Ukweli kuhusu unga airport.

Ukweli kuhusu unga airport.

Joined
Aug 4, 2013
Posts
5
Reaction score
6
wadau natumaini hamjambo,
nimekua nikisoma thread nyingi sana ambazo zimeandikwa kuhusu madawa ya kulevya uwanja wa ndege wa dar es salaam(JNIA),lakini waandishi wengi na hata magazeti yamekuwa yakitupia lawama baadhi wa watu bila kujua namna kazi zinazofanywa airport.ni kweli airport kuna vitengo vingi sana na kila kimoja kina kazi yake maalum na hadi abiria aweze kuruhusiwa kusafiri anakuwa amepita sehemu zifuatazo;
1.abiria anapofika airport,kabla ya kuingia ndani ya jengo la airport huwa kuna mwanausalama anayekaa mlangoni kwa ajili ya kukagua ticket na passport(kwa wanaoenda nje ya nchi....international flights) na ticket na kitambulisho kwa wale wanaosafiri ndani ya nchi.(domestic flights).nyaraka hizi hukaguliwa kama ifuatavyo;
a)kuangalia kitambulisho au passport ya muhusika kama kweli ni yeye.
b)kuangalia kama kitambulisho au passport ni valid.
c)kuangalia majina ya kitambulisho au passport kama yanaendana na ya kwenye ticket.
d)kuangalia tarehe husika ya safari(sio mtu ana ticket ya tar 8 ye anakuja tar 1)unless otherwise abiria awe amebadilisha tarehe ya safari na ni lazima atoe maelezo kwa mkaguzi kumjulisha kuhusu ilo.(hii ni kama hakuprint ticket yake mpya.
umuhimu wa zoezi hili ni kutokuruhusu watu wasiohusika na safari kuingia ndani ya kiwanja.pia afisa mkaguzi anaweza kumruhusu mtu kuingia ndani ya uwanja endapo atajiridhisha na maelezo ya muhusika kulingana na tatizo alilonalo na jinsi hali itakavyoruhusu.

2.baada ya abiria kukaguliwa ticket ataruhusiwa kuingia ndani na kuendelea na ukaguzi wa kwake mwenyewe na mizigo yake.maafisa usalama wanaokagua ni proffessionals ambao wamepata mafunzo ya usalama wa anga(aviation security) kwa ajili ya weapons,explossives,dangerous articles na chemicals kama acid n.hili ndilo jukumu kubwa na la msingi la hawa wakaguzi maafisa usalama wa anga na si vinginevyo.hwa maafisa wanapata mafunzo maalumu ya usalama wa anga ambayo huratibiwa na shirika la usafiri wa anga duniani(international civil aviation organization....ICAO) na msaafu wao mkubwa ni ANNEX 17 ambao ndio biblia au qurani kwao.so,tunapowabebesha lawama za madawa ya kulevya ni kuwaonea.ukiangalia annex 17 hakuna sehemu yoyote ile ambayo unga unatajwa.ila kuna kitu kinaitwa CONTRABAND....hivi ni vitu vya ziada ambavyo uhalali wake unategemea na sera ya serikali husika.mfano,jukumu la msingi la hawa mabwana ni explosives,weapons etc lakini kama watabahatika kuviona vitu hivyo kama pembe za ndovu,madawa au nyara zozote za serikali basi watatoa taarifa kwa wahusika,kama ni madawa basi kwa askari wa kuzuia madawa na kama ni nyara za taifa basi kwa afisa wanyamapori.....NASISITIZA TENA,MAJUKUMU YA MSINGI YA HAWA WAKAGUZI WA AIRPORT NDIYO HAYO NILIYOYATAJA NA HAYO MENGINEYO KAMA MADAWA,PEMBE ZA NDOVU,UTOROSHAJI WA FEDHA ETC NI YA ZIADA NA HUSHUGHULIKIWA ENDAPO WATAYAONA NA KAMA HAWATAYAONA BASI HAWAPASWI KUHUKUMIWA.MAAFISA HAWA WATAHUKUMIWA ENDAPO ITATHIBITIKA PASI NA SHAKA KUWA WALIKUWA NA TAARIFA KUHUSU CONTRABAND HIZO AU WALIZIONA WAKAZIACHA AU WALISAIDIA KUZIPITISHA KWA MAKUSUD

