Ujumbe murwa kabisa kwa kina baba fulani na kina mama fulani, malezi bora hayanunuliwi hutengenezwa na walezi/wazazi, kumnunulia mtoto nguo za thamani, michezo, shule za gharama hazitoshi kukamilisha malezi bora.
Tumia muda kukaa na watoto ujue mienendo yao, nini wanataka, wafahamu uwepo wa baba na mama, kwa kufanya hivyo utakuwa umetimilisha wajibu wako kama mzazi bora.
Watoto wanapobadilika tabia na kuharibikiwa kitu cha kwanza mzazi kulalamika ni gharama anazotumia kumlea mtoto, ""Yani nahangaika kazini ili msome shule nzuri....."" baadhi ya malalamishi.
Ewe mzazi jenga mazoea ya kuyaishi maisha ya uzazi halisi.
Tafakari chukua hatua.
Dah..... Hii dunia kuna wanasayansi jamii....wanasayansi maumbo....wanasayansi uchumi...wanasayansi siasa.....ukiwasikiliza wote utaishiwa kuchanganyikiwa.....Pambana na hali yako[emoji13] [emoji13] [emoji87]