Ukweli kuhusu Wanamtwara na Lindi kufaidika na gesi

Ukweli kuhusu Wanamtwara na Lindi kufaidika na gesi

Joined
May 20, 2013
Posts
71
Reaction score
151
Ndugu zangu watanzania, Baba wa Taifa hili mwalimu Nyerere alipoamua rasilimali za taifa hili zisichimbwe mpaka pale watanzania tutakapokuwa na weledi na uwezo wa kutosha katika kusimamia zoezi zima la exploitation ya natural resourses kuanzia uchimbaji, process za uongezaji wa thamani hadi kwenye masoko alijua kuwa hapo ndio tutaweza kunufaika. Kama baba wa taifa angekuwa na uchu wa kujinufaisha yeye na waliomzunguka, angeweza kufanya hivyo tena bila hata ya kelele za mtu yeyote maaan hata uelewa wetu ulikuwa mdogo sana, Tena wakati huo vitu vingi vilikuwa vinatolewa bure (siyo rushwa). Mwalimu angeweza hata kuamuru watu waunganishiwe umeme bure majumbani na isingeonekana kama ni rushwa ukilinganisha na ile rushwa waliyopewa watu wa Lindi na mtwara ya kuwaunganishia umeme kwa elfu 90.

Watanzania wenzangu na wana Lindi na mtwara, tusidanganyane, hakuna kufaidika na rasilimali za nchi kama wananchi hawatashiriki katika zoezi zima la uchimbaji. Nisiwafiche mimi nimefanyakazi mgodi wa north mara wa Barrick, Hakuna wananchi wanaozunguka mgodi wanaofaidika na ile dhahabu inayochimbwa pale, kwa sababu hakuna wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wanaoweza kuajirika katika migodi zaidi ya kazi ya ulinzi ambayo hata hiyo nayo makaburu wanaenda kuwachukua makaburu wenzao kutoka A/kusini. Kuna wakati mgodi wa North mara ulikuwa na makaburu walioajiriwa katika maeneo mbalimbali mgodini waliofikia zaidi ya mia tatu (300+). Mpaka walipokuja wakanada wenyewe ndio wakaamuru makaburu wapunguzwe.

Hii nchi ilipofikia saa hizi, bila resistance ya kutosha kama tunayoiona mtwara, rasilimali zote za nchi hii zitaisha bila kuwanufaisha majority ya wananchi wa Tanzania. Kwa hali ya watawala wetu walipofikia saa hizi, hawajali tena watanzania walio wengi katika kunufaika na rasilimali za nchi, wanachojali ni hizo kamisheni wanazozipata na kuzificha uswisi halafu wanawaacha wananchi waliowengi wakiwa kwenye lindi la umasikini. Mipango waliyopanga kuhusiana na gesi ya mnazibay hawajatekeleza wanarukia gesi ya mtwara. Kwa jinsi watawala wetu wanavyoamini katika rushwa wanafikia hadi kuwahonga wananchi wa Lindi na mtwara kwa kuwaunganishia umeme kwa punguzo la bei, wanawachukua wototo wawili watatu na kujifanya wanawasomesha ili wawalaghai wasilete upinzani. Mwisho wa siku kwenye hayo makampuni mtakuta wamejaa makaburu na watu kutoka nje ilivyo kwenye migodi (ambaye haamini hili atafute mtu yeyote aliyeko kwenye migodi ya barrik). Serikali ikilalamikiwa inasema watu wa immigration ndio wanaozembea (kwani immigration iko serikali ya Kenya?)

