Ukweli ni kuwa Tanzania ilikuwa lazima tupitie kwenye hili tanuru la moto ili kuendelea. Tuliache litatusaidia.

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
Siasa zetu zimeiathiri sana nchi hii. Mambo mengi yalikuwa hayaendi na tatizo kubwa lilikuwa mifumo ya kisiasa iliyoota mizizi na kuathiri kila sekta ya jamii.

Mara kwa mara tumeshuhudia wana CCM wanajisifu kuwa Tanzania ni kinara wa Ukombozi kusini mwa Afrika. Wasichosema na nadhani siyo kwa kusahau ni kuwa ukiacha Uganda na Zimbabwe ambao kwa kiasi kikubwa wamerithi mfumo wetu na ndiyo maana matatizo yao yanafanana na ya kwetu, nchi ambazo hazijafuata mifumo kama yetu mfano Namibia, Botswana na hata Kenya hawana mikwamo kama ya kwetu.

Magufuli amekuja kwa sababu nature imechukua mkondo wake kutuondoa kwenye mikwamo ambayo tulikuwa nayo. Ndiyo, kuna watu wengi wanaumia na wameumia. Sipendezwi na hayo hata kidogo. Uthibitisho, nimewahi kuleta nyuzi nyingi kumuongelea Tundu Lissu. Ila nawaambia huko tunapokwenda mtifuano utakuwa mkubwa sana.

Bila haya yanayotokea, tungeendelea na hali tuliyokuwa nayo huku kila siku tukijipa matumaini ya uongo. Wangekuja kina Makamba, Mavunde, Jokate, nk. na kwa muda mfupi watu wangeshangilia wakidhani sasa Tanzania mpya itazaliwa kwa sababu vijana wa kisasa wataenda kubadilisha utendaji lakini nakuhakikishia, tungekuwa tunazunguka pale pale kwa sababu tatizo kubwa ni mfumo wa kizamani uliosambaza virusi vyake kwenye kila sekta. Siyo elimu, biashara, kilimo, michezo, sanaa, taaluma mbalimbali, kote huko kunahitaji kusukwa upya kabisa.

Narudia tena, kuna mtifuano usio wa kawaida uko njiani na huo utagusa kila idara na taasisi muhimu. Mlichelewa sana kuzuia hayo yasitokee na kwa kila siku inayokwenda ndiyo inavyozidi kuwa ngumu kufanya hivyo. Wengine tuliyaona haya toka December 2015 wakati tulipoambiwa hakuna sherehe za uhuru. Matendo madogo madogo yaliyoonekana hayana madhara ambayo kila yalipopita yalikuwa yanafungua njia kwa matendo mengine makubwa zaidi. Mbinu hiyo inaendelea hata leo hii.

Niliwahi kuleta uzi nikisema 'Magufuli is smarter than he looks', wengi hamkunielewa. Sijui nani yuko nje ya pazia anaye pull the strings. Sio hao mnaowadhania. Sijui 'Karl Rove' wa Magufuli ni nani na hakuna kati yetu anayemjua ILA YUPO.

Na inafikirisha sana kwa jinsi hata wale waliokuwa sababu ya mikwamo hii na ndiyo sababu ya kutufikisha hapa tulipo nao pia wanaenda kuumia pia vibaya. Poetic Justice!

Vumbi likishatulia, ni matumaini yangu tutaweza kupata maendeleo ya kweli ambapo mifumo ya kisiasa, kijamii, kisheria na kiusalama itaheshimiana na itafanya kazi kwa weledi kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi. Kuna mambo mengi sana itabidi yafanyike na haitakuwa kazi ndogo.

Tanzania tulihitaji kupitia kwenye maumivu haya. Bahati mbaya hakukuwa na jinsi nyingine. Wengine tulishajikatia tamaa na nchi hii kupata maendeleo ya kweli. Tulishaona kila kitu kinachoendelea ni smoke screen na ujinga tu. Ki ukweli tulikuwa tunadanganyana sana. Ni bahati nzuri nature imeamua kutusaidia ila ndiyo hivyo tena kwa kupitia maumivu haya mengi.