3.baada ya maafisa wakaguzi,huwa kuna wahusika wa kada mbali mbali ambao huwa ni usalama wa taifa,polisi,afisa wanyamapori,askari wa madawa ya kulevya,maafisa wa chakula na dawa,madini etc etc,hawa huwa wamesimama pembeni wakiangalia ukaguzi unavyoendelea na kama watakuwa na wasiwasi na mtu yoyote,au kama wanaona hawakuridhika na ukaguzi aliofanyiwa abiria basi wana haki ya kuchukua huyo abiria na kumkagua tena au kumuhoji kwa chochote ambacho watakuwa wanahitaji kukijua kutoka kwake.

4.baada ya hapo abiria ataelekea kwenye check in desk,kwenye dawati la ndege husika,ataacha mizigo yake pale(check in luggages-hii ni mizigo kwa kawaida mikubwa kwa ajili ya kupelekwa kwenye buti ya ndege)na atabaki na mzigo wake mdogo wa mkononi kwa ajili ya kuelekea nao kwenye ndege.kwa kawaida mzigo wa aina hii hautakiwi kuzidi kilo kumi.inaweza kuwa pochi,begi la laptop etc etc.hapo atapewa boarding pass.hiki ni kipande maalum cha karatasi ambacho atakionyesha kabla ya kuingia kwenye ndege.MIZIGO MIKUBWA ATAKAYOIACHA HAPA,ITAPITISHWA KWA MBWA MAALUM WA KUGUNDUA MADAWA YA KULEVYA KABLA HAIJAPELEKWA KWENYE NDEGE.HAPA PIA TUNAONA KUNA ASKARI MAALUM WA MADAWA YA KULEVYA WANAOTUMIA MBWA KWA KUTIMIZA MAJUKUMU YAO.

5.akitoka hapo abiria ataelekea uhamiaji kwa ajili ya kugonga passport yake tayari kwa safari,maafisa uhamiaji watahakikisha passport iko sawa,visa kama inahitajika(kulingana na nchi abiria anayokwenda)na taratibu zote za kiuhamiaji kabla ya kumgongea mtu muhuri wa ruksa kuendelea na safari.IKUMBUKWE KUWA KUNA THREAD NYINGI NA HATA MAGAZETI YAMEKUWA YAKIWATUHUMU MAAFISA UHAMIAJI KUHUSU MADAWA YA KULEVYA,UKWELI NI KWAMBA WAO HAWAHUSIKI NA UKAGUZI WOWOTE WA ABIRIA,WANACHOKAGUA NI NYARAKA ZA SAFARI TU KAMA PASSPORT,VISA ETC ETC.KATIKA AKILI YA KAWAIDA KUWATUHUMU WATU HAWA NI SAWA NA KUJIDHALILISHA TU NA KUONYESHA KUWA HUJUI KAZI ZA AIRPORT ZINAVYOKWENDA.NI SAWA NA KUSEMA KILA ANAYEFANYA KAZI AIRPORT ANAHUSIKA NA MADAWA YA KULEVYA...JAMANI WENGINE NI WAFANYA USAFI TU.

6.baada ya kutoka uhamiaji abiria hukaguliwa tena kama mwanzo,safari hii ni kwa kiwango cha juu kidogo hasa yeye mwenyewe na mzigo wake mdogo wa mkononi kwani ndiyo vitu viwili pekee ambavyo huingia kwenye ndege.ikumbukwe kuwa mzigo mkubwa umeshapita kwenye ukaguzi wa mara a pili(mbwa)kabla ya kuelekea kwenye ndege.HII NDIYO SAFARI NZIMA INAVYOKUWA.

SASA BASI KUMEKUWA NA KAULI ZA KUWASUKUMIA BAADHI YA WATU MIZIGO NA LAWAMA KWAMBA WAO NDIO WANAHUSIKA NA UPITISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA AIRPORT BILA KUJUA NANI NI MUHUSIKA NA NANI SIO MUHUSIKA.MBAYA ZAIDI HATA WAKUU WA POLISI NA MADAWA YA KULEVYA WANAWATUPIA LAWAMA MAAFISA WAKAGUZI NZ UHAMIAJI ILI HALI ASKARI WA KUZUIA NA WENYE MAFUNZO MAALUMU YA MDAWA YA KULEVYA WAPO UWANJANI HAPO.