Kwa mtu yeyote ambaye hajatoka nje ya Tanzania kutembelea nchi nyingine za Afrika zenye mazingira sawa na yetu, anaweza asiamini kuwa tunaweza kufaidika . Mfano mzuri nenda Zambia, Zambia wamejiwekea sheria kuwa hakuna kampuni kutoka nje inayoenda kuwekeza bila kuwa na ubia na kampuni ya ndani. Na katika management lazima wazambia wawepo katika top management. Zambia ni sehemu ngumu sana kwa wageni kufanyakazi, matokeo yake ni kwamba wananchi ndio wanafaika wakubwa kuanzia mwananchi mmoja mmoja kwa ajira, kampuni za ndani katika kusupply bidhaa kwenye migodi, kampuni za ndani katika kupata tenda za migodini, kampuni za kuchimba za wazawa na serikali kupata mapato. Yaani ukienda Zambia ile “multiplier effect “ ya migodi unaiona kwenye miji inayozunguka migodi. Kuna wakati Ndola ikifika mwisho wa mwezi migodini wamelipwa hela zao wafanyakazi na makampuni yanayosupply, ukienda kwenye maduka ya kubadilishia fedha, unaambiwa kwacha hakuna mpaka uende Lusaka. Ile dola ya migodini unaiona inafanyakitu kwenye miji yote inayozunguka migodi.

Bara bara zinazounganisha mikoa ni “dual carriage way” au sisi tunaita barabara mbili. Hapa Tanzania barabara kubwa kama morogoro road inayocollect magari yote ya mikoani na nchi za nje kuingia na kutoka dares salaam “eti” bado ni “single lane”, ndio maana inaongoza kwa ajari. Serikali inajua sababu za ajali ni kwamba madereva wanaovateki kwenye “blackspot” na sababu ni kwamba “The whole segment of morogoro road is an accident blackspot”, traffic volume ni kubwa kuwa handled na single lane. Morogoro road, gari moja bovubovu linaweza kuwapa mnyororo kuanzia kimara mpaka mizani ya kibaha, halafu effect ya jam ika-induce hadi barabara nyingine. Ila kwa sababu za kisiasa serikali inachofanya ni kujaza matraffic police kwaajili ya kuchukua rushwa na kuacha kudeal na core problem. Nimekaa Zambia karibu miezi 8 sijaona ajali za kijinga kama za bongo.

Turudi kwenye mada, Ukweli ni kuwa wananchi wa Lindi na Mtwara hawawezi kufaidika bila kwanza kujengewa shule ili watoto wao wengi waende shule, otherwise watakaofaidika na ajira ni watu wa mikoa mingine ambao walishaenda shule kabla yao. Pili wajasilia mali wazawa wa Lindi na Mtwara wawezeshwe kwa mitaji na utaalamu ili waweze ku-supply mahitaji ya uwekezaji kwa full capacity. Bila hivyo TUSIDANGANYANE mengine yatakuwa ni rushwa au kile alichokiita Tundu lisu ni “kutongozea kura 2015”. Na maandalizi hayo yanahitaji si chini ya miaka 10 at the very least. Kwa hiyo kama wanamtwara na lindi wameamua kupambana kutoka moyoni basi bottom line ni kwamba hiyo gesi isifanyiwe chochote hadi wao wapelekwe shule na maandalizi mengine ya kuwawezesha yafanyike, lakini kusema viwanda vijengwe huko mtwara siyo hoja maana vitajengwa na watabaki watazamaji tu sana sana vitawaharibia mazingira. Watakaoajiriwa ni makaburu na watu wachache kutoka sehemu nyingine za Tanzania. NAOMBA KUWASILISHA
 
Ndugu zangu watanzania, Baba wa Taifa hili mwalimu Nyerere alipoamua rasilimali za taifa hili zisichimbwe mpaka pale watanzania tutakapokuwa na weledi na uwezo wa kutosha katika kusimamia zoezi zima la exploitation ya natural resourses kuanzia uchimbaji, process za uongezaji wa thamani hadi kwenye masoko alijua kuwa hapo ndio tutaweza kunufaika. Kama baba wa taifa angekuwa na uchu wa kujinufaisha yeye na waliomzunguka, angeweza kufanya hivyo tena bila hata ya kelele za mtu yeyote maaan hata uelewa wetu ulikuwa mdogo sana, Tena wakati huo vitu vingi vilikuwa vinatolewa bure (siyo rushwa). Mwalimu angeweza hata kuamuru watu waunganishiwe umeme bure majumbani na isingeonekana kama ni rushwa ukilinganisha na ile rushwa waliyopewa watu wa Lindi na mtwara ya kuwaunganishia umeme kwa elfu 90.

