'Ukweli' na siasa za Tanzania

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,429
1573393814868.png

Wakuu, moja ya tatizo ambalo limetuumiza, linatuumiza na litatuumiza sana kama hatutabadilika; ni kwamba hakuna anayetaka kuwa mkweli kwenye siasa zetu, na kama wapo wanaoamua kuwa wakweli, ni wachache sana na hawapati uungwaji mkono.

Mtu yoyote anayefuatilia kwa ukaribu atakubaliana kwamba, Tanzania tumekuwa na utaratibu mtu hatetei kitu kwa kuwa ni kizuri au kukemea kitu kwa kuwa ni kibaya bali kwa sababu kinamnufaisha je yeye au kundi lake. Kwa mfano;

Unakuta mtu anasema hadharani bila hata wasiwasi, hawa watu sio wakwetu mkiweza wafanyieni vurugu, na hakuna anaye kemea. Sasa subiri huyo anayesema hayo siku awe muhanga utaona atakavyoongea point hutaamini kama ni yeye.

Haya, unakuta mwingine naye anaongea point kweli leo ila ukiangalia unakuta ni muhanga. sasa ngoja atoke kwenye kundi la wahanga utaona atakavyowageuka wahanga wenzake.

Unaweza ukakuta mtu anatetea ujinga mpaka unashangaa huyu jamaa vipi, lakini sio kwamba hajui kwamba anatetea ujinga; bali ananufaika na anachotetea kwa wakati husika. Sasa subiri siku awe muhanga na aanze kuumizwa na kundi analotetea utaona atakavyoanza kujenga hoja madhubuti zilizojaa ukweli mtupu lakini sasa sio kwamba sasa anajenga hoja na kuongea ukweli kwa kuwa anaona ni wajibu kufanya hivyo, bali kwa kuwa ameshakuwa muhanga.

Kwa upande mwingine, unakuta mwingine anajenga hoja nzuri sana zenye ukweli mtupu ila wakati anajenga hoja hizo, anajitetea dhidi ya dhulma anayofanyiwa (ambapo unakuta kweli anadhulumiwa). Sasa siku na yeye akiwa upande wa mdhulumuji au akipata nafasi ya kudhulumu au kufanya 'the same error' aliyokuwa anaikemea kwa hoja nzuri na ukweli mtupu, atafanya kituko hakuna atakayeamini. Akiulizwa atajibu jibu rahisi tu! Siasa mchezo mchafu. Hivi kwa utaratibu huo, ni kwa vipi tunaweza kufanikiwa kwenye jambo lolote la maana?

Hali hii husababisha zoezi zima la kuondoa au kuzuia uovu usitokee kuwa gumu sana karibu kila mahali. Husababisha hata wanaodai kuwa wanakabiliana na uovu nao wasiaminike. Husababisha pia watu ambao ni waungwana na wana nia njema kweli ama waogope au washindwe kushiriki kwenye siasa lakini chaajabu hata wanapojaribu huwa hawapati uungwaji mkono nao ni wepesi kukata tamaa isivyo kawaida.

Ikumbukwe, kwa kadiri watu wema, wenye uelewa au maono positive wanavyoshindwa kushiriki kwenye siasa kwa sababu yoyote ile, ndivyo uwezekano wa kuwa na siasa zenye utata unavyoonezeka na hali hiyo katika hatua yake ya juu kabisa hatutaacha kutafutana.

Nini tufanye: Ni muhimu kila mtu bila kujali chama chake akajitahidi kuwa mkweli. Kwenye tatizo aseme ukweli na kwenye jambo zuri aseme ukweli bila kujali nani anafanya au nani anafanyiwa nani mnufaika au nani anaumia. Lakini wananchi nao wajenge tabia ya kukemea uovu wowote wanaouona bila kujali mfanyaji ni nani na mwathirika ni nani.

Tukiendelea na utaratibu wa kutokuwa wa kweli, na kila kitu tunaangalia kwa jicho la wao na sisi, mimi na wao nk. Mwisho wake hautakuwa mzuri bila kujali chama kipi ni kipi na madhara yake hayatachagua
 
Lakini pia kuna watu wanaongea hoja nzuri sana hapa, au waliwahi kuwa watoa hoja nzuri ila 'wakiwa wahanga wa waliyokuwa wanayajengea hoja, uhanga ulivyokoma, huwezi kuamini kama ndio wenyewe
 
Hapa jf kwenyewe kuna watu wanatetea ujinga wakati flani mpaka unashangaa hawa watu vipi, ila sio kwamba hawajui; wanajua vizuri sana, ndio maana inapotokea mmoja akawa muhanga wa uovu anaoutetea, humkuta ghafla kabadilika sasa anaongea point "Ambazo pia zina ukweli" Hili ni tatizo.
 
