Mcheza Karate
JF-Expert Member
- Jun 30, 2011
- 690
- 354
Nilikuwa kimya kidogo hapa jamvini kutokana na majukumu ya maisha, ile leo nashiriki nanyi wanaJF wenzangu.
Dhamira ya mada yangu ni kutaka kuwaeleza kwa undani juu ya hiki kitu kinachoitwa RAMLI kwa kuwa serikali imepiga marufuku kitu hicho.
RAMLI
Ni elimu ya nyota ihusuyo ubashiri juu ya jambo lililomtoke, kumtokea au litakalomtokea mtu ambalo limejificha.
AINA ZA RAMLI
Zipo aina nyingi sana za ramli lakini leo nitataja mbili. tu maarufu na kuzielezea.
1. Ramli za kutumia majini.
2. Ramli za kutumia maandishi na alama.
1. Ramli za kutumia majini
Hii ni aina ya ramli ambayo hutumiwa sana ktk nchi nyingi za Africa, mashariki ya kati na hata ulaya mashariki.
Aina hii ya ramli hufanyika kwa mtabiri kuwa anamiliki majini ambayo humwezesha kuwa anayatumia kufahamu mambo yajayo na yaliyojificha kwake au kwa mtu yeyote.
Na pia kuna baadhi huwapanda majini hao mwilini mwao(huwa hawaonekani kwa macho) na kuanza kuelezea ubashiri wa mtu mwenye kutazamwa matatizo yake.
2. Ramli za maandishi au alama
Hapa mtabiri/mpiga ramli huchukua alama ya mwili au unasaba wa jina la mhusika anayetaka kupigiwa ramli kisha hufanyiwa kazi. Kwani alama za mwili na jina lina uhusiano mkubwa sana ktk nyota.
MFANO
Mahitaji
*karatasi nyeupe isiyoandikwa na isiyo na mistari(plain paper)
*kalamu nyekundu au chaki nyekundu.
*wembe.
Namna ya kubashiri/kupiga ramli
1. Kata karatasi ktk umbo la mraba au iache kama ilivyo ktk umbo la mstatili(hasa zile za A4).
2. -Andika jina la unayempigia ramli, (jina lake na la mama yake) katikati ya karatasi kwa kutumia kalamu nyekundu au chaki nyekundu.
AU
-Anayetakiwa kupigiwa ramli aguse katikati ya karatasi kwa kiganja chake na atoe kiganja kutoka kwenye karatasi.
3. Kunja karatasi liwe vipande viwili vilivyo sawa. Kila ncha ya kona ya karatasi ikutane na ncha ya upande wa pili na kutengeneza kama umbo la V(samahani kwa kutokuwa na mchoro au picha)
4.Anza kutabiri kimya kimya(ukitamka rohoni)
Inaendelea...