Ukweli kuhusu mgomo wa UDOM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli kuhusu mgomo wa UDOM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Naibili, Jul 10, 2011.

 1. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,681
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  ​Kumekuwa na upotoshaji mwingi tangu kutokea na mgomo wa chuo kikuu cha dodoma.
  Ikumbukwe kuwa mgomo uliopelekea kufungwa kwa Chuo Cha Sanaa Na Lugha Cha Chuo Kikuu Cha DODOMA mnamo tarehe 22 mwezi wa saba unatokana na mgomo wa awali wa mwezi wa 12 katika chuo hicho uliopelekea serikali kuwatuma Waziri Wa Mambo Ya Ndani Na Mwenyekiti Wa Bodi Ya Chuo
  Kikuu Cha Dodoma Mh Shamsi Vuai Nahodha, na waziri wa elimu Mh shukuru kawambwa, kwenda chuoni hapo kumaliza mgomo huo, na tunaweza kusema walifanikiwa kwa Asilimia mia moja baada ya kuwaahidi wanafunzi wa chuo hicho cha sanaa na lugha kuwa, kwanza kukubali kuwa madai ya wanafunzi hao ni ya msingi, ni kisha kuwaahidi kupata mafunzo kwa vitendo kwa korsi zote ambazo hazikuwa na mafunzo kwa vitendo katika chuo hicho, katika makubaliano hayo Waziri aliagiza uongozi wa chuo hicho kufanya maandalizi yote kwa wanafunzi hao kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo, kwa maana kwamba kuwatafutia mahali pa kufanyia mafunzo hayo kwa wanafunzi hao na kuahidi kuwa pesa zote kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kutolewa na bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu. Hiyo ilikuwa asubuhi na mapema.
  Kwa kile kilichoonekana ni utekelezaji wa agizo la waziri, uongozi wa chuo kikuu cha dodoma ulichukua hatua kwa kuanza ufuatiliaji wa sehemu za kufanyia mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wote. Wakianza kwa kwenda huku na kule kutafutia wanafunzi sehemu ya kufanyia mafunzo kwa vitendo huku hivo ikipelekea baadhi ya wanafunzi kukosa vipindi kwa kile kilichoonekana kuwa walimu wameenda kutafuta mafunzo kwa vitendo, na matunda yake yalionekana kwani watu walianza kupangwa kuwa fulani atafanyia sehemu fulani, mwingine huku, mwingine kule kulingana na sehemu zilizopatikana ili mradi tu kuhakikisha kila mtu anapata sehemu ya kufanyia mafunzo hayo. Hizo ikiwa ni hatua za mwishoni. Baada ya hapo wanafunzi wakawa wanasubiri fedha kwa ajili ya kuwawezesha kufanya mafunzo kwa vitendo. Kama hiyo haitoshi wanafunzi wakaomba kwa uongozi wa chuo chao kupitia mshauri wa wanafunzi, kuwa wahakikishe fedha zinaingia kabla ya kuanza mitihani ya mwisho na wakaahidiwa kuwa kufikia tarehe 14 ya mwezi wa sita fedha zao zitakuwa zimeingia au ndo zitakuwa zinaingia.
  Kilichopelekea mgomo wa sasa
  Wanafunzi wakiwa hawana hili wala lile wakiendelea na masomo kama kawaida tarehe 9 siku ya alhamisi mwezi wa sita,ghafla hali ya hewa ikachafuka kila mwanafunzi akaanza kuwaza la kwake, mara watu wakaanza kuulizana maswali yasiyo na majibu kwa wanafunzi hao wa chuo cha sanaa na lugha, hiyo ni baada ya tangazo kutoka uongozi wa chuo hicho kueleza kuwa Tume ya Vyuo Vikuu imekataa wanafunzi ambao hawana mafunzo kwa vitendo katika kozi zao kwenda, wakiwa na maana kwamba watakao kwenda ni wale tu ambao kozi zao zimeelezewa kwenye prospectus ya chuo hicho ambayo kwa mujibu wa tume ya vyuo vikuu hiyo ni kama msaafu au biblia kwa wanafunzi hao ndo zitakazo kwenda mafunzo kwa vitendo ambazo ni kumi na tatu.
