UKWELI MCHUNGU

UKWELI MCHUNGU

UKWELI MCHUNGU ...
View attachment 984700Nyakati na Technology zimeharibu mambo mengi sana Tanzania.Wanawake wenye akili wasio na elimu walizaa na kulea ma Professors. Nyakati hizi wanawake wasomi wanashindwa kuzalisha vizazi bora vya watoto wenye adabu,hekima na maarifa. Nyakati hizi mwanamke jinsi anavyozidi kuelimika ndivyo anavyozidi kupoteza vinasaba maridhawa vya mke mwema na mama bora.

Uadilifu,unyenyekevu,lugha nzuri ni majukumu ya mwanamke kwa mume kwa sasa imekuwa misamiati kwa asilimia kubwa kwa wanawake wasomi wenye ndoa zao.
Mzazi anafurahia mtoto kuzungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha, lakini mtoto hana adabu, ni mjeuri na mwenye kiburi, social media wazazi tunapost picture za watoto wetu kwa ubora wa mavazi na uzuri wa sura lakini hatujivunii haiba na tabia njema za watoto.

"She is my happiness" mwingine utasikia "He is my handsome" lakini mtoto anamjua vyema house girl kuliko Mama.Wengi wamejificha kwenye kazi inachukua muda wangu mwingi nashindwa kukaa na mwanangu.
Wengine tumelelewa na wazazi ma -Nurse anaingia night lakini,tulisoma na kuimba table ya 1-12 ndipo tulipewa ruhusa ya kwenda kucheza,tulifundishwa kufua na kupiga pasi na bado mzazi alikuwa busy na kazi.

Mtoto ni wa mama, mama akikosa busara na hekima ya kulea watoto anaharibu kizazi chake,ukweli mchungu Tanzania divorce rate kubwa ni ya wanawake wasomi na wanaume wasomi,ndoa za watu ambao sio wasomi kuna ushirika na upendo mkubwa sana.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya mwanamke mwenye akili asiye na elimu na mwanamke mwenye elimu asiye na akili.

Busara ina unyenyekevu, uvumilivu, adabu na utu, wanawake waliokosa busara utawagundua kwa show off na kauli zao. Jiulize mtoto wa kike wa miaka 8 anafuliwa chupi,anaandaliwa chai,kumiminiwa chai na anawekewa sukari baba na mama wanaona ni haki.
Mtoto wa kike anasoma kidato cha nne anatumia IPhone 6 ,baba anatumia Techno ,mama anatumia Techno, mtoto anaongea na simu usiku kucha ,hakuna anayehoji simu kapata wapi,na pesa ya kununua airtime anapewa na nani?
Wazazi huwa wanahoji mimba ya nani na sio simu kakununuliwa na nani?Mabinti wanapenda kusema,"Nataka mwanaume mrefu aliyejazia "baba yake mfupi na ana kitambi ,mama yako sio mjinga binti.
Wanaume wanapenda kuoa mwanamke mwenye kazi nzuri na elimu nzuri ,baba yako hakuwa mjinga kuoa mama yako darasa LA saba na yupo kwenye ndoa miaka 40 na hakuna picture ya anniversary ya ndoa miaka 40 kwenye social media.
Vijana ambao hamjaoa wala kuolewa ,kigezo cha mke/mume mwema ni akili yake na sio elimu yake. Mungu humpa mtu kilicho bora.
Tujifunze kulea watoto kwa adabu,unyenyekevu na nidhamu na kukemea na kuadhibu kwa haki,tusijifiche mwenye kivuli cha kazi na ubusy.Binti anayefuliwa chupi miaka 10 anawezaje kuwa mke mwema?
Jiulize ni ni mara ngapi umeosha vyombo na binti yako? Ni mara ngapi umefanya usafi wa mazingira ya nyumbani na wanao? Ni Mara ngapi umemwambia mwanao baba/mama yako ni mtu bora kwangu na kwako?
Tafakari – tutavuna tunachokipanda.
Mkuu kwa kweli nashindwa niongee nini mana wadau tayali wameshaongea uko mwanzo, yote kwa yote nitoe tu wito kwa wazazi tujitaidi sana kwenye malezi ya watoto wetu embu tujiulize kama hali ipo hivi wakat huu je huko mbele hali itakuwaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NImependa namna ulivyojiuliza ... nafikiri tukipata jibu la swali lako litakuwa suruhisho.
 
Kibongobongo mtoto ni wa mama. Ki biblia mtoto ni wa baba.

Ewe mkristu soma hiyooooooo
 
Namaanisha akivaa kihuni ile kata k ya kihuni kabisa. Kwako ni sahihi kwasababu ni mtoto wa kiume? Itasaidia nini kumuweka mtoto wa kike katika maadili hlf wa kiume aachwe?
Ndio maana hata wasichana wenye tabia njema wanashindwa ndoa kwasababu ya kuolewa na wanaume wasio na maadili. Huwezi kuwekeza adabu kwa mtoto wa kike peke yake hlf ukategemea mambo yaende sawa. Haipo hivyo!
Dada yangu; ina maana ulitaka nitoe mifano yote ya upotokaji wa maadili kwa vijana wetu? Mimi nilitoa kwa upande wa mabinti; nilitegemea wewe uongeze na sio kuonesha kana kwamba unawatetea. Kiujumla maadili kwa vijana yameporomoja na kinachosababisha ni malezi.
 
