UKWELI MCHUNGU

UKWELI MCHUNGU

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,614
UKWELI MCHUNGU ...
Akili.jpg
Nyakati na Technology zimeharibu mambo mengi sana Tanzania.Wanawake wenye akili wasio na elimu walizaa na kulea ma Professors. Nyakati hizi wanawake wasomi wanashindwa kuzalisha vizazi bora vya watoto wenye adabu,hekima na maarifa. Nyakati hizi mwanamke jinsi anavyozidi kuelimika ndivyo anavyozidi kupoteza vinasaba maridhawa vya mke mwema na mama bora.

Uadilifu,unyenyekevu,lugha nzuri ni majukumu ya mwanamke kwa mume kwa sasa imekuwa misamiati kwa asilimia kubwa kwa wanawake wasomi wenye ndoa zao.
Mzazi anafurahia mtoto kuzungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha, lakini mtoto hana adabu, ni mjeuri na mwenye kiburi, social media wazazi tunapost picture za watoto wetu kwa ubora wa mavazi na uzuri wa sura lakini hatujivunii haiba na tabia njema za watoto.

"She is my happiness" mwingine utasikia "He is my handsome" lakini mtoto anamjua vyema house girl kuliko Mama.Wengi wamejificha kwenye kazi inachukua muda wangu mwingi nashindwa kukaa na mwanangu.
Wengine tumelelewa na wazazi ma -Nurse anaingia night lakini,tulisoma na kuimba table ya 1-12 ndipo tulipewa ruhusa ya kwenda kucheza,tulifundishwa kufua na kupiga pasi na bado mzazi alikuwa busy na kazi.

Mtoto ni wa mama, mama akikosa busara na hekima ya kulea watoto anaharibu kizazi chake,ukweli mchungu Tanzania divorce rate kubwa ni ya wanawake wasomi na wanaume wasomi,ndoa za watu ambao sio wasomi kuna ushirika na upendo mkubwa sana.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya mwanamke mwenye akili asiye na elimu na mwanamke mwenye elimu asiye na akili.

Busara ina unyenyekevu, uvumilivu, adabu na utu, wanawake waliokosa busara utawagundua kwa show off na kauli zao. Jiulize mtoto wa kike wa miaka 8 anafuliwa chupi,anaandaliwa chai,kumiminiwa chai na anawekewa sukari baba na mama wanaona ni haki.
Mtoto wa kike anasoma kidato cha nne anatumia IPhone 6 ,baba anatumia Techno ,mama anatumia Techno, mtoto anaongea na simu usiku kucha ,hakuna anayehoji simu kapata wapi,na pesa ya kununua airtime anapewa na nani?
Wazazi huwa wanahoji mimba ya nani na sio simu kakununuliwa na nani?Mabinti wanapenda kusema,"Nataka mwanaume mrefu aliyejazia "baba yake mfupi na ana kitambi ,mama yako sio mjinga binti.
Wanaume wanapenda kuoa mwanamke mwenye kazi nzuri na elimu nzuri ,baba yako hakuwa mjinga kuoa mama yako darasa LA saba na yupo kwenye ndoa miaka 40 na hakuna picture ya anniversary ya ndoa miaka 40 kwenye social media.
Vijana ambao hamjaoa wala kuolewa ,kigezo cha mke/mume mwema ni akili yake na sio elimu yake. Mungu humpa mtu kilicho bora.
Tujifunze kulea watoto kwa adabu,unyenyekevu na nidhamu na kukemea na kuadhibu kwa haki,tusijifiche mwenye kivuli cha kazi na ubusy.Binti anayefuliwa chupi miaka 10 anawezaje kuwa mke mwema?
Jiulize ni ni mara ngapi umeosha vyombo na binti yako? Ni mara ngapi umefanya usafi wa mazingira ya nyumbani na wanao? Ni Mara ngapi umemwambia mwanao baba/mama yako ni mtu bora kwangu na kwako?
Tafakari – tutavuna tunachokipanda.
 
"Times do change, and so is every thing"
Nadhani mabadiliko ya nyakati yamebadilisha mambo meengi saana sio tu malezi na makuzi ya watoto wetu, lakini pia hata mahusiano ya mtu na mtu au jamii na jamii yamebadilika pia..

