Wakuu habari za asubuhi .Kile kinachoonekana kuwa ni kuchafuliwa kwa eaziri mkuu mh. Mizengo Pinda hivi karibuni kimebainika. Wabunge mbalimbali kama David Kafulila, Sendeka, Serukamba na Ligola wakiwa wamelishika sakata la bilioni 200 za Escrow na wengine wakiwa wanataka Pinda ang'olewe katika nafasi yake ya waziri mkuu. Imefahamika kuwa si kweli kuwa mtoto huyu wa mkulima anahusika. Bali ni vita kati ya wabunge, baadhi ya mawaziri na Urais 2015.
VITA YA WABUNGE :Inasemekana David Kafulila anatumiwa na mh. Mbunge tajiri Nimrod Mkono. Mkono ana ugomvi mkubwa na TANESCO kutokana na malipo yake ya mamilioni ya dola aliyokua analipwa na serikali kila mwezi kupitia TANESCO kusitishwa na Muhongo na katibu mkuu wake Maswi.
Malipo haya tata yalikuwa ni ya kazi ya Mkono kama mwanasheria wa TANESCO. Hoja hapa ilikua ni kubainika kuwa malipo hayo yalikuwa mkubwa sana na yaligubigwa na giza katika kiwango cha malipo. Hivyo Mkono anataka Prof Muhongo ang'olewe katika wizara ya nishati na madini kama kisasi. Ndipo David Kafulila akapewa kazi hiyo kupitia ESCROW na anakula pesa za Mkono kwa kazi hii.
Christopher Ole Sendeka:
Huyu ni Mbunge wa Simanjiro na rafiki kipenzi wa Reginald Mengi wa IPP. Mtakumbuka vita ya mzee Mengi na Muhongo juu ya vitalu vya gesi hivi karibuni. Wawili hawa walichapana sana hadharani na kwenye makongamano huku Muhongo akidai kuwa Mengi ni dalali na sio mfanyabiashara.
Hasira za Mengi zimeelekezwa katika kumng'oa prof Muhongo katika kiti chake cha uwaziri. Hii ilibainika wakati wa kupitisha bajeti ya prof Muhongo mwaka huu. Baadhi ya wabunge wanasemekana kuhongwa ili wamshambulie Muhongo na kukwamisha bajeti yake. Kazi hii inafanyika sasa kupitia sakata la ESCROW. Ole Sendeka anasemekana kutumiwa na bilionea Mengi kumchapa Muhongo kama kisasi cha sakata la vitalu lililomvua nguo Mengi.
SERUKAMBA,FILIKUNJOMBE:
Wabunge hawa wanaongoza kundi la wabunge wa kambi ya mgombea Urais mmoja wa CCM mwenye nywele nyeupe. Hawa nia yao hasa ni kumchapa Pinda. Wanatumwa na kupewa fedha ili kuhakikisha kwa gharama yoyote wanatumia vuguvugu hili kama fursa ya kumsafishia njia mgombea wao kwa kumuhusisha Waziri Mkuu Pinda na sakata la ESCROW.
Lengo hapa ni kumuondoa madarakani japo hahusiki ili ionekane kuwa hata mgombea wao aliwajibika kisiasa tu na hivyo kumsafishia njia nywele nyeupe. Aidha katika siku za karibuni Pinda anasemekana tangu kuanza kutajwa kugombea Urais amepata kuungwa mkono sana na kuvuna wapambe wengi wa wagombea wengine akiwemo Nywele nyeupe.
Pinda ameonekana kuwapiku wenzie walioanza mbio hizi mapema kutokana na uadilifu wake na kuwa ni mtu anayependa watu, asiye na majivuno na aliyekuwa karibu sana na baba wa taifa hayati mwalimu Nyerere . Hivyo ni lazima ashughulikiwe apunguzwe kasi na ikiwezekana ajiuzulu kabisa ili kufanya safari ya nywele nyeupe kuwa nyepesi.
BARAZA KUU UVCCM :
Juhudi za kumchafua Pinda zimeendelea pia wakati wa vikao vya BARAZA KUU la UVCCM Dodoma. Kazi hii inaratibiwa na kada mmoja wa CCM mwenye asili ya Somalia akiwa ameweka kambi Dodoma.
Kada huyu ameleta kundi la vijana zaidi ya 30 wasiokua wajumbe wala watumishi wa CCM kutoka sehemu mbalimbali. Vijana hawa walikua Dodoma wakila na kunywa na kulipwa posho Kazi yao kubwa ikiwa ni kurandaranda katika baa na kumbi zote za Dodoma usiku na mchana kufuatilia wafuasi wa Pinda wamekaa na nani na namna bora ya kumchafua Waziri Mkuu kwa kumuhusisha na ugawaji wa pesa.
Kundi hili lilizagaa Dodoma kama paka wa baa kunusa kila mahali na kuandika mitandaoni kumchafua mzee Pinda. Inasemekana posho yao ilikua kati ya sh 100,000 na 200,000 kulingana na taarifa unayopeleka kwa kada huyo Msomali. Uroho wa pesa uliwafanya vijana hao kupeleka taarifa za uongo mradi wapate kula yao.
Hii ndio hali halisi wakuu juu ya mambo haya ambayo nimeyafanyia
kwa kina.
Pinda anaonekana ni tishio kwa wataka Urais ndani ya CCM.
[/SIZE]