  Ninachojiuliza mimi ni katika tukio kama hilo ni mda gani ushawishi kutoka kwa viongozi au kiongozi fulani wa chama cha upinzani kaenda kuwashawishi wanazuoni hawa, ifikie mahali serikali iache kutapatapa na kutumia wanafunzi kama mradi wao wa kisiasa, ambao wanapenda kuona wanachanga fedha kwa ajili ya kumchangia mgombea wa chama tawala kuchukua fomu, ambao wanapenda kuona wanachuo wakitoa tamko kuwakemea wapinzani wanaotoka nje ya ukumbi wa bunge kugomea hotuba ya rais, viongozi ambao wako tayari kuona wanafunzi wanahuzuria kwa wingi kwenye mikutano yao, hawapendi kuona wanafunzi wanahama chama chao na kuhamia chama kingine tena kwa wingi kiasi cha kufanya tawi la chama chao kubaki na viongozi, hawapendi kusikia wanafunzi wamewachoka. Kiasi cha mawaziri wao kukaririwa wakiahidi kuwakomesha wanafunzi wa chuo hicho.
  Kilichotokea baada ya tamko la tume ya vyuo vikuu, hapo mgomo ulipoanzia kwa wanafunzi kumtaka kiongozi wa wanafunzi kutoa tamko kuhusu hatma yao, lakini kama katiba ya serikali ya wanafunzi isemavyo juu ya mgomo kuwa lazima upitishwe na bunge la wanafunzi na kutiwa sahihi na kiongozi wa wanafunzi, na hivyo ndivyo ilivyofanyika, Kikao cha dharura cha Bunge la wanafunzi kikaitishwa na kuona kuwa kulikuwa na haja ya kuishinikiza serikali kushughulikia madai yao ya kuruhusiwa kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo pamoja na kupatiwa fedha kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo, hivyo ndivyo ilivyokuwa mgomo ukaanza rasmi siku ya ijumaa ya tarehe kumi ya mwezi wa 6, 2011.
  Jitihada za serikali kumaliza mgomo.
  Serikali kama kawaida haikosi kufanya jambo liwe la mbolea au laa, siku ya jumapili usiku mnamo saa 6, baada ya wanafunzi kudai watapeleka madai yao bungeni siku ya jumatatu ya tarehe 13, 2011 serikali ikaanza kuhaha kuzima maandamano yaliyopangwa kufanyika jumatatu kuanzia saa kumi alfajiri, wakamtuma makamu mkuu wa chuo hicho Pro. Idrisa kikula kuwaeleza wanafunzi kuwa serikali imekubaliana nao na watakwenda mafunzo kwa vitendo, wanafunzi kama kawaida hawakupenda siasa kwani wao wanasomea taaluma ikiwamo ya siasa, hawakutaka kudanganywa na wanasiasa hawakukubaliana na mkuu wa chuo huyo aliyekurupushwa usiku huo wa wanasiasa ambao walikaa kimya tangu siku ya ijumaa ambapo mgomo ulitangazwa kana kwamba hawajui nini kinaendlea chuoni hapo au kana kwamba jambo hilo ni geni kwao, wakisahau hata kauli walizotoa chuoni hapo kuwa serikali haishindwi jambo lolote iliyotolewa na waziri mkuu Mh Mizengo pinda. Huku akisahau kuwa serikali anayoitumikia imeshindwa mambo mengi. Wanafunzi wakaandamana kama walivyopanga wakaamkia mjini kama kawaida polisi hawakukosa kuzuia maandamano hayo wakafanikiwa kuyazima baada ya kuwapiga wanafunzi hao mabomu ya machozi pamoja na vipigo vya kutosha, lakini ilipofika jioni wanafunzi wakaachiwa na wakarudi chuoni kujumuika na wenzao. Lakini mimi najiuliza mkuu wa chuo hicho anaposema siku moja kabla ya maandamano hayo wanafunzi walikwenda mjini dodoma kununua mafuta kwa ajili ya kupambana na polisi sasa kama ni kweli mbona kama kulitokea mapambano na polisi mbona hayo mafuta hayakutumika, yeye hizo habari kaziokota wapi? Maana kama polisi waliwapiga wanafunzi na wanafunzi hawakufanya jambo lolote na mpaka chuo kinafungwa hakuna jengo lolote la chuo lililoharibiwa na wanafunzi katika mgomo huo wa amani uliodumu kwa siku tatu. Na tukio hilo linamfanya mkuu huyo wa chuo kuwa ni mwongo na taarifa anazopata zinaonekana si za kweli.