Nyakati zinakwenda mbio na vipaumbele vya binadamu wote sio tu wanawake ni kwenye kukimbizana na ulimwengu huu wa kibepari. Kuna yanayoweza kuepukika na kuna ambayo hatuwezi yaepuka, pesa kwa mfano ni lazima itafutwe ili hawa "watoto" wapate mahitaji muhimu.

Inawezekana kweli kuna kauzembe katika baadhi ya maeneo au nyanja za kimalezi, lakini pia "kauzembe" haka kanaweza kasiwe ka makusudi.

Pia suala la malezi kwa ulimwengu wa leo si la kumuachia mama au mwanamke peke yake bali ni suala la kushirikiana bega kwa bega sababu nyakati zimebadilika na kila kitu pia kimebadilika..
 
Unawaongelea hawa mama zetu?
 
Unaelewa nini kuhusu mgawanyo wa kazi / mgawanyo wa majukumu?
 
Sijajua una umri gani; yawezekana ninaowaongelea ni mabinti zetu au bibi zetu.
35 - 40 nipo hapo kati. Nahusika au unamuongelea mwenye umri wa Mama yangu?
 
Wewe unahusika, kwa vyovyote watoto wako wako primary na secondary. Unaonaje mienendo yao?
 
Unaelewa nini kuhusu mgawanyo wa kazi / mgawanyo wa majukumu?
Ni kweli kabisa mkuu mgawanyo wa majukumu kati ya baba, mama na watoto umekuwapo tangia enzi za wahenga wetu. Katika zama hizo ilikuwa ni aghalabu sana kukuta mama akifanya majukum ya kiume (kama yalivyokuwa yanaaminika) vile vile baba hakuweza fanya yale ya mama.

Katika ulimwengu wa leo ni kawaida kukuta mama ndio "bread winner" ndani ya familia na baba hana hata kipato na hakuna anayeshangaa.
kifupi ndio maana nilisema mabadiliko ya muda na kila kitu ndio chanzo cha kila kitu. Ifike wakati tupime umuhimu wa mgawanyo huu wa majukum kama una faida chanya au hasi katika ulimwengu wa sasa.

Je mgawanyo huu (ambao na mimi ni muumin wake) unatupeleka kwa kasi tuitakayo kule tuendako??
 
Wewe unahusika, kwa vyovyote watoto wako wako primary na secondary. Unaonaje mienendo yao?
Mienendo inatokana na malezi unayompa, pia zama zinabadilika watu wanaelimika kuliko ilivyokuwa zamani. Watoto wa kike wamepewa elimu na ndio iliyowafanya wabadilike.
Unavyosema asiyesoma anakuwa mke mwema may be upo sahihi lkn je tuache kuwasomesha watoto wetu wa kike? Jibu ni kwamba haiwezekani..tukubaliane na matokeo hatuwezi kurudi nyuma.
 
Ni kweli kabisa mkuu mgawanyo wa majukumu kati ya baba, mama na watoto umekuwapo tangia enzi za wahenga wetu. Katika zama hizo ilikuwa ni aghalabu sana kukuta mama akifanya majukum ya kiume (kama yalivyokuwa yanaaminika) vile vile baba hakuweza fanya yale ya mama.

Katika ulimwengu wa leo ni kawaida kukuta mama ndio "bread winner" ndani ya familia na baba hana hata kipato na hakuna anayeshangaa.
kifupi ndio maana nilisema mabadiliko ya muda na kila kitu ndio chanzo cha kila kitu. Ifike wakati tupime umuhimu wa mgawanyo huu wa majukum kama una faida chanya au hasi katika ulimwengu wa sasa.

Je mgawanyo huu (ambao na mimi ni muumin wake) unatupeleka kwa kasi tuitakayo kule tuendako??
Nimekuelewa ila ...
Tatizo ni kwamba mabadiliko haya yanaingiza mambo hasi zaidi ya chanya.
Mfano mdogo tu, zamani - enzi zetu ilikuwa marufuku mtu kucheza kamali adharani ... leo hii kampuni za kamali zinaweka matangazo kila sehemu. Hivi ni sahihi kupokea mabadiliko ya namna hii?
Ilikuwa nadra sana kuona nguo ya ndani ya binti - leo hii tunayaona ya kawaida tu kwenye daladala hadi makanisani - hiyo ni sahihi?
Kwa ujumla kuna vitu ambavyo mama anapaswa kuplay part yake. Mimi nikimuona binti yangu amevaa nguo inaonesha nguo ya ndani wala simuulizi yeye - ugomvi mkubwa utakuwa kwa mama yake.
 