WADAU NAOMBA WATU WAHUKUMIWE KULINGANA NA UKWELI HUU NA SIO MTU ANAANDIKA NA KULAUMU WATU BILA KUJUA NINI HUFANYIKA AIRPORT.TATIZO KUBWA LA WATZ HUWA HAWATAFUTI CHANZO,BALI HUWA WANATAFUTA NANI WA KUMTOA KAFARA.KAMA AKINA MASOGANGE WAMEWATAJA WENYE MZIGO HUO,KWANINI TUSIWAWAJIBISHE NA HAO PIA KAMA TUNA NIA YA DHATI YA KUPAMBANA NA MADAWA HAYA HARAMU?KUWAWAJIBISHA WAFANYAKAZI WA AIRPORT NDIO KUZUIA MADAWA KUINGIZA NA KUTOKA NCHINI?LAZIMA TUTAFAKARI KUHUSU HILI.
 
Asante kwa andiko lako limetujuza baadhi
kwa kina kinachoendelea airport.
Naamini wstakuja wanaojua zaidi nao
watatupa mwanga zaidi hata ikiwezekana
pale usipopaelezea kwa undani zaidi.
 
Hivi nyie maafisa wa airport si mnakimtambo chenu kile (scanner )ambayo inaonyesha vitu vinavyobebwa ndani ya mzigo sasaaa inakuwaje mzigo unascaniwa na bado unapita tu hadi ufike nchi za nje wakati mmefundishwa kutambua aina tofauti za vitu kutokana na ilivyoscaniwa...au mnapigwa upofuuu
 
Hizi dawa bana zinavyopitishwa, hasa kwenye uwanja wa JNIA ni wazi kabisa, hizo pesa zinagawiwa kwa watu wengi wenye vitengo mbalimbali, kuanzia kwa yule kuruta wa mlangoni, wadhibiti mihadarati, mpaka ofisi ya uhamiaji pale uwanjani! Ni ukweli usiopingika kwamba watu wanaofanya hii biashara wanajulikana, kama na wewe kaka upo kwenye moja ya kitengo na unajaribu kujitetea kidgo ni vyema, lakini ni ukweli usiopingika kwamba WOTE NYIE MNAJUA SIKU "MABOSI" WENU wanapopitisha punda wao, na mnakuwa mshapata mgao, tofauti pekee iliyopo ni kiasi cha mgao kwa kila kitengo.:disapointed:
 
Umetoa maelezo mengi mazuri lakini umeshindwa kutuambia nani hatimizi wajibu wake hadi madawa yanapita? Wenzetu wa viwanja vya nchi nyingine wanatumia mbinu gani za usalama kuwakamata ambazo sisi hatuna?
 
unaambiwa kuwa hio ni sehemu ya "CONTRABAND......hivi ni vitu vya ziada ambavyo uhalali wake unategemea na sera ya serikali husika.mfano,jukumu la msingi la hawa mabwana ni explosives,weapons etc lakini kama watabahatika kuviona vitu hivyo kama pembe za ndovu,madawa au nyara zozote za serikali basi watatoa taarifa kwa wahusika,kama ni madawa basi kwa askari wa kuzuia madawa na kama ni nyara za taifa basi kwa afisa wanyamapori" jamaa hawawezi ulizwa kwa maana hawakubahtika kuviona! sawa - ni bora ukae kimya! sheria bwana ni kazi kweli kweli, mtu unajitetea humo kwa humo
Kwa hiyo hizo kilo 150 wanazodai zimekamatwa S.A hapo JNIA hamkuziona?????!!! Are you kidding me??!!!
 
Najaribu kuikumbuka issue ya mama aliyepigiwa simu na mume wake kuwa kwenye begi alosafiria kulikuwa na bunduki, wakati huo mama kesha board ndege ! Unaielezeaje hiyo issue? Sio kutokuwajibika kwenu unakojaribu kutetea?
 
