Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,636
- 22,488
Ni kitu ambacho watu wengi hawakifikirii kwa makini, lakini ukweli ni wazi kwamba Tanzania ni mojawapo ya nchi zenye sheria na jeshi la Polisi lenye uonevu kwa raia zake duniani.
Hii ni kwa sababu, hapa Tanzania Polisi wanaweza kukutia ndani (arrest) kwa kosa ambalo halipo au la uzushi, au hata kubambikiwa na polisi, na kukupeleka makamani kisha wamwambie hakimu upelelezi bado unaendelea, na hakimu akakubaliana na Polisi. Matokeo ni kwamba unaweza kurudishwa rumande, na kukaa sana huko, wakati polisi wakiendelea na "upelelezi" - ili kupata uhakika (ushahidi) kama kweli ulitenda kosa.
Sasa matokeo ya upelelezi yanaweza kuwa hukutenda kosa, labda hata polisi wakagundua umesingiziwa, au hakimu akaitupilia kesi yako mbali kwa kuwa "haina mshiko" wakati ulishasota sana rumande. Huu ni uonevu wa hali ya juu.
Katika haki za msingi za binadamu, polisi hawapaswi kumkamata mtuhumiwa na huyo mtuhumiwa kunyimwa dhamana ikiwa upelelezi haujakamilika. Kwa hiyo ikiwa polisi watamwambia hakimu tunaomba kesi iahirishwe kwa kuwa upelelezi haujakamilika, basi hiyo inapaswa iwe sababu ya kumpa mtuhumiwa dhamana. Kwa nini umkamate (arrest) mtu bila kwanza kufanya upelelezi kama kweli ana kosa? Tuna sheria zinaruhusu Polisi wakamate (arrest) watu kwanza kwa kuhisi kisha ndio watafute kosa? Na kama hujakamilisha upelelezi mwachie kwa dhamana.
Lakini sijui kama wabunge, wanasheria, majaji na mahakimu wetu na hata Raisi wetu Magufuli analiona hili - au wanaliona lakini hawajali.