwa na kila mtu ina maana umeweza kwa kiasi kikubwa kupuuzia na kutelekeza majukumu yako ipasavyo, ukweli ni kwamba watu watakupenda endapo tu utaachana na mambo yako na kufuata mambo yao, watakushangilia kwa ujinga wako, kwa upuuzi wako, kwa uzembe wako na Zaidi kwa umbumbu wako.

Kuchukiwa sio dhambi, swali unachukiwa kwa lipi jambo la kutia moyo ni kwamba wote wanaoonesha chuki dhidi ya watu wengine huwa na uwezo mdogo kufikiri na watu wenye uwezo mkubwa huwa wanapuuzia ata kama ungefanya jambo la kipuuzi mbele yao, tofauti ni kwamba watu wenye uwezo mdogo huesabu udhaifu wetu, ujinga wetu au umbumbu wetu, lakini ni kwamba yote hayo ni nyakati amabazo kila mwanadamu mwenye nyama hupitia kisha hujifunza na maisha huendelea mbele, watu wenye uwezo mkubwa kiakiri hawahesabu mapungufu yetu hupuuzia na kuona ni sehemu ya ubinadamu ambayo kila mtu hupita kwayo, watu wenye uwezo mdogo hutukalia vikao kuujadili udhaifu wetu, hufurahia na kuushangilia wakizani wao ni bora Zaidi yetu lakini ukweli ni kwamba wao ndio wajinga Zaidi yetu.

Ni ngumu kupedwa na kila mtu kwa sababu una uelekeo wa maisha ambao ni tofauti na wao hivyo ni lazima wataonesha chuki wakidhani unashindana nao, kwasababu una namna ya kutatua mambo yako watadhani unaonesha ubora dhidi yao, hivyo ni lazima watakukalia vikao, kwasababu unajukumu tofauti na lao watadhani unaringa au unajikwaza dhidi yao hivyo watakusengenya tu.

Ni ukweli wa uharisi kwamba huwezi kupendwa na kila mtu na huwezi ukachukiwa na kila mtu, chamsingi ni kwamba kila mtu anajukumu lake katika maisha yako kwa wakati wake, ukigundua kuwa kuna watu hawakupendi sio jibu kujitenga nao kuwajua itakusaidia kuchukua tahadhari unapokuwa nao, lakini ukiishi nao yapo utajifunza kutoka kwao kwamaana binafsi naamaini twapaswa kuyatafuta maarifa sehemu zote ata ikiibidi kuyapata maarifa hayo kwa shetani haidhuru sana ukuujua kila ukweli.

Jamii isiyo na migogoro, jamii hiyo imekufa nadharia hii kutoka kwa kwa mwana ujamaa karl markx ndiyo iliyochochea maudhui ya ndani ya mwana fasihi nguli wa wakati wote shaban Robert kuandika hadithi ya kusadikika, katika hadithi hii yenye mtindo wa safari ya wajumbe wa kusadika waliotumwa kwenda kujifunza mambo mema katika nchi jirani na zenye maendeleo kuiliko ilivyo nchi ya kusadikika, tunaona mvutano wa majadiliano ulivo kinzana na kukinzwa, ulivyo vutanwa na kuvutwa, ulivyopiganwa na kupigwa kisha mawazo bora yakapatikana na jamii ya watu wa kusadikika wakapata mwelekeo mpya wa maendeleo ya nchi yao.

Wajumbe walichukiwa kutokana na ujumbe wao, wakadhuriwa kwasababu ya elimu yao, wakafungwa kwasababu ya mtazamo wao, wakabezwa kwasababu ya mafanikio yao, lakini si wote wanakusadikika waliwachukia, sio wote waliwabeza, sio wote waliwadhihaki, ilihitajika mawazo bora hayo washilikishwe watu wenye ubongo mkubwa mkubwa wa kufikiri tu ili kufikia lengo. Chuki ilikua kifuani mwa wapumbavu kama isemavyo biblia ya kwamba chuki na hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu tu.

Ushindi wa kimaendeleo wan chi ya kusakika ulikuja baada ya madhira yote. Bhivyo nakusihii ten asana uonapo unachukiwa na kudhihakiwa kwa jambo unalolifanya jua ya kwamba uko katika njia sahihi, unachotakiwa kufanya ni kuongeza nguvu Zaidi kwa sababu hapo ndipo mafanikio yako yalipo. Tena nakukumbusha ni kheri ushindwe kwa jambo uliloliamua wewe mwenyewe kulifanya kuliko kusikiliza maoni juu ya watu usiowaamini.

Kufahamu ukweli ni jambo moja la msingi sana katika maisha, lakini kuchukua hatua ni jambo lenye maana zaidi. Kujua sababu ya kuchukiwa ni kitu kizuri sana. Angalau sasa una pa kuanzia baada ya kufahamu ukweli.Ndugu zangu, ukishagundua kuwa unachukiwa kwa sababu ya tabia zako mbaya, basi ni wajibu wako kubadilisha tabia zako hizo mbaya.

Kumbuka unaishi na jamii na ni lazima ukutane nayo katika mambo haya na yale. Kama wewe ndiye kero kutokana labda na roho mbaya, kuwasengenya wenzako, kuongopa na tabia nyingine za namna hiyo ni wajibu wako sasa kubadilika ili uishi vizuri kwenye jamii inayokuzunguka.

Lakini ikiwa umegundua kuwa unachukiwa kwa sababu kinyume na nilizoeleza hapo juu, pia ni sawa, maana utakuwa umeshaujua ukweli. Mtu kukuchukia kwa sababu ya mafanikio, umaridadi wako, uwezo wako wa kuchangia mada na kadhalika, isikupe shida kabisa. Kwa sababu binadamu ni wabinafsi asiri ya binadamu wote duniani ni ubinafsi. Hii ni hulka ya kila mtu. Lakini hata hivyo mtu akiamua huweza kubadilika kitabia au kuficha ubinafsi wake.

Hivyo basi, ieleweke kuwa binadamu yeyote akimuona mwenzake amefanikiwa kwenye eneo fulani, hata kama hatamuonea wivu, lakini moyoni mwake angetamani kuwa na mafanikio kama fulani. usinyong’onyee moyo wako kwa sababu kuna watu wanakuchukia kwa sababu yoyote ile. Fahamu kuwa binadamu wameumbwa na tamaa ya kuwa na mafanikio.

kwa watu wanaochukia mafanikio ya wenzao ni kuongeza juhudi ili kuendelea kufanikiwa zaidi. Ikiwa labda kazini kwako watu wanakuchukia kwa sababu ni mfanyakazi bora, usirudi nyuma, fanya kazi kwa nguvu zaidi. Kama kuna mtu anakuchukia kwa sababu unavaa vizuri, endelea kununua mavazi mazuri zaidi ili uendelee kuwaumiza. Hii ni dawa kubwa zaidi, kuliko kurudi nyuma kwa sababu eti unachukiwa.

Ukipendwa na watu wote unashida katika kuishi kwako na hakuna jambo lolote unalolifanya kusogeza maisha yako, sisemi utafute kuchukiwa la hasha, jail mambo yako na yafanye kwa nguvu zako zote.

By kamchicha
 
Back
Top Bottom