Maandiko yanatuambia kwa kila jambo tushukuru. Kwa hivyo basi, kwa hili tanuru la moto tunalopitia, pia tushukuru. Pia tusiache kuomba tufike huko salama.
 
Unaongea hivi kwa sababu kwa namna moja ama nyingine unanufaika na hili tanuru ila trust me kama ungekuwa ndani unaungua kama wanavyoungua vijana wasio na ajira, wafanyabiashara waliofilisika, walioachishwa kazi katika makampuni binafsi baada ya mapato ya makampuni hayo kupungua KAMWE usingeandika ulichoandika
 
Kwani hao vijana wanaokosa ajira huko nyuma hawakuwapo? Je ni tanzania ndo hawana ajira peke yake?
Je hao vijana wamezuiwa kujiajiri?
Je ni nchi ambayo vijana wakimaliza shule wote wanaajiriwa?
 
Mbona hoja yako yote imebase kwenye kuattack vijana? Vipi kuhusu wafanyabiashara? Kama huko nyuma walikuwepo vijana ambao hawajaajiriwa haikuwa jukumu la kwanza na mahususi kwa awamu hii kutatua tatizo hili na kutengeneza mazingira mazuri kwa sekta binafsi ili iweze kuajiri watu wengi zaidi na kuondoa au kupunguza kadhia hii...Je pia ilikua ni lazima tupitie tanuru la moto kama anavyodai mtoa mada??? Hakukua na njia nyingine zaidi ya tanuru la moto??? Na je awamu hii ni bora zaidi kuliko awamu zote zilizopita? Ni bora kuliko awamu ya kwanza ya baba wa taifa?? Je Mwalimu alikua mjinga kutolipitisha taifa kwenye tanuru la moto??
 
Kukopa bila limitations kutakuja kutusaidiaje huko mbele?
One man show itakuja saidiaaje huko mbele?

Kujenga chato kunaisaidiaje nchi?
 
Siasa zetu zimeiathiri sana nchi hii. Mambo mengi yalikuwa hayaendi na tatizo kubwa lilikuwa mifumo ya kisiasa iliyoota mizizi na kuathiri kila sekta ya jamii.

Mara kwa mara tumeshuhudia wana CCM wanajisifu kuwa Tanzania ni kinara wa Ukombozi kusini mwa Afrika. Wasichosema na nadhani siyo kwa kusahau ni kuwa ukiacha Uganda na Zimbabwe ambao kwa kiasi kikubwa wamerithi mfumo wetu na ndiyo maana matatizo yao yanafanana na ya kwetu, nchi ambazo hazijafuata mifumo kama yetu mfano Namibia, Botswana na hata Kenya hawana mikwamo kama ya kwetu.

Magufuli amekuja kwa sababu nature imechukua mkondo wake kutuondoa kwenye mikwamo ambayo tulikuwa nayo. Ndiyo, kuna watu wengi wanaumia na wameumia. Sipendezwi na hayo hata kidogo. Uthibitisho, nimewahi kuleta nyuzi nyingi kumuongelea Tundu Lissu. Ila nawaambia huko tunapokwenda mtifuano utakuwa mkubwa sana.

Bila haya yanayotokea, tungeendelea na hali tuliyokuwa nayo huku kila siku tukijipa matumaini ya uongo. Wangekuja kina Makamba, Mavunde, Jokate, nk. na kwa muda mfupi watu wangeshangilia wakidhani sasa Tanzania mpya itazaliwa kwa sababu vijana wa kisasa wataenda kubadilisha utendaji lakini nakuhakikishia, tungekuwa tunazunguka pale pale kwa sababu tatizo kubwa ni mfumo wa kizamani uliosambaza virusi vyake kwenye kila sekta. Siyo elimu, biashara, kilimo, michezo, sanaa, taaluma mbalimbali, kote huko kunahitaji kusukwa upya kabisa.

