Ukweli kuhusu UDA na madai ya Robert Kisena

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Wiki iliyopita Mwenyekiti wa Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (UDA), Robert Kisena alikutana na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam akazungumza nao kuhusiana na habari kuu tuliyoichapisha katika toleo Na 225 la Gazeti la JAMHURI.

Katika maelezo yake, alikanusha habari tuliyoichapisha ukurasa wa kwanza iliyosema “Familia ya Kikwete inahusika UDA.” Katika habari hiyo, tulionyesha kuwa mtoto wa Rais (mstaafu) Jakaya Kikwete, Khalfan Mrisho Kikwete nyaraka za kampuni ya Simon Group Ltd zinamtaja kama mmoja wa wakurugenzi.

Habari hii tuliichapisha baada ya kupata taarifa ya uchunguzi wa kina (due diligence report) iliyofanywa na Kampuni ya Philip and Co iliyochunguza Simon Group ni nani na ana uwezo kiasi gani katika kuendesha biashara ya usafirishaji wa abiria hadi apewe shirika kama UDA iliyowasilishwa kwa Jiji la Dar es Salaam, Novemba 2009.

Kati ya mambo yote yaliyomo kwenye ripoti hiyo tuliyoyachapisha, Kisena amekanusha suala la familia ya Kikwete kuhusika katika UDA pekee. Baada ya kukanusha huko, mjadala mkubwa umeendelea katika vyombo vya habari kwa maana ya magazeti, redio, televisheni na mitandao ya kijamii.

Kisena wakati anakanusha alisema kuna watu wanatumia waandishi kisiasa, hapana shaka akimaanisha kuwa waandishi wa JAMHURI wanatumika kisiasa. Kwa nia ya kulinda heshima ya gazeti hili linalothaminika katika jamii kwa habari za uchunguzi, tumeamua kuweka kumbukumbu sawa na wala si kuanzisha malumbano.

La kwanza tumekubali kitaaluma Kampuni ya Simon Group kutoa makala ya mtangazaji katika toleo letu la leo. Tumefanya hivyo kwa kuamini kuwa chombo cha habari ni uwanja huru unaopaswa kutoa fursa kwa yeyote mwenye jambo analotaka kulisema aliseme bila kunyimwa fursa hiyo kisha jamii ndiyo ipime uhalisia wa asemalo. Ni kwa msingi huo tumekubali kuchapisha toleo lake.

Pili tunapenda kuweka wazi kuwa hatuna shaka, wala wasiwasi na taarifa hii ya uchunguzi tuliyoipata na kuichapisha katika toleo Na 225. Tumeamua kutafsiri kifungu cha 2.1.2 kinachohusu umiliki wa hisa katika ripoti hiyo kinachosema:

Umikili wa hisa
“Kama kampuni nyingi za Tanzania ambazo zilianzishwa na watu binafsi au familia, kampuni hii haina leja ya hisa.

Simon Group Ltd
Mwaka 2008 hesabu zilizokaguliwa za Simon Group Ltd, wakurugenzi waliotajwa ni wawili tu: Ndugu Robert Kisena, na Ndugu Khalfan Mrisho [Kikwete]. Hata hivyo, hati ya mkopo iliyotiwa saini Mei 31, 2008 kwa ajili ya mkopo uliochukuliwa kutoka Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), mtia saini wa pili katika hati hiyo ni mtu aitwaye William Simon Kisena. Hivyo idadi ya wakurugenzi bila shaka ni zaidi ya wawili ikiwa nyaraka hizi zitaaminika. Idadi ya wamiliki wa hisa pia haiko wazi.

Hesabu pekee zilizochapishwa, ambazo ni za Simon Group Ltd pekee, zinaonyesha kwamba hisa za mtaji zilizoidhinishwa ni Tsh bilioni 2, lakini mtaji uliolipiwa ni Tsh milioni 670.

Kwa kutokuwapo mapato ya mwaka wa 2008, umiliki halisi na makazi ya wakurugenzi na mengine hayawezi kuthibitishwa.” Sehemu hii ya repoti ya ukaguzi wa kina ambayo ipo kwenye vitabu vya taasisi nyeti za kifedha nchini, tunaamini inaendelea kuwa sahihi hadi itakapofutwa na wakaguzi walioifanya.

Katika taarifa yake, Kisena amesema Kampuni ya Simon Group ilianzishwa mwaka 2007 na wanafamilia wa familia ya Mzee Simon na imepewa jina hilo kwa heshima ya Baba yao, Mzee Simon Kisena Maige.

