Ndio maana tunataka tuwaone kwani ni sisi tumewachagua ....acheni uwehu wa kujitakia.....aliekwambia kwamba kuna mwanasiasa abaesimamia maslah yako gizani ni nani?Hawa wabunge wetu ukichunguza sana hawasimamii maslahi ya wananchi bali wanasimamia matakwa yao binafsi. Wala wabunge wetu hawa si sauti yoyote ya wananchi waliowachagua. Idadi kubwa ya watanzania ni maskini wanaohangaikia kupata angalau mlo mmoja kwa siku. Watawezaje kuwatuma wabunge wao wakashupalie bunge lionyeshwe live wakati wa kazi za kujitafutia huo mlo mmoja? Enyi wabunge wetu hebu shupalieni ya maana kwa manufaa ya wananchi waliowapeleka bungeni. Eti wabunge wanataka waonekane bungeni wanavyoisimamia serikali! Wanaisimamia serikali kwa kuikwamisha ktk juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo yanayostahili? Ooh sijui sheria, haki za binadamu nk nk. Wananchi watashiba sheria? Waangalie hali halisi ya nchi na wasaidie katika juhudi zinazofanywa na Serikali za kuirejesha nchi mahali inapostahili kuwa. Tena kama kweli hao wapinzani wana nia njema ya kutaka kuwakwamua wananchi kutoka kwenye lindi la umaskini wangelegeza ama wangerekebisha baadhi ya sheria kuisaidia serikali badala ya kung'ang'aniza sheria zinazoikwamisha serikali na kufifisha matumaini ya hali bora kwa wananchi walio wengi.
Bunge la Tanzania ni chafu, linanuka rushwa, limejaa majipu kama ilivyo bandari, na halshamauri. Kwa ajili hiyo linatakiwa litumbuliwe majibu halafu ndio tuanze kuongea maana ya mihimili. Wananchi wamechoka ni kiini macho cha kuuza sura.
Kwani TBC ina kazi gani labda? Maana ipo ipo tu na inahudumiwa na kodi zetu......
Kwanini kipindi cha uwajibikaji wa serikali ndio bunge lifichwe?
Mafichoni kuna nini?
Kuna mzee mmoja hapa aliwah sema wanataka kuturoga...hoja za kutaka kubana matumizi ni mufilis.......
Imeku touch eh? Pole sana!N
Ndio maana tunataka tuwaone kwani ni sisi tumewachagua ....acheni uwehu wa kujitakia.....aliekwambia kwamba kuna mwanasiasa abaesimamia maslah yako gizani ni nani?
Acheni unafiki.
Umenifurahisha mkuu. Hawa wabunge chenga tu nao, wapo kwaajili ya maslahi yao tu na si vinginevyo.Wabunge ni wawakilishi wetu. Sisi tumewaamini na kuwachagua wakatuwakilishe kuisimmamie na kuibana serikali kwa manufaa yetu. Sisi tunasubiri matunda tu (results) na siyo kuona mchakato walilotumia. Kama hatuwaamini na wanachokifanya huko bungeni ni sisi siyo wao ndiyo tungetaka tuwaone live wanachotuwakilisha kule. Sisi hatujalalamika kwa kuwa tunawaamini. Cha ajabu wao ndio wanalalamika eti tuache shughuli zetu tuwaangalie wanavyotuwakilisha. Na kama hawaonyeshwi wanasusa vikao.
Halafu chadema ndiyo wanafanya liwe chafu.Bunge la Tanzania ni chafu, linanuka rushwa, limejaa majipu kama ilivyo bandari, na halshamauri. Kwa ajili hiyo linatakiwa litumbuliwe majibu halafu ndio tuanze kuongea maana ya mihimili. Wananchi wamechoka ni kiini macho cha kuuza sura.
Hapo penye hoja namba 1 kwenye post yako ambapo umeuliza swali, nami nalinukuu:-Kimsingi, Dola inakua na mihimili mitatu, yaani Bunge, Serikali na Mahakama..
Kwa vile Ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Tanzania 1977(Kama ilivyorekebishwa mara kwa mara) inasema mamlaka ya nchi yapo chini ya wananchi, Bunge ni mhimili muhimu sana kwasababu unawakilisha Sauti ya mamlaka halisi ya wananchi...
Moja kati ya kazi muhimu ya Bunge ni kuisimamia na kuikosoa Serikali ili ihakikishe inaweka maslahi ya wananchi mstari wa mbele...
