Ukweli mchungu hatuwezi kuendelea tukiwa chini ya wanasiasa

Siansa ni biashara, na malengo ya biashara siku zote ni kupata faida na siyo hasara. Kila anayeunga mkono au kukosoa utawara flani, anayo masilahi binafsi ya kufanya hivyo.

Anayeunga mkono, aidha ananufaika kwa namna moja ama nyinge, pia anayepinga huenda mfumo umemkataa, na unashindwa kuwa na manufaa kwake, hivyo anajaribu kutafuta sehemu ya kupumulia.

Ukweli ni kwamba, hakuna binadamu anayepigana vita kwa ajiri ya mtu au masilahi ya watu wengine. Ndugu zangu WATANZANIA tutaendelea na kufanikiwa, endapo tutaachana na utumwa na Ung'ombe tuliopewa na wanasiansa...
Hii falsafa ya kuwatumia hawa wanaoitwa 'wanasiasa' nadhani ni mojawapo ya falsafa mbovu kabisa za utawala/uongozi kuwahi kubuniwa na binadamu. Fikiria, watu milioni 70 tunakabidhi akili zetu, maono yetu na juhudi zetu kwa Samia ili atufikishe kwenye nchi ya ahadi. Ni jambo la kuchekesha, lakini pia ni upuuzi mtupu.
 
Bado kipo kwenye mchakato wa kisheria, ila ningependekeza ujishikize kwanza CHADEMA kwa muda, kikiwa tear nitakupatia taarifa...
Kwa mara ya kwanza napokea kadi ya Chama nilikabidhiwa na Dr Slaa, baada ya Mbowe kuingiza tamaa ya pesa Chadema ilikufa na Dk Slaa, kwa sasa Chadema sio tena chama cha siasa, chadema ya sasa ina operate mithili ya Muslim Brotherhood. Utanisamehe kwa maneno yangu.
 
Uongozi na viongozi ni jambo lisilokwepeka pale mnapokuwa kwenye kundi la watu. Elimu yetu ni majanga ndiyo maana inatoa watu wanaofikiria kwa kukata tamaa. Ulichotakiwa kusema ni kuwa wananchi wanatakiwa wawakalie viongozi kooni muda wote ili kuhakikisha wanafanya kila kinachotakiwa. Tatizo la watanzania ni kudhani ukishagua kiongozi basi wewe unarudi nyumbani kukunja nne na yule kiongozi atatekeleza yote aliyoahidi. Treat viongozi kama shamba, ambalo huwa linahitaji uangalizi muda wote. Nakuapia hata hawa hawa CCM kama sisi wananchi tungekuwa tunajitambua, wangefanya vizuri sana just kwa kuwakalia kooni.
Hoja yako ni nzuri, lakini je hujasikia walio jaribu kuwakalia kooni wametekwa wengine wamepotezwa?...
 
Kwa mara ya kwanza napokea kadi ya Chama nilikabidhiwa na Dr Slaa, baada ya Mbowe kuingiza tamaa ya pesa Chadema ilikufa na Dk Slaa, kwa sasa Chadema sio tena chama cha siasa, chadema ya sasa ina operate mithili ya Muslim Brotherhood. Utanisamehe kwa maneno yangu.
Ni haki yako kuamini unacho kiamini, huu ni uongozi wa Tundu Lissu si Mbowe, ni wakati wa kulejea utazamie upepo mpyaa...
 
Hoja yako ni nzuri, lakini je hujasikia walio jaribu kuwakalia kooni wametekwa wengine wamepotezwa?...
TAtizo tunategeana kuwakalia kooni, wengine wamekaa wanakuna mbupu huku wanasubiri kuona Lissu anapelekewa moto peke yake. Wakisha share vile visimulzi vya matukio ya mahakama basi nao wanajihisi wamemaliza kazi
 
Hii ni kweli kabisa, Watanzania tunahitaji Tiba hakika...
 