Wakurugenzi wa Simon Group anasema ni Robert Simon Kisena, William Simon Kisena, Kulwa Simon Kisena, Gloria Robert Simon, Simon Robert Simon, George Robert Simon, Modesta Pole, na mwanahisa pekee kutoka nje ya familia, Juma Kapuya, anayemiliki asilimia 5.

Alihitimisha kwa kusema inawezekana kuna watu wana ugomvi wa kisiasa na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete hivyo wasitumie ugomvi wao kupitia kampuni ya Simon Group.

Tunachofahamu na kuamini ni kwamba habari za uchunguzi zinajikita katika ukweli, ukweli tupu bila uonevu, wala upendeleo. Tunaindesha kampuni ya Jamhuri Media Ltd na gazeti inalozalisha la uchunguzi la JAMHURI kitaaluma na kwa weledi wa hali ya juu.

Kama ambavyo mara zote tumechapisha habari zetu bila hiyana, woga, upendeleo au uonevu kwa kutaja mifano michache kama Bandari, maliasili, dawa za kulevya, watakatisha madini na nyingine nyingi tunaamini kote huko tulifanya kwa kusukumwa na uzalendo tukitanguliza masilahi ya taifa chini ya falsafa yetu ya “TUNAANZIA WANAPOISHIA WENGINE”, na hivyo ndivyo tulivyofanya kwa UDA. Taarifa ya Simon Group tumeichapisha ukurasa wa 19.

Chanzo: Gazeti la Jamhuri
 
Tanzania ni nchi ya maajabu!

Kuanzia Watoto wa Kikwete mpaka kina Juma Kapuya ndani ya harakati za ubadhirifu wa mali za umma kupitia UDA!

Mbaya zaidi huyu Kisena aliwahi kukanusha kama Juma Kapuya siyo mmoja wa shareholders wa kampuni wakati ukweli ni shareholder.

Kanusho lake pia kwa sasa kuhusu mtoto wa Kikwete ni yale yale aliyojaribu kufanya kuhusu Juma Kapuya.

The guy is lying through his teeth!
 
Huu ndio UKWELI bila chenga, anachofanya huyu bw kisena junior's ni kaujanja ujanja ambako mwisho wa siku utaishia ku mgharim yeye na walioko nyuma yake.

Sidhani kama anashauriwa vizuri lakini aelewe kwamba safari hii meya na halmashauri zote jijini daresalaam ziko chini ya upinzani na hawatakubali madudu haya na si ajabu wajayafukua vizuri.... Hii ni kitu inaitwa a ticking bomb..... Just a matter of time....
 
Robert Kisena teh teh, eti anamiliki UDA huwa ikifika hapa mbavu zangu huuma sana. Ni kituko na kichekesho. Huyu bwana hadi 2005 alikuwa masikini kama masikini wengine TZ. Aliaanza biashara (ulanguzi) wa pamba ya wakulima ikiwa shambani (kanda ya ziwa watakuwa wananielewa vizuri biashara hii ilivyo haramu). Akiwa anabangaiza ndo kina Kapuya na kina Idd Simba wakaweka mtaji na kununua ginery moja ipo Malampaka (soma walipora toka SHIRECU) over sudden Kisena kapewa ukurugenzi (hawa wengine walikuwa watumishi wa umma so walijificha) hatimaye wamevamia UDA kama mali isomwenyewe. Hebu Simon atoke aonyeshe hesabu za biashara hiyo (ya familia) ya mwaka 2000 kama hata milioni itafika achilia mbali uwepo wa biashara yenyewe.

Ushauri wa bure, Simon rudisha shirika serikalini na rudisha pesa kwa wenyewe. Jk mrija unakatwa (soma unatumbuliwa) hana msaada sana ndo maana kawatuma kina Membe kuzuia mafuriko zaidi
 
Ukitazama jinsi Simon Group ilivyouziwa UDA na haraka walivyopata mkopo WA kununulia mabasi ambayo walisamehewa kodi
Sasa kampuni hii isiyokuwa na uzoefu WA biashara ya usafirishaji abiria mijini imepewa kuendesha mradi mkubwa DART
Angalia nauli wanayotaka kutoza (toka 500.=hadi 1400.=)
Some thing is fishy somewhere
 
Robert Kisena teh teh, eti anamiliki UDA huwa ikifika hapa mbavu zangu huuma sana. Ni kituko na kichekesho. Huyu bwana hadi 2005 alikuwa masikini kama masikini wengine TZ. Aliaanza biashara (ulanguzi) wa pamba ya wakulima ikiwa shambani (kanda ya ziwa watakuwa wananielewa vizuri biashara hii ilivyo haramu). Akiwa anabangaiza ndo kina Kapuya na kina Idd Simba wakaweka mtaji na kununua ginery moja ipo Malampaka (soma walipora toka SHIRECU) over sudden Kisena kapewa ukurugenzi (hawa wengine walikuwa watumishi wa umma so walijificha) hatimaye wamevamia UDA kama mali isomwenyewe. Hebu Simon atoke aonyeshe hesabu za biashara hiyo (ya familia) ya mwaka 2000 kama hata milioni itafika achilia mbali uwepo wa biashara yenyewe.