Nikuambieni kitu, Vitu hupitia mlango wa wafanyakazi yaani hao wakuu, halafu mfagiaji anavipeleka lango la mwisho, halafu kule ndio packing mpya hufanywa kwa ustadi. Msafiri anafika masaa kibao kabla ya check in. Chawa akuumaye yuko nguoni mwako. Bila hukumu kali ya kunyongwa hadharani pale mnazi mmoja, Tz bila unga ni porojo tu. Umekamatwa redhanded sasa uchunguzi unaendelea vipi? Kamba iwekwe tayari na mtarimbo wa kumpandishia hapo, TV zionyeshe kazi ikiendelea. Kama ni kilio, sisi tunalia sana ndugu zetu wanavyopukutika Banaa. Tanzania imezidi huruma, hata jambazi anaambiwa siku ya msako uliona wapi? Polisi wanakamata kilo 3 za cocain wanapeleka kilo 3 za sembe!! Mungu atusaidie. Halafu anahamishwa kituo na kupandishwa cheo. Uliona Wapi. Hii ni kufru.
 
Sasa hapa mantiki ya uzi ni nini????

1. Kwamba uhamiaj.hamuhusiki??
2. Hakuna mtu maalum wa kazi hii as hata watu wa kitengo ni mpaka wastuliwe???
3. Kwamba hata watu wa usalama nao ni sehemu tu ya gwaride la ukaguzi na hufanya kazi kwa a mere guess!!!!

Kwa kuwa una uzoefu na kazi yako hebu weka ushauri nini kifanyike???
 
...jamani tutambue unapo deal na international drug dealers ni majitu mengine hatari sana yenye utawala wao ambao uko well & carefuly organised, na wapo ktk ngazi na vitengo/idara zote za serikali including tiss. so hata zikifungwa scanner 200 bado yatapitisha tu mzigo maana siku zote yako pro active. hata sasa yanausoma mchezo na kubadili mbinu wakati sisi tunatupiana lawama badala ya kuyanasa...
 
Wewe unataka kukatisha watu tamaa. Naona uu mvivu unataka na wenzako wakuige
 
. Si keshasema sio kazi yao kuangalia???

Hujamsoma, kasema wanawajibika kuripoti ikiwa wataona mzigo kama huo. Sasa hapa swali ni je hawakuziona zile 150K??!! Soma vizuri hapa

HAYO MENGINEYO KAMA MADAWA,PEMBE ZA NDOVU,UTOROSHAJI WA FEDHA ETC NI YA ZIADA NA HUSHUGHULIKIWA ENDAPO WATAYAONA NA KAMA HAWATAYAONA BASI HAWAPASWI KUHUKUMIWA.

Hicho ndicho alichoandika huyo bwana. Kwa hiyo swali langu liko pale pale hizo 150K hawakuziona???!!!
 
Vyovyote uelezeavyo hapo airport lazima mlaumiwe maana hao askari maalum si wapo hapo tena na mbwa? au hao mbwa wanakuwa washalewa madawa ya kulevya washindwe kunusa mizigo??
btw, hiyo hatua namba 2 kweli hamuwezi kujiuliza ni mzigo wa aina gani mwingi hivyo?? au kuna staff alipita nao pembeni kama wa kwake kwa kucheza dili na kuepuka utaratibu wa security screening?
 
Hakuna lolote,tukipita sie tusiokuwa na nyunga mnatunyanyasa kama nini.na vizawadi vyetu vya korosho na viungo vya pilau.wenzetu na mikilo yote ya drugs,mtadai labda maziwa.msonyoooo.
 
wadau natumaini hamjambo,
nimekua nikisoma thread nyingi sana ambazo zimeandikwa kuhusu madawa ya kulevya uwanja wa ndege wa dar es salaam(JNIA),lakini waandishi wengi na hata magazeti yamekuwa yakitupia lawama baadhi wa watu bila kujua namna kazi zinazofanywa airport.ni kweli airport kuna vitengo vingi sana na kila kimoja kina kazi yake maalum na hadi abiria aweze kuruhusiwa kusafiri anakuwa amepita sehemu zifuatazo;
1.abiria anapofika airport,kabla ya kuingia ndani ya jengo la airport huwa kuna mwanausalama anayekaa mlangoni kwa ajili ya kukagua ticket na passport(kwa wanaoenda nje ya nchi....international flights) na ticket na kitambulisho kwa wale wanaosafiri ndani ya nchi.(domestic flights).nyaraka hizi hukaguliwa kama ifuatavyo;
a)kuangalia kitambulisho au passport ya muhusika kama kweli ni yeye.
b)kuangalia kama kitambulisho au passport ni valid.
c)kuangalia majina ya kitambulisho au passport kama yanaendana na ya kwenye ticket.
d)kuangalia tarehe husika ya safari(sio mtu ana ticket ya tar 8 ye anakuja tar 1)unless otherwise abiria awe amebadilisha tarehe ya safari na ni lazima atoe maelezo kwa mkaguzi kumjulisha kuhusu ilo.(hii ni kama hakuprint ticket yake mpya.
umuhimu wa zoezi hili ni kutokuruhusu watu wasiohusika na safari kuingia ndani ya kiwanja.pia afisa mkaguzi anaweza kumruhusu mtu kuingia ndani ya uwanja endapo atajiridhisha na maelezo ya muhusika kulingana na tatizo alilonalo na jinsi hali itakavyoruhusu.

