Ukweli kuhusu Ubabe wa CCM, kazi maalumu ya naibu spika na Kufungiwa kwa wabunge

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411
Habari wanaJF,

Baada ya wabunge wa vyama vilivyoko Bungeni kuungana na kutoka bungeni jana. Serikali ya chama cha mapinduzi ikatafuta counter attack baada ya kuona tishio la kura ya kutokuwa na imani na naibu spika. Naomba ifahamike na ikumbukwe kwamba mchakato wa kumpata naibu spika ulikuwa na vigugumizi vingi kwakuwa alikuwa ametoka kuwa mtumishi wa serikali tena katika nafasi kubwa na ya juu maswali yalikuwa ni lini alikuwa na kadi ya chama?

CCM walimuona yeye ndiye jibu la usumbufu wa kanuni na sheria amabao Tundu Lissu alikuwa akiwatesa kwa miaka 5 iliyopita. Pia mwanadada huyu ni mbobezi wa mashuala ya kisheria hata kama anajitoa ufahamu kwasasa. Hivyo yuko pale kwa kazi maalumu na Kifupi alipitishwa kibabe sana ndani na nje ya chama.

Kwamba baada ya wabunge kutoka nje ya bunge kukawa na tishio la kukusanya sahihi za kutokuwa na imani na naibu spika na taarifa ya bunge kutoka kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge ikiwatia hatiani wabunge saba kwa makosa mbalimbali ikiwemo kudharau madaraka ya bunge ambapo wabunge Easther Bulaya na Tundu Lissu wameadhibiwa kutokuhudhuria vikao vilivyobaki vya mkutano wa tatu na vikao vyote vya mkutano wa nne.

Kwamba wabunge Pauline Geku, Halima Mdee, Zitto Kabwe, Godbless Lema wamepewa adhabu ya kutokuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya mkutano wa tatu na Mbunge John Heche hatohudhuria vikao kumi vya mkutano wa tatu. Makosa hayo waliyafanya mkutano wa pili mwezi January.

Sasa kufungiwa kwao kumekuja kama njia ya kuzuia kukusanywa kwa hizo sahihi kwasababu wabunge wenye ushawishi hawatakuwepo tena bungeni hivyo naibu atajimwayamwaya mpaka hoja isahaulike. Naomba tuweke akilini kwamba ZITTO ZUBERI KABWE ni mmoja ya wabunge wenye ushawishi wa kiwango cha ajabu na anauwezo usiomithilika linapokuja suala la kujenga hoja. Kama wangeachwa wangeweza kuleta madhara kwa kiti cha spika, suluhu pekee ni kuwatolea maamuzi ili wakae nje ya mchezo. Swali la kujiuliza kwanini kamati itoe hukumu kwa makosa ya kikao cha pili cha mwezi january? tena adhabu inakuja siku ambayo bunge liko kwenye hali tete na ya sintofahamu.

Hizi ni sarakasi za kisiasa zinazofanyiaka lakini zinavaa sura ya kusimamia sheria huku nyuma ya pazia sarakasi hizi zinaficha ubabe wa CCM, kazi maalumu ya Dr Tulia Akson Mwansasu.

Karibuni kwa mawazo yenye tija.

==================

Tujikumbushe sakata la wabunge hawa mpaka wakaadhibiwa leo kupitia video hizi:





 
Najiandaa kuomba mwongozo...
Coz kwa maelezo ya kawaida tu, ZITTO ni mtu muhim bungeni kwa maana pote anafit
 
Je kupigwa ban wenzao. Wao wakigoma nao wakapigwa ban.
Hili swala la kufungiwa muda mrefu ni hatari kwa taifa letu.
 
Wakati wanaomba miongozo ambayo imeonekana no makosa siku ile kwenye kiti hakuwa TULIA.change ndio alikuwa anaongoza kiti. TULIA anahusikaje?
 
Hii imenikumbusha pale miccm ilipokimbilia kumfungia zitto alipotoa ukweli kuhusu Buzwagi na ushiriki wa akina karamagi!Walimpiga ban ya miezi kama minne ila baadaye ikaja thibitika kuwa alichokuwa anaongea ni ukweli na alihujumiwa!Hapo ndipo watanzania wakampenda na kumuunga mkono zitto,kila alikopita alikuwa lulu!
Leo naona ccm imerudi kwa koti lingine,inafanya hujuma kwa upinzani kwa maslahi ya wachache,hakuna mabadiliko zaidi ya sarakasi za maigizo!
Magufuli atambue kuwa haya sio mabadiliko aliyowaahidi watanzania!
 
Kama ndio hivyo basi ccm inaendesha siasa zake kisasa, kibabe na kisayansi zaidi...
 
Hakika bunge safari hii limepata Naibu Spika mwenye msimamo, hayumbishwi. Watanzania tulio wengi tunakuunga mkono, chapa kazi!
 
Kosa kubwa ni la wananchi kukubali kurubuniwa na chama dhalimu kilichojaa hila kila wakati na kukipa viti vingi Bungeni hili litaigharimu nchi hii miaka kumi migumu, lau kama nafasi ya urais ingekuwa kwa ccm na asilimia kubwa ya wabunge wakawa upinzani nadhani mizani inge balance na pangekuwa na umakini kwenye utendaji na kuheshimiana.
 
Lazima ifike mahala tufanye haya mambo kwa kufuata sheria kanuni na taratibu vinginevyo ni uhuni.
 
Back
Top Bottom