Hakuna uhusiano wowote kati ya pesa na mapenzi ya kweli, wengi wanatoa pesa na hawapati ya mapenzi ya kweli, wengi wanapokea pesa na hawatoi mapenzi ya kweli. Pesa zinatafutwa na waliowengi kutokana na ugumu wa maisha, wengine sio ugumu wa maisha bali ni kutokulizika na tamaa tu kupata vitu vizuri na starehe.
Wanawake wengi shughuli zao / ajira zao zinawapatia kipato kidogo hivyo hakiwatoshelezi kimaisha, wanaamua kutoa utu wao ili wapate pesa za kujikimu zaidi, wengine wanamaisha yao mazuri na vipato vinavyojitosheleza lakini tamaa ya pesa na mali nyingi zaidi huwafanya watoe miili yao kwa mijibaba na mikaka yenye tamaa za anasa - kimwili. kumbuka hapo hakuna mapenzi ya kweli hata kidogo, ndo mana kuna wanawake wakishajijenga tu kupitia mwanaume fulani a.k.a ATM mashine wanasepa.
Mapenzi ya kweli ni yale yasiyo na usaliti ndani yake, yenye kuridhika kwa kila mmoja ndani ya penzi hilo, na yenye real commitment - wangu mpaka kufa.
Nb: kumbuka sio rahisi sana kuwabadilisha watu ktk karne hii ambayo maisha yamebadilika sana na ni magumu sana. Hivyo pesa itabaki kuwa nguzo ya kila kitu, wanaotaka mapenzi kwa pesa watayapata ila si ya kweli. Wapo wachache wenye kuridhika na maisha yao basi ndo hivyo tunaendelea, yanafanywa wanaugua - wanakufa, wengine wanazaliwa.
Ila changes ni wewe simama wewe kama wewe huzikwi na mtu.