Kama mfumo uliopo hauleti viongozi bora unashauri njia ipi itumike kuundoa mfumo uliopo na kuuweka mfumo madhubuti wa kuleta viongozi bora ?
Watanzania bado hawajawa tayari kupata viongozi bora, bado wanaridhishwa na utawala uliopo na hawaoni shida..ushahidi ni idadi ya ng'ombe wanaosombwa Kwa malori kwenda mikutanoni..na maelfu ya bodaboda wanaosindikiza misafara ya watawala waliopo...
 
Tundu Lissu kwa aina ya siasa zake ni ngumu kutoboa kibongo bongo.
Imani ndiyo msingi wa yote, binafsi tangu utoto wangu nilikua ni mshabiki mkubwa wa ccm, sielewi ni mwaka huu tuu chuki niliyo nayo juu yao sielewi imetoka wapi, sina namna kumunga mkono Tundu Lissu tu hata kama siansa zake ni ngumu kumuelewa.
 
Watanzania bado hawajawa tayari kupata viongozi bora, bado wanaridhishwa na utawala uliopo na hawaoni shida..ushahidi ni idadi ya ng'ombe wanaosombwa Kwa malori kwenda mikutanoni..na maelfu ya bodaboda wanaosindikiza misafara ya watawala waliopo...
Hoja yako izingatiwe tunahitaji ukombozi wa fikra kwanza la sivyo tutangoja sana...
 
Imani ndiyo msingi wa yote, binafsi tangu utoto wangu nilikua ni mshabiki mkubwa wa ccm, sielewi ni mwaka huu tuu chuki niliyo nayo juu yao sielewi imetoka wapi, sina namna kumunga mkono Tundu Lissu tu hata kama siansa zake ni ngumu kumuelewa.
Watz wangekuwa sio wanafki na wanazielewa Siasa za Lissu wasingekubali kumuacha ateseke peke yake huko mahabusu.
 
Watanzania bado hawajawa tayari kupata viongozi bora, bado wanaridhishwa na utawala uliopo na hawaoni shida..ushahidi ni idadi ya ng'ombe wanaosombwa Kwa malori kwenda mikutanoni..na maelfu ya bodaboda wanaosindikiza misafara ya watawala waliopo...
Kuna watu wanawalaumu ccm kusomba watu ila Mimi nasema hawa watu wangekuwa wanajitambua wasingekubali kusombwa. Sasa kama wapo watu wanaokubali kusombwa unategemea hawa watu wasitiki ikifika Oktoba ?
 
Siansa ni biashara, na malengo ya biashara siku zote ni kupata faida na siyo hasara. Kila anayeunga mkono au kukosoa utawara flani, anayo masilahi binafsi ya kufanya hivyo.

Anayeunga mkono, aidha ananufaika kwa namna moja ama nyinge, pia anayepinga huenda mfumo umemkataa, na unashindwa kuwa na manufaa kwake, hivyo anajaribu kutafuta sehemu ya kupumulia.

Ukweli ni kwamba, hakuna binadamu anayepigana vita kwa ajiri ya mtu au masilahi ya watu wengine. Ndugu zangu WATANZANIA tutaendelea na kufanikiwa, endapo tutaachana na utumwa na Ung'ombe tuliopewa na wanasiansa...
Wanasiasa wameiharibu nchi yetu Tanzania kwa siasa zao za maji taka,uchawa mwingi, kukosa maono,ushirikina,ulafi wa madaraka,ufisadi,ubinafsi n.k
 
Kuna watu wanawalaumu ccm kusomba watu ila Mimi nasema hawa watu wangekuwa wanajitambua wasingekubali kusombwa. Sasa kama wapo watu wanaokubali kusombwa unategemea hawa watu wasitiki ikifika Oktoba ?
Oktoba hawatiki, kwa sababu nasikia wengine walikuwa nalipwa ili kwenda si kusombwa tu, hata mm ningeenda naachaje furusa kizembe...
 
Wanasiasa wameiharibu nchi yetu Tanzania kwa siasa zao za maji taka,uchawa mwingi, kukosa maono,ushirikina,ulafi wa madaraka,ufisadi,ubinafsi n.k
Upo sahihi ni wakati wa kuamka usingizini sasa...
 
Back
Top Bottom