Watanzania wenzangu na wana Lindi na mtwara, tusidanganyane, hakuna kufaidika na rasilimali za nchi kama wananchi hawatashiriki katika zoezi zima la uchimbaji. Nisiwafiche mimi nimefanyakazi mgodi wa north mara wa Barrick, Hakuna wananchi wanaozunguka mgodi wanaofaidika na ile dhahabu inayochimbwa pale, kwa sababu hakuna wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wanaoweza kuajirika katika migodi zaidi ya kazi ya ulinzi ambayo hata hiyo nayo makaburu wanaenda kuwachukua makaburu wenzao kutoka A/kusini. Kuna wakati mgodi wa North mara ulikuwa na makaburu walioajiriwa katika maeneo mbalimbali mgodini waliofikia zaidi ya mia tatu (300+). Mpaka walipokuja wakanada wenyewe ndio wakaamuru makaburu wapunguzwe.

Turudi kwenye mada, Ukweli ni kuwa wananchi wa Lindi na Mtwara hawawezi kufaidika bila kwanza kujengewa shule ili watoto wao wengi waende shule, otherwise watakaofaidika na ajira ni watu wa mikoa mingine ambao walishaenda shule kabla yao. Pili wajasilia mali wazawa wa Lindi na Mtwara wawezeshwe kwa mitaji na utaalamu ili waweze ku-supply mahitaji ya uwekezaji kwa full capacity. Bila hivyo TUSIDANGANYANE mengine yatakuwa ni rushwa au kile alichokiita Tundu lisu ni "kutongozea kura 2015". Na maandalizi hayo yanahitaji si chini ya miaka 10 at the very least. Kwa hiyo kama wanamtwara na lindi wameamua kupambana kutoka moyoni basi bottom line ni kwamba hiyo gesi isifanyiwe chochote hadi wao wapelekwe shule na maandalizi mengine ya kuwawezesha yafanyike, lakini kusema viwanda vijengwe huko mtwara siyo hoja maana vitajengwa na watabaki watazamaji tu sana sana vitawaharibia mazingira. Watakaoajiriwa ni makaburu na watu wachache kutoka sehemu nyingine za Tanzania. NAOMBA KUWASILISHA
Mkuu Heinrich Himmler, siamini kama hii mada, haikuchangiwa na mtu yoyote mpaka leo!. All and all, hii ndio jf yetu!, sasa utashangaa hapa umeeleza mambo ya maana sana, hakuna aliyechangia, ila kupitia ile mada yako hii, [h=3]Harakati za WAMA project against Lowassa [/h]utapata wachangiaji wengi, sio kutokana na hoja zako, no!, bali kutokana na hilo jina "la jamaa yangu" ambalo kwa humu jf kwa sasa ndilo jina kuu kupita yote!.

Pasco
 
Hahahaha Pasco bhana, Jamaa yako kutajwa tu na huyu Jamaa imekufanya kuvamia Profile lake na kucheck activity zake hatimaye ukakutana na hiii..

Anyway kati ya wote ambao hawakuchangia mada hii mmoja wapo ni wewe mwenyewe, sema tushukuru kwa mada aliyokuja nayo this time imekufanya ukatufukunyulie mada hii maridhawa, heko kwa hilo

Jamaa yako tunamtegemea sana ktk "kutupasulia" ccm vipande vipande ktk uchaguzi ujao maana tunahakika kiti cha ugombea hawezi kupewa hata kwa dawa ba tayari tumesikia akihusishwa na yule dogo aliyeondolewa hivi karibuni ndaniw ya cnama chake na wewe kuja hapa jamvini ukisifia eti ni "mzalendo wa kweli ambaye hujapata kumwona", Sasa kwa mwendo huu mambo si mabaya kwa upinzani hapo mwaka kesho.

Na ndiomaana si rahisi kwa Chadema,cuf wala Nccr kukuta wakimshambulia jamaa yako, now kwasababu ya "mategemeo" waliyonayo juuw yake......

Tuendelee kuchochea kuni

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:

Mkuu , asante kwa hii, kiukweli nimekukubali sana, sio tuu una uwezo mkubwa wa kusoma "in between the lines!", pia una uwezo wa kubaini the "the motive behind" na the underlying factors!".