  serikali badala ya kujibu hoja za wanafunzi wakajikita kwenye kuwazuia waandishi wa habari kutangaza habari za mgomo huo, ikiwa ni pamoja na kutawasikiliza wanafunzi na kweli kana kwamba hakuna kilichotokea siku hiyo Television ya taifa ikaa kimya kama vile hawakuwepo dodoma au hata hawakuwepo bungeni ambapo kuliimarishwa ulinzi ili wanafunzi wasiweze kusogelea maeneo hayo. Siku hiyo hiyo ya jumatatu naibu waziri wa elimu akijibu swali la mh felix mkosamali alisema serikali imepanga milioni 383 kwa wanafunzi 1260, kauli hiyo ya waziri ikikinzana na ya mkuu wa chuo hicho ambaye alisema fedha kwa wanafunzi wote kwa kozi ambazo hazina mafunzo kwa vitendo inakadiriwa kuwa ni 1.6 bilioni hapo wanafunzi akili zikawacheza kuwa hilo ni changa la macho, wakamtaka waziri afike awaambie kwa kinywa kama walivyofanya mara ya kwanza. Kama kawaida waziri kwa kile kinachodhaniwa na wanafunzi ni kushindwa kuja kudanganya kwa mara ya pili. Hapo sasa ikawa ni akili kumkichwa waziri hataki kuzungumza na wanafunzi bali anaongea na waandishi wa habari juu kwa juu. Akitaka wanafunzi waamini kile anachoongea na waandishi wa habari kuwa kozi tajwa ndo zitakazo kwenda field, na kwa mujibu wa prospectus ya chuo ni kozi kumi na tatu kati ya kozi 40 chuo kizima zinabaki kozi 27 ambazo hazina mafunzo kwa vitendo, sasa waziri anang’ang’ania wanafunzi waamini kuwa serikali imesikia madai yao waache kugoma kwani kozi tajwa zitakwenda mafunzo kwa vitendo, hataki kuja kwa wanafunzi kuwaeleza kwa kina kama walivyofanya mara ya kwanza na wanafunzi wakaamini na si wanafunzi tu bali hata uongozi wa chuo wakiwamo maprofesa na madaktari wote wakapigwa changa la macho.
  Nini suluhisho la mgomo udom
  Hata leo watu wafukuzwe kwa kudai haki yao, hilo si suluhisho, cha msingi sirikali wakubali mahali walikosea na kuwapa wanafunzi hawa mafunzo kwa vitendo kama madai yao ya msingi kwani chuo hiki hakijawahi kuwa na mgomo ambao unatokana na tatizo lingine tofauti na hilo. Hilo ni dai la msingi kama ambavyo waziri Nahodha alikiri lakini pia waziri mkuu alikubali hilo ni tatizo, ifike mahali chuo hiki kisitumike kama mtaji kwa wanasiasa kwa shughuli zao za kisiasa na pale mtaji unapokufa wanageuka mbogo,lakini pia viongozi wa chuo wasikubali kutumika kwa wanasiasa kwani matokeo yake yameonekana mwisho wake wanakuwa wakiahibika pamoja na taaluma zao, hiyo si sawa. Lakini pia waandishi wa habari watumike kwa mujibu wa taaluma zao, kwani kukubali kutumika na serikali tu pamoja na uongozi wa chuo, wanakuwa wanapotosha umma kwa mambo ya msingi kama haya watu wanatakiwa wafahamu ukweli wa jambo lenyewe. Hata wanaporipoti habari zao kuhusu chuo kikuu cha dodoma wanaegemea upande mmoja wa mlalamikiwa, hii si haki na wala si sahihi wajaribu kuwashirikisha na wanafunzi kujua ukweli wa jambo lenyewe. Ifahamike kuwa wanafunzi wanachukia sana upotoshaji wa habari zinazowahusu wenyewe hiyo imekuwa ikipelekea baadhi ya vyombo vya habari kufukuzwa na wanafunzi mfano mzuri ni TBC[SUB]1[/SUB] wamekuwa wakikumbwa na kadhaa hiyo ya kufukuzwa na wanafunzi kwa kile kinachodaiwa uchakachuaji wa habari zao.
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  poleni ndugu zangu, kwa namna iwayo yote inakuja siku yatakuwa ourstoria, tafadhali msijesahau njia mliyopita kufika huko mtakakokuwa kila mmoja wenu (jambo/tendo baya huugharimu utakatifu wa mtu) piganieni haki yenu maadam kwa macho na akili zenu mnaiona ipo!!! kwa mujibu historia ni mtu mmoja tu ameripotiwa kuwahi kusimamisha wakati- wa zama zetu, mvua tu imewashinda!!!! wausimamishe muda kwa utakatifu gani walionao?
   
