Ukweli kuhusu huduma za serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli kuhusu huduma za serikali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kakende, Sep 20, 2012.

 1. Kakende

  Kakende JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 2,734
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwa sasa kuna juhudi kubwa ya kuhakikisha kuwa tatizo la foleni linapunguzwa katika jiji la Dar es salaam. Lakini kwa upande wangu nina wasiwasi na hali ya huduma za serikali hasa kwa upande wa train itakayokuwa inasafirisha abiria ndani ya jiji.

  Wakati kampuni ya ndege ya serikali (ATCL) inaanza kutoa huduma niliwahi kuongea na rafiki yangu kuwa nina wasiwasi na utendaji wa wafanyakazi wa serikali, hawako serious. Haikuchukua muda tukasikia kuwa ndege pekee ya ATCL imepata ajali.

  Wasiwasi wangu ni kwamba kuna uzembe mkubwa ndani ya serikali katika kipindi hiki, ndiyo maana tunaona inafikia hatua wanafunzi wanakwenda sekondari wakiwa hawajui kusoma. Vivyo hivyo sina uhakika na treni ya serikali itakayokuwa inasafirisha abiria ndani ya jiji, inaweza ikawa ni kaburi linalotembea. Hayo ni maoni yangu juu ya huduma za serikali ingawa wengi wataniona mchawi lakini palipo na ukweli lazima tuseme ili watu wajirekebishe
   
Loading...