Tukirudi kwa huyu "jamaa yangu!", nakubaliana na wewe, CCM hawawezi wakalogwa kumsimamisha!, hivyo kwa jinsi alivyojiandaa, akijimega, ana meguka na pande nono!, kwangu mimi ni kupitia huyu pekee, ndio angalau kuna matumaini japo kiduchu kwa wapinzani kuingia Ikulu.

Pasco
 
CCM watafute kura za ubunge na uraisi mikoa mingine si Mikoa ya Kusini hili napenda walielewe na mapema sana ,hakuna mwaka ambao wa kusini tutajiandikisha kwa wingi kama mwaka huu ,kama kule Pemba Zanzibar hakuna mbunge wa CCM basi 2015 hakuna mbunge wa ccm wala kura ya raisi kuipa CCM itatokea Mikoa ya Kusini ni haramu kuipa CCM kura hata moja, mmetudhalilisha vya kutosha haijawahi kutokea sehemu yeyote ile hapa Tanganyika tokea tupate Uhuru ,mkoa kupelekewa polisi na majeshi kutesa kwa awamu kisa ,kusema gesi iwanufaishe watu wa kusini kwanza imekuwa kosa basi na iwe kosa vilevile kuikataa CCM.
 
Good analysis mkuu, mungu awape watanzania moyo wa kusoma uchambuzi wa aina hii, pengine uwezo wetu wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi utaongezeka.
 
Mkuu , asante kwa hii, kiukweli nimekukubali sana, sio tuu una uwezo mkubwa wa kusoma "in between the lines!", pia una uwezo wa kubaini the "the motive behind" na the underlying factors!".

Tukirudi kwa huyu "jamaa yangu!", nakubaliana na wewe, CCM hawawezi wakalogwa kumsimamisha!, hivyo kwa jinsi alivyojiandaa, akijimega, ana meguka na pande nono!, kwangu mimi ni kupitia huyu pekee, ndio angalau kuna matumaini japo kiduchu kwa wapinzani kuingia Ikulu.

Pasco

Kwa mwendo huuhuu ulimwamini Six leo umekuwa mpinzani wake...tusubiri tuone
 
Mtu yeyote yule mwenye akili timamu lazima hili limuingie akilini, ila kuna wapuuzi wafulani hivi huwezi kuwaona kuja kuchangia katika jambo nyeti kama hili. Ila kwa mambo ya kipuuzi hukosi kuwaona wakija na matusi na maneno meengi ya utovu wa nidhamu. Ila kwa hili umeona mbali sana Mkuu Heinrich.
 
Tatizo ni malengo ya watawala na matakwa yao...hawana nia njema na nchi hii, wamenia katika tumbo zao na kwa vile wamejiaminisha (kwa kujidanganya) kwamba shida ya watanzania ni tumbo watajarbu kufanya yale ya kutatua mahitaji ya tumbo kwa muda mfupi na hawataki kutizama mbele

Swala la kutoa elimu kwa watanzania lingekuwa moja ya jambo zuri wakati huu wa kutumia rasilimali hii ila hofu ya wezi (watawala) inabaki kwamba wakituelimisha mito yao ya kutunyonya itakauka hivyo hawawezi kamwe kusubiri tuelimike..na hata tukijielimisha katika nyanja hizo hawatatoa nafasi ya kuonyesha uwezo wetu katika maeneo hayo maana tayari mikataba yao na wanyonyaji inawaruhusu wanyonyaji waje na wafanyakazi wao..
 
Mkuu , asante kwa hii, kiukweli nimekukubali sana, sio tuu una uwezo mkubwa wa kusoma "in between the lines!", pia una uwezo wa kubaini the "the motive behind" na the underlying factors!".

Tukirudi kwa huyu "jamaa yangu!", nakubaliana na wewe, CCM hawawezi wakalogwa kumsimamisha!, hivyo kwa jinsi alivyojiandaa, akijimega, ana meguka na pande nono!, kwangu mimi ni kupitia huyu pekee, ndio angalau kuna matumaini japo kiduchu kwa wapinzani kuingia Ikulu.