Ushauri wa bure, Simon rudisha shirika serikalini na rudisha pesa kwa wenyewe. Jk mrija unakatwa (soma unatumbuliwa) hana msaada sana ndo maana kawatuma kina Membe kuzuia mafuriko zaidi
Membe ni vumbi tu kama Kisena; wote ni wanufaika wa msoga group, hawachomoki hata kama hawajui walichomekwa wapi!?!
 
Huu ndio UKWELI bila chenga, anachofanya huyu bw kisena junior's ni kaujanja ujanja ambako mwisho wa siku utaishia ku mgharim yeye na walioko nyuma yake.

Sidhani kama anashauriwa vizuri lakini aelewe kwamba safari hii meya na halmashauri zote jijini daresalaam ziko chini ya upinzani na hawatakubali madudu haya na si ajabu wajayafukua vizuri.... Hii ni kitu inaitwa a ticking bomb..... Just a matter of time....
Hawa kina Kisena ni high profile matapeli wa Tanzania!

Huyu Kisena alishawahi kukanusha kama Juma Kapuya ni mmoja wa shareholders katika kampuni lakini kumbe ni shareholder.

Huu ni utapeli!

Hii ni sehemu ya article kutoka gazeti la The Citizen Toleo la 15 January 2012 kuhusu kanusho la Kisena,

By Bernard James
Dar es Salaam — Official bank and court documents have linked Urambo West MP, Prof Juma Kapuya, to Simon Group Limited, the firm that is currently under both a parliamentary and government probe in a suspect deal to acquire the Dar es Salaam public commuter bus company, UDA.

For some time now, Simon Group officials have severally and publicly denied any link or business association with Prof Kapuya, a former minister for Labour, Employment and Youth Development.Mr Simon Kisena, a director in the company which claimed to have acquired 51 per cent shares in UDA repeatedly said that Prof Kapuya was not a co-shareholder after selling his stake.
 
Huu ndio UKWELI bila chenga, anachofanya huyu bw kisena junior's ni kaujanja ujanja ambako mwisho wa siku utaishia ku mgharim yeye na walioko nyuma yake.

Sidhani kama anashauriwa vizuri lakini aelewe kwamba safari hii meya na halmashauri zote jijini daresalaam ziko chini ya upinzani na hawatakubali madudu haya na si ajabu wajayafukua vizuri.... Hii ni kitu inaitwa a ticking bomb..... Just a matter of time....

Well said. Nami nasema, hii issue ianze kufukuliwa toka Mwanzo. Huo mradi lazima kuna mkono wa former............................................. Halafu anajibu kirahisirahisi mno. Kampuni irudishwe kwenye mikono ya wananchi full stop.
 
Vipi kuhusu kesi,kisena aliwahi kumpiga mangumi OCD wa Maswa kwenye mkutano wa kampeni,wakati huo kisena alikuwa anagombea ubunge kupitia CCM, iliishia wapi? Au ndo sisi Nyumbu tumesha sahau?
 
ki ukwel kisena alipiga, tunamshauri arudishe UDA yetu vinginevyo hlo jip limeiva, linasubr kutumbuliwa tu
Wajanja kama Home Shopping Centre(HSC) baada ya kunusa hali ya kisiasa nchini waliamua kufunga biashara zao.

Huyu Kisena anafahamu anadanganya akidhani uongo wake utaendelea kusimama katika mazingira ya kisiasa ya leo.

Jiji kwa sasa liko mikononi mwa vyama vya upinzani wakati Serikali Kuu iko mikononi mwa no nonsense and results driven politicians.

Wanatakiwa wabadilishe aina ya utapeli ili kuendana na mazingira ya kisiasa!
 
Mwisho wa wiki serikari inadai itakuwa imekamilisha umiliki wa hisa zake zote TTCL kwa asilimi 100% baada ya kuuzwa kwa ujanja ujanja huko nyuma na mwekezaji ambaye ajaongeza thamani yeyote kwenye shirika zaidi ya kunufaika kutumia infrastructure at cheap.

