Besta Mlagila
Senior Member
- May 29, 2018
- 101
- 191
SERIKALI ilitangaza kuyapandisha hadhi mapori ya akiba matano yaliyoko mkoani Kagera na kuwa hifadhi za taifa, Mei, mwaka jana.
Mapori hayo ni pamoja na Biharamulo, Burigi na Kimisi (BBK) pamoja na Ibanda na Rumanyika.
Kutokana na uamuzi huo, mapori hayo yatatengeneza hifadhi mbili za zaifa ambapo Biharamulo, Burigi na Kimisi zitakuwa moja zikitengeneza hifadhi ya Taifa iliyopendekezwa kuitwa Chato au Kimisi huku Ibanda na Rumanyika kila moja ikijitegemea.
Hatua ya kuyapandisha hadhi mapori hayo ina umuhimu mkubwa kwa wananchi waliopakana nayo hususani kwa mkoa wa Kagera na taifa kwa ujumla katika kukuza utalii na hifadhi ya mazingira.
====
26 AUG2018: Utalii wapiga hodi Kagera
Ni kutokana na kupandishwa hadi kwa mapori kuwa hifadhi za taifa… mkoa wajipanga kutumia fursa hiyo kiuchumi…
SERIKALI ilitangaza kuyapandisha hadhi mapori ya akiba matano yaliyoko mkoani Kagera na kuwa hifadhi za taifa, Mei, mwaka huu.

Hatua ya kuyapandisha hadhi mapori hayo ina umuhimu mkubwa kwa wananchi waliopakana nayo hususan kwa mkoa wa Kagera na taifa kwa ujumla katika kukuza utalii na hifadhi ya mazingira.
Kupandisha hadhi kwa mapori hayo, kutawawezesha wananchi wanaoishi mkoani Kagera kupata fursa za kuanzisha na kuendesha kampuni za utalii kwa ajili ya kupokea wageni wanaoenda kwa lengo la kutembelea hifadhi hizi.
Wawekezaji kutoka mkoa wa Kagera watapata fursa za kuwekeza kwenye ujenzi wa hoteli za kisasa, nyumba za kulala wageni na kambi za kitalii za aina mbalimbali.
Kama ilivyo kwa mikoa ambayo ni kitovu cha utalii ya Arusha na Kilimanjaro, kuwapo kwa uwekezaji huu kutasaidia kukuza mitaji kwa wafanyabiashara wa mkoa huu na wakati huo huo kutoa ajira kwa jamii inayozunguka maeneo haya.
Aidha, wananchi watapata masoko ya bidhaa zao hasa wale wanaopakana na hifadhi hizi pale watalii wanapopita katika maeneo yao, hivyo kusaidia kukuza vipato vyao bila kusahau fedha za kigeni.
Kuwepo kwa hifadhi hizo kutasaidia kuimarisha miundombinu hasa ya barabara zinazotokea maeneo ya vijijini kuelekea hifadhini zitakazokuwa zinatumika kwa ajili ya shughuli za utalii lengo ikiwa ni kufanya utalii kufanyika bila kumchosha mgeni.
Hifadhi hizo zinapakana na vijiji 58 vilivyoko katika Wilaya za Biharamulo, Muleba, Karagwe na Ngara mkoani Kagera pamoja na Chato, mkoani Geita.
Hata hivyo, hifadhi hizo mpya zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na uharibifu wa makusudi wa vigingi vya mpaka (beacons) unaofanywa na watumiaji haramu wa mapori hayo.
Changamoto nyingine ni pamoja na askari kugeuka waswagaji na wachungaji wa ng’ombe pale mifugo hiyo inapokamatwa na kushikiliwa kusubiri taratibu zingine za kisheria.
Aidha, maofisa ambao wanafanya kazi katika hifadhi hizo pia wanataja uhaba au uchakavu wa vitendea kazi na miundombinu kama magari, mahema na boti vinapokosekana vinafanya utendaji kazi kuwa mgumu.
Uchakavu wa majengo ya vituo pamoja na ukosefu wa huduma muhimu kama maji na umeme katika vituo vya nje.
Changamoto nyingine kubwa ni Unyemeleaji wa maeneo yaliyohifadhiwa (Encroachment) mfano Nyarwambu, Ichwankima na Nyakahura(Amsali). Hifadhi hizo pia zimezungukwa na vijiji kwa sehemu kubwa na hata kwa upande wa Magharibi upande wa Rwanda kuna vijiji na Kambi ya wakimbizi ya Mahama.
MKAKATI KUJIIMARISHA
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) limeshatenga Sh. bilioni 3.9 kwa ajili ya kuimarisha na kuendeleza hifadhi hizo mpya pamoja na nyingine mbili za Ibanda na Rumanyika.
Ofisa wa TANAPA anayesimamia kipindi cha mpito, Damian Saru, Alisema hivi karibuni kuwa fedha hizo zitatumika katika kuimarisha ulinzi, kuainisha mipaka kwa kuwashirikisha wananchi na kujenga miundombinu ya utalii na utawala.
Kazi zingine, kwa mujibu wa Saru, ni kuweka mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa mapato, kuandaa na kuendeleza miundombinu ya utalii, kuandaa na kuendeleza vivutio vya utalii.
Aidha uongozi wa mkoa wa Kagera unaeleza kwamba umejipanga kikamilifu kupokea wawekezaji na watalii kwenye hifadhi hizo na jinsi fursa zilizopo zitakavyotumika kwa kuwaelimisha wananchi na wadau wote ndani ya na nje ya mkoa juu ya mabadiliko ya mapori ya akiba kuwa hifadhi za taifa.
Katibu Tawala wa Mkoa huo, Diwani Athumani, alisema kabla ya mabadiliko hayo, mkoa ulikamilisha Operesheni Ondoa Mifugo iliyofanikisha kuondoa mifugo na wavamizi wote waliokuwa kwenye mapori hayo na hali ya uoto wa asili imeanza kuimarika na wanyamapori wamerejea na kuanza kunawiri.
“Majangili waliokuwa wanajificha kwenye kivuli cha kuwepo kwa mifugo hifadhini kwa kujifanya wachungaji nao wamepungua
Chanzo: Nipashe