Pasco

Hii issue ya urais inatutoa sana ufaham, mada hapa ni jinsi ya kufanya ili M kusini afaidike na Gas!! Kwa kifupi ni kwamba ni ngumu sana kuwakomboa hawa ndugu wa Kusini kutokana na mila na tamaduni zao !!
Mosi, wabunge wao wamelala kiasi kwamba Hata hawana Hata priorities! Mfano mzuri ni Mbunge wa Lindi mjini Salim Baruany wa CUF!! WAKATI ANAINGIA MADARAKANI ALIKUWA NA SLOGAN YAKE YA "LINDI KWANZAA VYAMA BAADAYE "Na kwa jinsi anavyojua kuongea, wananchi wakamkubali wakamchagua!
Mara baada ya kuchaguliwa akahama mji kbs!! Hajafanya Hata kitu kimoja kwa ajili ya Jimbo lake!
Watu wa kusini wanahitaji elimu lakini Baruany,kwa miaka mitano alokaa madarakani, huwezi kuamini kwamba hana hata kiwanja cha shule!!
Pili,Baruany hajawahi Hata kutembelea hospital yoyote Ile kutazama kero km Mbunge na kuona namna ya kuzitatua!! Lindi cku hizi wanaoisemea ni kina Lulida (ambao nao upeo wao mdogo,wanapingana na sera nzuri Za maendeleo ili kujipatia umaarufu),Mbunge wa Lindi mjini akiwa amelala, kazi yake kubwa kudandia hoja!!
Tatu, hajajenga Hata zahanati moja!Lakini amejenga Guest House Nzuri tena kaujengea Mchepuko kwa jina la RAHMA GUEST HOUSE!!
Nne,huyu jamaa Baruany ni mwongo sana!!WAKATI wa campaign zake aliwaahidi vijana kwamba atawapatia mikopo ya bei nafuu na kuongea na banks ili masharti ya mikopo yapunguzwe, akiulizwa jibu lake ni kuvuta subra! #
Tano, huyu jamaa anawadanganya Watu kwamba maji yanayosambazwa Lindi mjini ni kwa nguvu zake! Tunajua maji haya ni ahadi ya Rais Kikwete alipokuwa anapiga campaign Za urais pale Uwanja wa Ilulu!!
Ninashangaa Mbunge km huyu kuwakomboa Watu wa Kusini na WAKATI hana Hata dira ya maendeleo ya Jimbo lake!!
Atawakomboaje bila kuwapa elimu? Baruany atuambie Ana viwanja vingapi kwa ajili ya kujenga shule? Hata ya Chekechea?.....Kama wabunge wako hivi Ukombozi Kusini itakuwa ngumu sana!!!

Pili, wabunge wa Kusini hawana Ile nia ya dhati ya kuwakomboa wana Kusini!! Wanafikiria juu ya matumbo yao na ustawi wa familia zao!!

Tatu, hawana sauti moja! Wangelikuwa na sauti moja wakaungana na Mbunge wa Mtwara mjini MH.Murje mambo pengine yangekaa sawa lakini Kila Mbunge wa Kusini ana msimamo wake

TATU,raia wa Kusini hasa Huku Pwani, uvivu ndo tatizo!! Watoto hawataki kusoma, wakaidi na wajeuri!!

Kwa haya machache tu, UKOMBOZI KUSINI UTACHUKUA MUDA MREFU SANA "
 
Tuliopata kutembea mkoa wa Lindi na Mtwara utaona wananchi hawajajiandaa wala kuandaliwa kwa hiyo gesi ni zaidi ya kuoneshwa kwenye tv kuhusu hao watu wapatao scholarship na ujenzi wa Dangote.
 