Narudia tena, kuna mtifuano usio wa kawaida uko njiani na huo utagusa kila idara na taasisi muhimu. Mlichelewa sana kuzuia hayo yasitokee na kwa kila siku inayokwenda ndiyo inavyozidi kuwa ngumu kufanya hivyo. Wengine tuliyaona haya toka December 2015 wakati tulipoambiwa hakuna sherehe za uhuru. Matendo madogo madogo yaliyoonekana hayana madhara ambayo kila yalipopita yalikuwa yanafungua njia kwa matendo mengine makubwa zaidi. Mbinu hiyo inaendelea hata leo hii.

Niliwahi kuleta uzi nikisema 'Magufuli is smarter than he looks', wengi hamkunielewa. Sijui nani yuko nje ya pazia anaye pull the strings. Sio hao mnaowadhania. Sijui 'Karl Rove' wa Magufuli ni nani na hakuna kati yetu anayemjua ILA YUPO.

Na inafikirisha sana kwa jinsi hata wale waliokuwa sababu ya mikwamo hii na ndiyo sababu ya kutufikisha hapa tulipo nao pia wanaenda kuumia pia vibaya. Poetic Justice!

Vumbi likishatulia, ni matumaini yangu tutaweza kupata maendeleo ya kweli ambapo mifumo ya kisiasa, kijamii, kisheria na kiusalama itaheshimiana na itafanya kazi kwa weledi kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi. Kuna mambo mengi sana itabidi yafanyike na haitakuwa kazi ndogo.

Tanzania tulihitaji kupitia kwenye maumivu haya. Bahati mbaya hakukuwa na jinsi nyingine. Wengine tulishajikatia tamaa na nchi hii kupata maendeleo ya kweli. Tulishaona kila kitu kinachoendelea ni smoke screen na ujinga tu. Ki ukweli tulikuwa tunadanganyana sana. Ni bahati nzuri nature imeamua kutusaidia ila ndiyo hivyo tena kwa kupitia maumivu haya mengi.

Maandiko yanatuambia kwa kila jambo tushukuru. Kwa hivyo basi, kwa hili tanuru la moto tunalopitia, pia tushukuru. Pia tusiache kuomba tufike huko salama.
Wewe utakuwa umerogwa na si vinginevyo, hujui kuwa haya yote yameruhusiwa na katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania? Kama hamyataki kwanini msibadili katiba? Hujui chochote wewe.
 
Ha
Mbona hoja yako yote imebase kwenye kuattack vijana? Vipi kuhusu wafanyabiashara? Kama huko nyuma walikuwepo vijana ambao hawajaajiriwa haikuwa jukumu la kwanza na mahususi kwa awamu hii kutatua tatizo hili na kutengeneza mazingira mazuri kwa sekta binafsi ili iweze kuajiri watu wengi zaidi na kuondoa au kupunguza kadhia hii...Je pia ilikua ni lazima tupitie tanuru la moto kama anavyodai mtoa mada??? Hakukua na njia nyingine zaidi ya tanuru la moto??? Na je awamu hii ni bora zaidi kuliko awamu zote zilizopita? Ni bora kuliko awamu ya kwanza ya baba wa taifa?? Je Mwalimu alikua mjinga kutolipitisha taifa kwenye tanuru la moto??

Hakuna mtu ana attack vijana, jambo la ajira ni kubwa na kwa kuwa vijana wengi siku hizi wanamaliza vyuo basi hata wazazi tuanze kuwaandalia mitaji na kazi za kufanya, na sio kusema srikari tu,
ajira za serikali zinaweza kuwa milioni moja na vijana wanaomaliza vyuo ni zaidi ya laki moja, sasa watafanya wapi huko serikarini wakati kuna waliotangulia hawajastaafu?
 
Back
Top Bottom