Mtoto wa kiume akionyesha nguo yake ya ndani utamlaumu mama pia?
 
Mienendo inatokana na malezi unayompa, pia zama zinabadilika watu wanaelimika kuliko ilivyokuwa zamani. Watoto wa kike wamepewa elimu na ndio iliyowafanya wabadilike.
Unavyosema asiyesoma anakuwa mke mwema may be upo sahihi lkn je tuache kuwasomesha watoto wetu wa kike? Jibu ni kwamba haiwezekani..tukubaliane na matokeo hatuwezi kurudi nyuma.
Kwenye bold - Uko sawa kabisa ...
Kama unamwambia akuimbie wimbo wa Diamond ni lini atajua 7 x 7?
Kama mfanyakazi anafanya kila kitu hapo nyumbani ni lini atajua kazi za nyumbani?
Shule anayosoma ni bweni na huko hakuna kazi yoyote wanayofundishwa zaidi ya kusoma - akirudi mtaani unategemea atafanya nini?
Nakumbuka ... mimi nilifundishwa kusoma na kuandika na mama yangu. Mama anafundisha vizuri kwa upendo na upole ... mambo ya muhimu unamwachia housegirl + walimu? Hawa wako kipesa zaidi.
Kuna mengi nilijifunza baada ya kupata mtoto wangu wa kwanza - -baada ya hapo sikuruhusu hata siku moja watoto wangu walelewe na housegirl. Naandika haya nina uchungu. Nidhamu hakuna tena.
 
Mtoto wa kiume akionyesha nguo yake ya ndani utamlaumu mama pia?
Labda wewe umezaliwa mjini ... nguo ya ndani ya mtoto wa kiume hata enzi zetu ilikuwa kawaida. Tena huko vijijini ilikuwa hata tako la mtoto wa kiume kuchungulia kwenye matobo ya kaptula ilikuwa kawaida tu.
 
Namaanisha akivaa kihuni ile kata k ya kihuni kabisa. Kwako ni sahihi kwasababu ni mtoto wa kiume? Itasaidia nini kumuweka mtoto wa kike katika maadili hlf wa kiume aachwe?
Ndio maana hata wasichana wenye tabia njema wanashindwa ndoa kwasababu ya kuolewa na wanaume wasio na maadili. Huwezi kuwekeza adabu kwa mtoto wa kike peke yake hlf ukategemea mambo yaende sawa. Haipo hivyo!
 
Kwenye bold - Uko sawa kabisa ...
Kama unamwambia akuimbie wimbo wa Diamond ni lini atajua 7 x 7?
Kama mfanyakazi anafanya kila kitu hapo nyumbani ni lini atajua kazi za nyumbani?
Shule anayosoma ni bweni na huko hakuna kazi yoyote wanayofundishwa zaidi ya kusoma - akirudi mtaani unategemea atafanya nini?
Nakumbuka ... mimi nilifundishwa kusoma na kuandika na mama yangu. Mama anafundisha vizuri kwa upendo na upole ... mambo ya muhimu unamwachia housegirl + walimu? Hawa wako kipesa zaidi.
Kuna mengi nilijifunza baada ya kupata mtoto wangu wa kwanza - -baada ya hapo sikuruhusu hata siku moja watoto wangu walelewe na housegirl. Naandika haya nina uchungu. Nidhamu hakuna tena.
Unavyosema hauruhusu mwanao alelewe na house girl ni sawa lakini haiwezekani kwa watu wengi maana wake nao wana majukumu ya kutafuta pesa. Hiyo itawezekana tu Kama mke hana shughuli nje ya nyumbani.
Kuhusu shule bado zipo shule ambazo Kuna kazi za mikono nyingi tu na pia mtoto akirudi nyumbani anafanya kazi Kama kawaida na house girl yupo.
Ndio maana nikakuambia inategemea na malezi. Mimi nimeishi maisha ya kulelewa na house girl lakini kazi zote nimefanya, mama yetu hakutuacha tubweteke kwasababu Kuna msichana wa kazi.
So jinsi tu unavyomlea, house girls hawana tatizo wakiwepo.
 
Back
Top Bottom