Shida yetu kubwa ni kutokufuata yale tuliyokubaliana na kuyaweka kwenye maandishi kua Ndiyo tutaongozwa navyo. Kila mtu anadhani anauwezo wa kutenda mazuri nje ya tuliyokubaliana kuyafuata. Kama mazazo yako ni mazuri na hayapo kwenye makubaliano basi shawishi wananchi wayakubali na kuyaandika Ndiyo uyatende tofauti na Hapo unakua Dikteta.

Hapo Ndiyo tunatofautiana na Wazungu; ukubaliani na Jambo unakaa pembei au unashawishi jamii wanayakubali then mnayaweka kwenye maandishi ndipo unaanza kuyatenda...siyo ujenga wako unayatenda tu unavyotaka wewe.
 
Wakuu, kutegemea kwamba tunaweza kupata matunda ya 'good will' bila kujenga hiyo 'good will' yenyewe ni jambo la kushangaza, lakini kinachoshangaza zaidi ni kwa nini tufikiri hivyo?
 
Na pia usije ukashangaa watu wengi wakijifanya kuwa hii mada hawajaiona, sio kwamba hawaioni, tatizo wengi inawagusa na wanajua kuwa ina ukweli ila hawako tayari kuufuta ukweli kwa sababu hizi hizi
 
Lakini pia kuna wengine sio wahanga kwa 100% kwenye baadhi ya mambo ni wahanga, kwenye mambo mengine wao ndio wanafanya wenyine wahanga. Hawa utawakuta kwenye yale ambayo wamefanywa wahanga wanapinga kwa hoja nzito zenye ukweli mtupu, ila kwa yale maeneo ambao nao wanazalisha wahanga wao, wakiambiwa nao kazi kujimwambafai, kujibu kirejareja au kupuuza, kujifanya siasa ni mchezo mchafu kwa hiyo wanatekeleza mchezo huo au kujitia ubeberu. Hii haikubaliki na sijui kwa nini tunashabikia na kuendekeza mambo kama haya?
 
Inasikitisha sana...

Mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu...


Cc: mahondaw
Yaani ni changamoto kubwa sana kwa kweli. Ushawahi kuona mtu anachungulia mahali kwa macho mawili, mwenzake analalamika kwamba jamaa anachungulia na macho mawili hataki kumuacha naye achungulie, lakini naye akipata nafasi ya kuchungulia japo kwa jicho moja, ananasia hapo hapo hawapishi wenzake hahahaa, na wenzake ambao hawaoni wanaendelea kulalamika hivyo hivyo. Kwa hiyo watu wanakuwa hawashughuliki na tatizo la msingi 'Kuchungulia peke yako badala ya kuchungulia na wenzako' bali kila mtu anawaza atakavyochungulia hahahahahha
 
Team ya Jafo na ccm yenu mkuje huku, mana nyie ndio mfano halisia, mlitetea wagombea wa serikali za mitaa kukatwa, sasa JAFO KABADILI GIA ANGANI, mnatoa mapoint kutetea kurudishwa. Mlisema haya ni matapishi ajabu sasa mnasema ni asali
 
Na kama ni mabadiliko tunayohitaji Tanzania; mabadiliko ya kwanza ni mabadiliko ya fikra za watu, Zaidi ya hapo hakuna mabadiliko mengine yoyote yanaweza kuwa na matokeo makubwa kama tutakuwa na fikra hizi hizi
 
Na kama ni mabadiliko tunayohitaji Tanzania; mabadiliko ya kwanza ni mabadiliko ya fikra za watu, Zaidi ya hapo hakuna mabadiliko mengine yoyote yanaweza kuwa na matokeo makubwa kama tutakuwa na fikra hizi hizi

Tanzania hii ya
1. Magufuli na ccm ya Vilaza (ndiyoooooo)
2. Vilaza wa taasisi muhimu- wameacha kutekeleza majukumu yao kikatiba... wanaunga mkono mambo yahovyohovyo
I. Bunge
II. Mahakama