 3. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kazi ya magamba hiyo, kuwapa wanafunzi field wanaona gharama wakati wenyewe wanatanua kwenye mishangingi ambayo garama yake kwa siku moja ni sawa na karibu wiki 6 za field kwa mwanafunzi mmoja. hawa jamaa wezi sana nadhani wengi wenu 2015 mtakuwa makini sana kupiga kura zenu
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Yaani hata chuo cha VETA wana mafunzo kwa vitend,vyuo vya ualimu vina mafunzo kwa vitendo,vyuo vya kariakoo vina mafunzo kwa vitendo,vyuo vya hoteli menejiment vina mafunzo kwa vtendo.........sasa Chuo kikuuu unamaliza bila mafunzo kwa vitendo!!!!!!!!!!!!??????????
   
 5. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2011
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280
  I'm amazed why am not surprised with this.., am I ok??
   
 6. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Wanafik nyie..s ndo mlimchangia J.k Milion kadhaa pale Nyerere square akachukue form ya urais?wala ata amuamink makada nyie...wenzenu Udsm wametngsha kberit juz..vjana wakaingia mzgon jana wakaingziwe mpunga..
   
 7. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2011
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Poleni sana ndugu zangu wa UDOM.

  However, ningependa kuona au kupata maelezo kuhusu kozi ambazo zinaelezwa kuwa hazina mazoezi kwa vitendo. Kama wewe ulidanganywa kuwa degree ni degree, ukaenda chuoni bila kujua utasoma nini na utaajiriwa wapi hiyo ni juu yako. Wanafunzi wengi katika ngazi ya Chuo Kikuu hawajui wanachotakiwa kujua/kufundishwa kwenye kozi anayosomea. Sijaona mwanafunzi anayeuliza "Curriculum" ya somo ambalo anasoma hinyo mwalimu huweza akaingia akafundisha anachokitaka na wanafunzi wasijue kuwa ndicho au sicho walichotakiwa kujua.

  Kama kweli kuna kozi ambazo kwenye "Course curriculum" (siyo prospectus) haionyeshi/haisemi kuwa wanafunzi watakwenda mazoezi ya vitendo, then hawana haki ya kudai hayo mafunzo. Utakuwa ni umbumbumbu wa hali ya juu kama utafukuzwa kwa kudai haki ambayo hustahili kisheria.

  Fikiria, tambua na amua ukiwa na taarifa sahihi. Huo ndio msingi wa wasomi wa Chuo Kikuu.
   
 8. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Dah........Poleni sana GODLIZEN.....Inasikitisha sana...

  Kwani hayo mafunzo ya vitendo yameainishwa kwenye mtaala wa kozi husika(course curriculum)?.....
   
 9. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  habari yako nzuri bt kuna vitu umepotosha ntaja kukukosoa baadaye
   
 10. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  wazo tatizo sio walimu tatizo ni kata na vitu vyote vya kata ni mali ya usanii..
   
 11. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #11
  Jul 10, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Rekebisha kidogo ni mwezi wa "sita"
  Pole sana ndugu zetu! Serikali ya ccm imebeba dhambi ya kubwa kwa watz!
   
 12. m

  mbaba Member

  #12
  Jul 10, 2011
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  wengi tunashindwa kuelewa,prospectus sio qurain wala bible inaawezabadirishwa zenyewe zimekaa kisiasasiasa an then kudai haina maana iwanufaishe wao tu,lahasha nifaida kwa next generation achen ubinafisi,nakumbuka Udsm mwaka wa3 waligoma kushinikiza nyongeza ya accomodation hadi kufikia elfu5,je wao ilikua inawasaidia nin,si wangetulia wanamaliza but kwa faida ya wadogo zetu wakafanya ivo,hakuna course isio na vitendo..sias izi,ata hao maprof wameshusha hadhi yao kuaandaa kitu kisicho na vitendo thn leo twaambiwa prof hakosei
   
 13. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #13
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  nahisi kuna fungu kubwa limetengwa kwa ajili ya kuwasaka wanafunzi popote walipo majumbani mwao kutoa maelezo, uhakika huo ninao coz kuna mdogo wangu amefuatwa na gari ya serikali na maofisa kadhaa wa serikali wakiwemo wahadhiri wa udom kwenda kumhoji.
   
 14. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #14
  Jul 10, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mafunzo kwa vitendo kwenye kozi za siasa hata mimi sielewi! Halafu muda mwingi si mnafanya siasa na MH LEMA? , nadhani inatosha! Subirini Padre akiwa rais!
   
 15. M

  Mtei Member

  #15
  Jul 10, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  jaman naomba 2elewe kwenye jamii kila mtu anahaki ya kuchagua anakotaka walio mchangia kikwetwe ni wanachama wa ccm tawi la Udom na sio kuwakilisha wanafunzi wa udom, mbona lema alikuja na alijaza watuwengi sana kuliko hata hao walioenda kwa kikwete pamoja na kukusanya wanachama wa ccm kwenye vio vikuu vyote
   
 16. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #16
  Jul 10, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Mnakula dhambi yenu ya kumchangia milion 1. Nashangaa chuo kikuu watu wanakuwa na fikra za kimagamba kweli na amini ule usemi uliambiwa prof. Chachage kwamba africa si lazma tuwe na vyuo vikuu badala yake tuwe na vyuo vya ufundi kama veta.
   
 17. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #17
  Jul 10, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Mnakula dhambi yenu ya kumchangia milion 1. Nashangaa chuo kikuu watu wanakuwa na fikra za kimagamba kweli na amini ule usemi ulioambiwa prof. Chachage kwamba africa si lazma tuwe na vyuo vikuu badala yake tuwe na vyuo vya ufundi kama veta.
   
Loading...