2.baada ya abiria kukaguliwa ticket ataruhusiwa kuingia ndani na kuendelea na ukaguzi wa kwake mwenyewe na mizigo yake.maafisa usalama wanaokagua ni proffessionals ambao wamepata mafunzo ya usalama wa anga(aviation security) kwa ajili ya weapons,explossives,dangerous articles na chemicals kama acid n.hili ndilo jukumu kubwa na la msingi la hawa wakaguzi maafisa usalama wa anga na si vinginevyo.hwa maafisa wanapata mafunzo maalumu ya usalama wa anga ambayo huratibiwa na shirika la usafiri wa anga duniani(international civil aviation organization....ICAO) na msaafu wao mkubwa ni ANNEX 17 ambao ndio biblia au qurani kwao.so,tunapowabebesha lawama za madawa ya kulevya ni kuwaonea.ukiangalia annex 17 hakuna sehemu yoyote ile ambayo unga unatajwa.ila kuna kitu kinaitwa CONTRABAND....hivi ni vitu vya ziada ambavyo uhalali wake unategemea na sera ya serikali husika.mfano,jukumu la msingi la hawa mabwana ni explosives,weapons etc lakini kama watabahatika kuviona vitu hivyo kama pembe za ndovu,madawa au nyara zozote za serikali basi watatoa taarifa kwa wahusika,kama ni madawa basi kwa askari wa kuzuia madawa na kama ni nyara za taifa basi kwa afisa wanyamapori.....NASISITIZA TENA,MAJUKUMU YA MSINGI YA HAWA WAKAGUZI WA AIRPORT NDIYO HAYO NILIYOYATAJA NA HAYO MENGINEYO KAMA MADAWA,PEMBE ZA NDOVU,UTOROSHAJI WA FEDHA ETC NI YA ZIADA NA HUSHUGHULIKIWA ENDAPO WATAYAONA NA KAMA HAWATAYAONA BASI HAWAPASWI KUHUKUMIWA.MAAFISA HAWA WATAHUKUMIWA ENDAPO ITATHIBITIKA PASI NA SHAKA KUWA WALIKUWA NA TAARIFA KUHUSU CONTRABAND HIZO AU WALIZIONA WAKAZIACHA AU WALISAIDIA KUZIPITISHA KWA MAKUSUD

3.baada ya maafisa wakaguzi,huwa kuna wahusika wa kada mbali mbali ambao huwa ni usalama wa taifa,polisi,afisa wanyamapori,askari wa madawa ya kulevya,maafisa wa chakula na dawa,madini etc etc,hawa huwa wamesimama pembeni wakiangalia ukaguzi unavyoendelea na kama watakuwa na wasiwasi na mtu yoyote,au kama wanaona hawakuridhika na ukaguzi aliofanyiwa abiria basi wana haki ya kuchukua huyo abiria na kumkagua tena au kumuhoji kwa chochote ambacho watakuwa wanahitaji kukijua kutoka kwake.