3. Ukimya wa watu muhimu na mashuhuri
I. Mzee Ally Hassan Mwinyi
II. Mzee Benjamin William Mkapa
III. Mzee Jakaya Mrisho Kikwete

4. Ukimya/kunyamazishwa wa makundi muhimu kitaifa
I. Mashirika ya utelezi haki za binadamu
II. Uhusika wa viongozi wa kiroho

5. Kunyamazishwa vyombo vya habari na wakosoaji wenye maono na utalaamu

6. Kupuuzwa wananchi... wenye nchi yao

Kwa mustakabali huo wa tusitegemee hata siku moja kusonga mbele

Mchawi wetu ni CCM imeuwa Elimu na bado inafunga watu midomo nakufanya mambo wengi bila kuzingatia
1. Katiba
2. Utaalamu
3. Wel
 
3. Weledi

Siku CCM itatoka madarakani ndio ufunguo wa kuanzia ukurasa mpya na Tanzania mpya
 
Tunaweza kushauri kuwa ifikie hatua tuache kukimbizana na matukio, matukio yapo na yataendelea kutokea accordingly. Tunachotakiwa tufikirie ni kubadilikia ili pia kubadilisha aina ya matukio na yawe yanatokea katika mfumo positive.

Na moja ya vitu vya kukabiliana navyo kwa kuanzia ni kuondua dhana ya sasa ni mchezo mchafu. Kama tunaamini siasa mchezo mchafu na tunaamini Imani hiyo ni sahihi, sasa kwa nini tutarajie kupata matokeo safi kutokea kwenye uchafu? Tukaeni chini tufikirie wakuu, kushangaa effects badala ya kufikiria causes hakuwezi kutusaidia kitu, na kujidanganya juu ya real causes ni sawa na kujifungia kwenye kachumba ili usione kilichopo nje halafu unajidanganya nje hamna kitu
 
Shida yetu kubwa ni kutokufuata yale tuliyokubaliana na kuyaweka kwenye maandishi kua Ndiyo tutaongozwa navyo. Kila mtu anadhani anauwezo wa kutenda mazuri nje ya tuliyokubaliana kuyafuata. Kama mazazo yako ni mazuri na hayapo kwenye makubaliano basi shawishi wananchi wayakubali na kuyaandika Ndiyo uyatende tofauti na Hapo unakua Dikteta.

Hapo Ndiyo tunatofautiana na Wazungu; ukubaliani na Jambo unakaa pembei au unashawishi jamii wanayakubali then mnayaweka kwenye maandishi ndipo unaanza kuyatenda...siyo ujenga wako unayatenda tu unavyotaka wewe.
Nimekuelewa Sana. Na ndio tatizo kubwa Sana kwa awamu hii. Watu wanataka taifa liende wanavyowaza wao hata bila kutushawishi tuwaelewe. Watu wachache wanawaza, then wanaamua jambo Fulani liende hivi hata kama linaathiri taifa zima.
 
Nimekuelewa Sana. Na ndio tatizo kubwa Sana kwa awamu hii. Watu wanataka taifa liende wanavyowaza wao hata bila kutushawishi tuwaelewe. Watu wachache wanawaza, then wanaamua jambo Fulani liende hivi hata kama linaathiri taifa zima.
Watu wanadhani Ulaya kwenye demokrasia yao Wameweka nakutenda Mambo yote mazuri bali wanafuata yale waliyokubaliana kuyafauata yawe mazuri au mabaya.
 
Wasiotaka ukweli ni ccm tu dunia hii.

Walipinga mgombea huru, wakasema mgombea ni mali ya chama.

Leo wanataka wagombea washiriki licha ya vyama vyao kujitoa, sasa watashiriki vipi ikiwa vyama vimejitoa na havishiriki?!

Umeona wapi inzi aeneze kipindupindu, kisha inzi huyo huyo asambaze dawa kuua inzi waenezao kipindupindu?
 
Asili ya kazi za Wanasiasa zinashinikiza kutumikia maslahi binafsi kabla ya ya umma, na mara nyingi maslahi hayo huwa ya muda mfupi yasiotazama mbali.
Kuwaachia kufanya maamuzi ya msingi ni kama kuwaacha watoto jikoni bila msimamizi
 
Back
Top Bottom