Ukweli na Uhalisia

Elisha Chuma

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
275
262
Ishi kiuhalisia endana na uhalisia wako,huenda ukweli unakuvuta ili usimame mahala ama kuonyesha uwezo lakini uhalisia ndio sehemu pekee unayoweza kuwa na amani na kutengeneza mafanikio yako.

Watu wengi wamefeli kwa kuusimamia ukweli kuliko uhalisia mathalani,ukweli ni kwamba unahitaji kula ili uishi uhalisia ni kwamba unahitaji kufanya kazi ili upate hela ya kukuwezesha kununua chakula ili uishi.

Wasanii,wafanyabiashara na watu wengi wamefelishwa sana na hiki kitu na bado kinawatafuna wengi kuung'ang'ania ukweli ilhali uhalisia unakataa ndio matokeo yake unaishi maisha yasiyokuwa ya kwako mwisho wa kuishi hivyo ni kufeli.

Ishi maisha yako ya uhalisia utapata amani ya moyo na ni rahisi kutengeneza mafanikio na mbinu zake ukiwa kwenye uhalisia kuliko kwenye ukweli wako.

#Maishanihayahaya #wakubadilikaniwewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja,watu wengi tunaishi kwa ukweli na sio kwa uhalisia.hii mentality tungeibadilisha na kuwa vice versa tungekuwa na mafanikio makubwa sana
 
Back
Top Bottom