4.baada ya hapo abiria ataelekea kwenye check in desk,kwenye dawati la ndege husika,ataacha mizigo yake pale(check in luggages-hii ni mizigo kwa kawaida mikubwa kwa ajili ya kupelekwa kwenye buti ya ndege)na atabaki na mzigo wake mdogo wa mkononi kwa ajili ya kuelekea nao kwenye ndege.kwa kawaida mzigo wa aina hii hautakiwi kuzidi kilo kumi.inaweza kuwa pochi,begi la laptop etc etc.hapo atapewa boarding pass.hiki ni kipande maalum cha karatasi ambacho atakionyesha kabla ya kuingia kwenye ndege.MIZIGO MIKUBWA ATAKAYOIACHA HAPA,ITAPITISHWA KWA MBWA MAALUM WA KUGUNDUA MADAWA YA KULEVYA KABLA HAIJAPELEKWA KWENYE NDEGE.HAPA PIA TUNAONA KUNA ASKARI MAALUM WA MADAWA YA KULEVYA WANAOTUMIA MBWA KWA KUTIMIZA MAJUKUMU YAO.

5.akitoka hapo abiria ataelekea uhamiaji kwa ajili ya kugonga passport yake tayari kwa safari,maafisa uhamiaji watahakikisha passport iko sawa,visa kama inahitajika(kulingana na nchi abiria anayokwenda)na taratibu zote za kiuhamiaji kabla ya kumgongea mtu muhuri wa ruksa kuendelea na safari.IKUMBUKWE KUWA KUNA THREAD NYINGI NA HATA MAGAZETI YAMEKUWA YAKIWATUHUMU MAAFISA UHAMIAJI KUHUSU MADAWA YA KULEVYA,UKWELI NI KWAMBA WAO HAWAHUSIKI NA UKAGUZI WOWOTE WA ABIRIA,WANACHOKAGUA NI NYARAKA ZA SAFARI TU KAMA PASSPORT,VISA ETC ETC.KATIKA AKILI YA KAWAIDA KUWATUHUMU WATU HAWA NI SAWA NA KUJIDHALILISHA TU NA KUONYESHA KUWA HUJUI KAZI ZA AIRPORT ZINAVYOKWENDA.NI SAWA NA KUSEMA KILA ANAYEFANYA KAZI AIRPORT ANAHUSIKA NA MADAWA YA KULEVYA...JAMANI WENGINE NI WAFANYA USAFI TU.

6.baada ya kutoka uhamiaji abiria hukaguliwa tena kama mwanzo,safari hii ni kwa kiwango cha juu kidogo hasa yeye mwenyewe na mzigo wake mdogo wa mkononi kwani ndiyo vitu viwili pekee ambavyo huingia kwenye ndege.ikumbukwe kuwa mzigo mkubwa umeshapita kwenye ukaguzi wa mara a pili(mbwa)kabla ya kuelekea kwenye ndege.HII NDIYO SAFARI NZIMA INAVYOKUWA.

SASA BASI KUMEKUWA NA KAULI ZA KUWASUKUMIA BAADHI YA WATU MIZIGO NA LAWAMA KWAMBA WAO NDIO WANAHUSIKA NA UPITISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA AIRPORT BILA KUJUA NANI NI MUHUSIKA NA NANI SIO MUHUSIKA.MBAYA ZAIDI HATA WAKUU WA POLISI NA MADAWA YA KULEVYA WANAWATUPIA LAWAMA MAAFISA WAKAGUZI NZ UHAMIAJI ILI HALI ASKARI WA KUZUIA NA WENYE MAFUNZO MAALUMU YA MDAWA YA KULEVYA WAPO UWANJANI HAPO.

WADAU NAOMBA WATU WAHUKUMIWE KULINGANA NA UKWELI HUU NA SIO MTU ANAANDIKA NA KULAUMU WATU BILA KUJUA NINI HUFANYIKA AIRPORT.TATIZO KUBWA LA WATZ HUWA HAWATAFUTI CHANZO,BALI HUWA WANATAFUTA NANI WA KUMTOA KAFARA.KAMA AKINA MASOGANGE WAMEWATAJA WENYE MZIGO HUO,KWANINI TUSIWAWAJIBISHE NA HAO PIA KAMA TUNA NIA YA DHATI YA KUPAMBANA NA MADAWA HAYA HARAMU?KUWAWAJIBISHA WAFANYAKAZI WA AIRPORT NDIO KUZUIA MADAWA KUINGIZA NA KUTOKA NCHINI?LAZIMA TUTAFAKARI KUHUSU HILI.
Tupe ukweli kuhusu taarifa kwamba siku zilipopitishwa kilo 150 sniffing dogs wa Airport hawakuwepo.
 
Back
Top Bottom