Unavyosema hauruhusu mwanao alelewe na house girl ni sawa lakini haiwezekani kwa watu wengi maana wake nao wana majukumu ya kutafuta pesa. Hiyo itawezekana tu Kama mke hana shughuli nje ya nyumbani.
Kuhusu shule bado zipo shule ambazo Kuna kazi za mikono nyingi tu na pia mtoto akirudi nyumbani anafanya kazi Kama kawaida na house girl yupo.
Ndio maana nikakuambia inategemea na malezi. Mimi nimeishi maisha ya kulelewa na house girl lakini kazi zote nimefanya, mama yetu hakutuacha tubweteke kwasababu Kuna msichana wa kazi.
So jinsi tu unavyomlea, house girls hawana tatizo wakiwepo.
Nakubaliana na wewe kwenye hilo; lakini wazazi wengi wanawadekeza watoto.
Kuhusu shule zenye kazi za kujitegemea .. kama zipo labda .... sijui ...
Naangalia hapa nilipo jijini Mwanza;
Ni shule ipi yenye shamba?
Ni shule ipi yenye mradi wa nguruwe, ng'ombe, kuku n.k
Ni shule ipi ina mradi wowote ambao vijana wanaenda kujifunzia?
Nakumbuka shuleni kwetu (sekondari) kulikuwa na shamba kubwa; na bado kulikuwa na m ifugo ambapo wanafunzi tulipangiwa zamu za kuhudumia hiyo mifugo.
Tusidanganyane hiyo haipo tena.
 
Kama nimekuelewa vile.umegusa ukweli uliyopo hakika hii itakuwa Post Bora sana...
 
Umeongea kitu kikubwa sana mie naona tuache lawama za kusukumiana mzigo na familia ilelewe na wazazi wote kuepukana na majuto ya badae maana unaweza mtegemea mwanamke na ukakuta yeye anaishi kisasa so ni bora baba kama kichwa cha familia ukashika usukani wa malezi maana aibu ikurudi itawarudia watoto wa baba na mama fulani haitamwacha mtu salama
Ukweli wanawake wa sasa hivi wengi wao tunaishi maisha ya maigizo sana tunazalisha kizazi cha ajabu muhimu ni kinababa mrudi kama vichwa vya familia sio kazi kurudi nyumbani usiku mkubwa na kuondoka ( nakumbuka zamani kuna nyumba huingii ukisikia baba yao kaja kwanza anawashikisha majembe + mafyekeo ni kulima bustani huko njee kukata michongoma na kazi nyingine) tofauti na wababa wa siku hizi wakirudi anachukua watoto wanakaa kuangalia movie mara music mara game ndio ni nzuri lakini je unawafundisha kazi nyingine za nyumbani
 
Educative thread even tho' the decision of caring kids should be not to women/wives only.
 
Kama nimekuelewa vile.umegusa ukweli uliyopo hakika hii itakuwa Post Bora sana...
Tuendelee kushauriana kwa yaliyo mema badala ya kujadili yale ya sirini.
 
Umeongea kitu kikubwa sana mie naona tuache lawama za kusukumiana mzigo na familia ilelewe na wazazi wote kuepukana na majuto ya badae maana unaweza mtegemea mwanamke na ukakuta yeye anaishi kisasa so ni bora baba kama kichwa cha familia ukashika usukani wa malezi maana aibu ikurudi itawarudia watoto wa baba na mama fulani haitamwacha mtu salama
Ukweli wanawake wa sasa hivi wengi wao tunaishi maisha ya maigizo sana tunazalisha kizazi cha ajabu muhimu ni kinababa mrudi kama vichwa vya familia sio kazi kurudi nyumbani usiku mkubwa na kuondoka ( nakumbuka zamani kuna nyumba huingii ukisikia baba yao kaja kwanza anawashikisha majembe + mafyekeo ni kulima bustani huko njee kukata michongoma na kazi nyingine) tofauti na wababa wa siku hizi wakirudi anachukua watoto wanakaa kuangalia movie mara music mara game ndio ni nzuri lakini je unawafundisha kazi nyingine za nyumbani
Ndiyo maana lawama yangu namba moja ilikuwa kwenye tech! Nimekuelewa vizuri sana Sonia G
 
Nadhani mtoa post watakao kuelewa kwa wingi ni wanawake wa mikoani,%kubwa watu wa mijini wanasingizia kazi na kukwepa majumu yao na muda mwingi wanatumia wakiwa katika mitandao ya kijamii na malezi ya watoto anaachiwa dada wa kazi,kwa hili naungana na mtoa uzi nazaidi upande was akina mama badilikeni

Uko powa!
Wa mijini (wanawake) ukijaribu kuwatreat inavyotakiwa wanakimbilia kwenye taasisi za kutetea haki zao. Hizi taasisi zimekaa kimasilahi zaidi. Tujue wazi kwamba tunakokwenda sio kwema.
 
Back
Top Bottom