MKOMBOZI ameshapatikana kuna kijana mmoja mtoto wa LINDI amenidokeza kuwa atagombea,tena amenidokeza atagombea jimbo la MTAMA,ila jamaa na mkubali sana ameshatengeneza STRATEGIC PLAN YA MAENDELEO MIKOA YA KUSINI ambayo ina phase 4,anaitwa MALICK MALICK
 
Mkuu , siasa za Lindi nazo zina mambo yake!, kule Mtama, Membe atagombea urais na kumpisha Mohamed Abdul Aziz wakati Lindi mjini, inasemekana kwa vile Salum Baruany, alichaguliwa kwa kura za "compassion" kwa rangi yake, then 2015, wanamuandaa cheupe original, Jarufu kuongoza jahazi la Lindi!, "Mamaa!" ameisharidhia!.

Pasco
 
Maada nzuri sana,, TAIFA LA TANZANIA halijaweza mpaka sasa kuandaa watu wake kupambana na mazingira yao. Watanzania hawajui mpaka sasa dunia inataka nini, serikali imelala na ikawalaza watu wake, TUKO kwenye ulimwengu wa technolojia na innovation lakini watanzania bado wanawaza ukalani na kuhesabu hela za wazungu... Tumeegemea kwenye mteremko na urahisi wa maisha,,, tunashindwa kujiuliza kwa nini tunapewa misaada na kwa nini tusisaidiwe
 
Mkuu , siasa za Lindi nazo zina mambo yake!, kule Mtama, Membe atagombea urais na kumpisha Mohamed Abdul Aziz wakati Lindi mjini, inasemekana kwa vile Salum Baruany, alichaguliwa kwa kura za "compassion" kwa rangi yake, then 2015, wanamuandaa cheupe original, Jarufu kuongoza jahazi la Lindi!, "Mamaa!" ameisharidhia!.

Pasco
Acha uongo wewe..Mtama itakuwa ya Nape Nnauye, Lindi Mjini ni ya Salma Kikwete
 
Acha uongo wewe..Mtama itakuwa ya Nape Nnauye, Lindi Mjini ni ya Salma Kikwete
Mkuu Chalinze Mzee, asanta kwa hii, kwanza sio vema kuanza kuitana waongo kwa taarifa za speculations tuu, unless kama fomu za kugombea zimeishatolewa na wagombea kupitishwa na vyama vyao!.

Pili siku zote sio static, ni very dynamic hivyo zina change with time kila wakati!. Mimi nilikuwa Lindi mwezi wa nane wakati wa Nane Nane ndipo nikasikia Membe atagombea urais, Abdul Aziz Mtama, Jarufu Lindi Mjini, sasa kama leo ndio umesikia Nape ndie atagombea Mtama na Mama Salma Lindi, wala sikuiti muongo, uchaguzi ukukaribia ndio ukweli utabainika, kama watu humu wanavyoweweseka na "kuianza safari ya matumaini" yule "jamaa yangu!", na hapo ndio wala hajatamka atagombea!, wengi wataweza kuja kushangaa na kupigwa na bumbuwazi pale watakapo kuta hata fomu hatachukua!, na wala hagombei chochote, popote!.

Pasco
 
Mkuu Pasco ni kweli siasa za kusini zina mambo yake,ila MEMBE ndo alimuangusha Abdul-aziz(silipideni),hawaivi chungu kimoja sababu ABDUL-AZIZ anaonekana ni mtu anaemuunga mkono EDO,pia alikua mshikaj mkubwa wa R.A,tatizo la ABDUL-AZIZ ni shule ndogo(anajua kusoma na kuandika tu),ila tetesi LINDI MJINI ni kuwa ABDUL-AZIZ anaenda kugombea jimbo la mchinga kumtoa SAID MTANDA
 
Yaah,nilishawai leta uzi wa kuhusu nape kufutulisha jimbo la mtama,pia kuna Selemani mathey diwani wa tuangoma nae amejipitisha sana na kuanzisha ligi ya mpira wa miguu,zawadi akaingia mitini
 
MKOMBOZI ameshapatikana kuna kijana mmoja mtoto wa LINDI amenidokeza kuwa atagombea,tena amenidokeza atagombea jimbo la MTAMA,ila jamaa na mkubali sana ameshatengeneza STRATEGIC PLAN YA MAENDELEO MIKOA YA KUSINI ambayo ina phase 4,anaitwa MALICK MALICK

Naona mada imegeukia kwenye mgombea

Back
Top Bottom