Labda na UDA sasa irudi serikarini watu wakubali tu muda wa kurekebisha ni aibu kumiliki mali za umma ambazo azikununuliwa na valuation ambazo sio sahihi na hatua zisizo halali za kujimilikisha halafu leo watu wawe wanavuna tu.
 
Robert Kisena teh teh, eti anamiliki UDA huwa ikifika hapa mbavu zangu huuma sana. Ni kituko na kichekesho. Huyu bwana hadi 2005 alikuwa masikini kama masikini wengine TZ. Aliaanza biashara (ulanguzi) wa pamba ya wakulima ikiwa shambani (kanda ya ziwa watakuwa wananielewa vizuri biashara hii ilivyo haramu). Akiwa anabangaiza ndo kina Kapuya na kina Idd Simba wakaweka mtaji na kununua ginery moja ipo Malampaka (soma walipora toka SHIRECU) over sudden Kisena kapewa ukurugenzi (hawa wengine walikuwa watumishi wa umma so walijificha) hatimaye wamevamia UDA kama mali isomwenyewe. Hebu Simon atoke aonyeshe hesabu za biashara hiyo (ya familia) ya mwaka 2000 kama hata milioni itafika achilia mbali uwepo wa biashara yenyewe.

Ushauri wa bure, Simon rudisha shirika serikalini na rudisha pesa kwa wenyewe. Jk mrija unakatwa (soma unatumbuliwa) hana msaada sana ndo maana kawatuma kina Membe kuzuia mafuriko zaidi
You've have said it!

Mbaya zaidi, hata katika Awamu hii ya Tano anafanya uzembe hata katika kudanganya!

Wenzake Home Shopping Centre wamenusa harufu mbaya wakaingia ''mitini''.

Tanzania kuna vituko!
 
Kwa wanaojua vyema ni rahisi kugundua kauli za Membe zinasukumwa na nini .....tumeamua kwa dhati kusimama na JPM kwa faida ya vizazi vijavyo ....vita ya haki haishindwi kamwe ...
 
SIMON GROUP CO.LTD inayojitambulisha kununua shirika la usafiri Dar es Salaam ni wawakilishi wa viongozi wa Tanzania katika kufisadi mali za Umma. Anae jitambulisha kama Robert Simon Kisena ambae alisoma Nsumba Sekondari School akijulikana kwa jina JOKALA KISEANA na kumaliza Kidato cha Nne mwaka 1991 baada ya hapo alijiunga na Kidato cha Tano Shule ya Sekondari Mirambo Tabora mwaka 1992, hapa alifukuzwa akiwa Kaka Mkuu baada ya kuwasaliti wanafunzi wenzake aliokuwa akiwachongea kwa mwalimu mkuu na wanafunzi kuungana na kusababisha kusimamishwa, baada ya hapa JOKALA KISENA ambae leo anajulikana kwa majina ya Robert kisena bila kutoa sababu za kubadilisha jina lake la awali alikuwa akikaa na rafiki yake huku akifanya kazi NCU Ushirika kanda ya ziwa-Nyanza,inasemekana baadae alikosana na rafiki yake huyo baada ya kumpa mimba dada wa rafiki yake .Katika Uchaguzi mkuu wa 1995 Kisena alichukuliwa na John Cheyo wakati huo Cheyo akiwa mgombea urais na kumuweka kuwa kama masidizi wa kusimamia mali zake Shinyanga,hapa ndio kisena alipata pesa kidogo isiyoweza kununua UDA. Kisena katika kusimamia mali za cheo alifanikiwa kujenga nyumba Tatu zote zipo Nyegezi Mwanza eneo lijulikanalo kwa jina la CALIFONIA.Baada ya hapo ndio akaanzisha SIMON Agency iliyokuwa inajishughulisha na uuzaji wa spare za magari kwa muda na baadae akajiunga na Profesa Juma Kapuya akiwa waziri ambapo walifanikiwa kuanzisha kampuni iliyofahamika kwa jina la ROBASIKA-Robert Simon Kapuya na kufanikiwa kuchota bilioni 13 za wananchi kupitia Benki ya NMB mwanza kwa ushawishi wa kapuya na kuanzisha ginery ya pamba katika jimbo la kapuya .Ndio maana ukifuatilia pesa zilizolipwa kwenye account ya Iddy Simba imelipwa na Robasika kwa niamba ya Simon Group ili wafanikiwe kuchukua UDA na Kapuya akiwamo uku Simon Group wakidai kuwa ni malipo iliyokuwa ikidaiwa na Simon Group kutoka kwa Robasika kutokana na mkataba kati ya Simon Group na Robasika wa kusafirisha mizigo.Robet kisena ni chambo tu katika kuwafanikishia watu maalum kazi
 
Back
Top Bottom