Katika kulinda Uhuru na Haki za Bunge kufanya kazi yake vizuri, Bunge linajisimamia na linakua Bajeti yake huru(Kama ni msaada utakua ni kidogo sana kutoka kwa serikali)..
Bunge ni chombo huru..
Miezi kadhaa iliyopita, tulisikia TBC ikitangaza kwamba, inasitisha kurusha matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni(Live) kutokana na kile wanachokiita ukosefu wa pesa ya kurushia matangazo hayo, Tukumbuke kua TBC ni stesheni ya serikali, Mhimili mwingine kabisa wa dola, mhimili ambao Bunge lina kazi ya kuusimamia na kuukosoa...
Bila kujali kwamba maamuzi hayo ya serikali yalikua ni ya kisiasa au la, kuna maswali kadhaa ya kujiuliza;
1. Je, Bunge lenye bajeti yake inayojitegemea linashindwaje kutenga bajeti ya kuanzisha kituo cha kurushia matangazo yake moja kwa moja bila kutegemea favor kutoka kwa serikali?
2. Bunge ni mhimili ambao waliomo ni moja kati ya watu wanaopokea mishara na posho nono za kutisha, wabunge(kama kweli wanataka wananchi wao tuone wanavyofanya kazi zao vema) wanashindwaje kukata posho hizo na kuanzisha utaratibu wa kuanzisha kituo?
3. Kwa nature ya kazi za bunge(kuisimamia) serikali, walikua wanategemea nini kama sio hiki kinachoendelea?
4. Bunge linaendeshwa kwa kodi zetu, na serikali inaendeshwa kwa kodi zetu, Bunge kutegemea fedha za serikali halioni kua lina-parasite kodi za wananchi kote kote?
5. Bunge halioni kua kuendelea kuitegemea serikali kwenye matangazo ya live litashindwa kuiwajibisha serikali vizuri?
Wananchi Hatuungi mkono kitendo cha serikali kwa upande mmoja, lakini kwa upande mwingine, tunaunga mkono kwasababu Bunge lilinde uhuru wake kwa kuweza kujitegemea, (ni mfano wa baba anapomfukuza nyumbani mwanawe wa kiume aliyefika umri wa kujitegemea akapambane atengeneze maisha yake.)
Vile vile tukija kwenye kile wanachokiita uvunjifu wa Haki ya kupata Habari ni kweli inawezekana serikali wamevunja Haki hiyo, lakini Haki hiyo ni moja kati ya Haki ambazo utekelezaji wake unategemea rasilimali za nchi husika, Serikali inaweza kabisa ikajitetea kua imeshindwa kufanya hivyo kwasababu ya ufinyu wa bajeti yake!
Suluhisho pendekezwa:
Bunge lianzishe kituo chake cha kurushia matangazo ya moja kwa moja, kama zilivyo nchi zingine, mfano Uingereza.. Parliamentlive.tv - Commons... na liache kulia lia. Bunge lijitegemee ili liisimamie serikali vizuri.
Wabunge ni wawakilishi wetu. Sisi tumewaamini na kuwachagua wakatuwakilishe kuisimmamie na kuibana serikali kwa manufaa yetu. Sisi tunasubiri matunda tu (results) na siyo kuona mchakato walilotumia. Kama hatuwaamini na wanachokifanya huko bungeni ni sisi siyo wao ndiyo tungetaka tuwaone live wanachotuwakilisha kule. Sisi hatujalalamika kwa kuwa tunawaamini. Cha ajabu wao ndio wanalalamika eti tuache shughuli zetu tuwaangalie wanavyotuwakilisha. Na kama hawaonyeshwi wanasusa vikao.
Wabunge ni wawakilishi wetu. Sisi tumewaamini na kuwachagua wakatuwakilishe kuisimmamie na kuibana serikali kwa manufaa yetu. Sisi tunasubiri matunda tu (results) na siyo kuona mchakato walilotumia. Kama hatuwaamini na wanachokifanya huko bungeni ni sisi siyo wao ndiyo tungetaka tuwaone live wanachotuwakilisha kule. Sisi hatujalalamika kwa kuwa tunawaamini. Cha ajabu wao ndio wanalalamika eti tuache shughuli zetu tuwaangalie wanavyotuwakilisha. Na kama hawaonyeshwi wanasusa vikao.