Ukweli kuhusu Dr. Slaa

Ukweli kuhusu Dr. Slaa

LINCOLINMTZA

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2011
Posts
1,639
Reaction score
519

Taharuki imetanda juu ya wapi alipo Katibu mkuu wa Chadema Dr.Wilbroad Slaa. kila mtu anazungumza lake kwa kadri anavyoelewa. wengine wakisema yupo kwenye maandalizi ya vikao vya kamati kuu na wengine wakisema amejificha kwa sababu hakubaliani na maamuzi ya kumleta EL kwenye chama.

Mimi kama kada wa chadema wa muda mrefu na mwanasheria mzoefu nimefanya utafiti na nimejiridhisha bila shaka yoyote kuwa hali si shwari ndani ya chadema licha ya juhudi mbalimbali zinazofanywa kuonesha kuwa hakuna tatizo.

Ukweli ni upi? Ukweli ni kuwa Dr.Wilbroad Slaa hakubaliani na maamuzi yaliyofanywa na kamati kuu ya Kumleta EL na kumpa nafasi ya kugombea Urais bila kufanya utafiti wa kutosha. Slaa anadai kuwa maamuzi haya ni ya haraka mno na chama kilitakiwa kijitafakari zaidi kabla ya kumpa ridhaa ya kugombea Urais.

Ikumbukwe siku ya jumapili tar.26 wakati UKAWA wamefanya kikao cha mwisho na EL Dr.Slaa alikuwepo na baada ya hapo akapotea kabisa na hajaonekana hadharani hadi leo.


Ukweli ni kwamba ndani ya kikao kile chs jumapili Slaa alionesha msimamo wake juu ya EL na kudai kuwa watanzania hawatatuelewa wakituona tukipita kumsafisha mtu yuleyule tuliyemchafua awali.

Hivyo Slaa akatoa masharti mawili makubwa. La kwanza ni EL aitishe Press na ajisafishe mwenyewe kabla hajatangaza kuja UKAWA. Aruhusu waandishi wamuulize maswali yote kuhusu Richmond na kashfa nyingine ikiwemo umiliki wa jengo la Ubalozi wa S.Africa na EL ajibu hoja zote kwa maelezo ya kueleweka. Sharti la pili la Slaa ni kuwa EL asupewe nafasi ya kugombea urais kwa sasa kwani ni ngumu kupima dhamir yake kama ni ya kweli. Slaa akapendekeza EL aje CHADEMA na aisaidie UKAWA kuchukua dola bila kugombea Urais.

Lakini Mbowe akampinga sana Slaa na akasema Katibu mkuu hawezi kuweka "ultimutum" ya EL kujiunga na chadema. Mbowe akapuuza mawazo ya Slaa na akaagiza mchakato wa kumpokea uanze mara moja na kesho yake Mbatia akaambiwa atoe tamko la kumkaribisha EL UKAWA.

Hali hii ilimfanya Slaa kujihisi mnyonge na aliyepuuzwa. akahisi hathaminiki ndani ya chama licha ya mchango mkubwa alioutoa kukijenga chadema. jambo la ajabu Mbowe alipopelekewa taarifa hizo alijibu kwa kejeli kuwa liwalo na liwe. yani yuko tayari kumpoteza Slaa na kumkumbatia EL.

Haikujulikana wazi Mbowe ana maslahi gani katika hili la EL na kwanini aamue kuwa na msimamo mkali hivyo wa kumtetea EL.

Inadaiwa tangu jumapili Slaa alipoachana na viongozi wenzie wa UKAWA hadi sasa yupo ndani hajatoka na hakuna mgeni anayeruhusiwa kumuona. Anautumia muda huu kusali na kushauriana na marafiki zake kwa njia ya simu (wengi ni maaskofu) juu ya nini afanye katika kipindi hiki.

Wengi wamemshauri aachane na siasa na ajiuzulu nafasi yake ya SG ndani ya chadema wazo ambalo limeungwa mkono na mkewe Josephine na baadhi ya watu wenye misimamo mikali.

Baada ya ushauri huu mkewe wa Slaa ameonekana kufurahia na ameanza kuelezea kwenye mitandao ya kijamii. Jsna kupitia kundi la Nyakahoja la whatsapp Josephine alisema mumewe ameteseka sana na chama hiki na amekitoa mbali sana. Dr.Slaa alivunjika mkono na hadi sasa ana ulemavu wa kudumu kwa sababu ya kuitetea chadema. yeye mwenyewe alipigwa na kuharibiwa mimba mwaka 2011 kwa sababu ya chadema halafu leo wanapuuzwa kama vile si chochote ndani ya chama.

Anasema ni afadhali Mbowe angesikiliza ushauri wa Slaa wa EL kujisafisha kwanza kabla hajaja chadema maana kuja bila kujisafisha ni kuwaweka viongozi wote wa chadema kwenye mtego.

Madai ya Mbowe kupewa fedha na EL. Yapo madai kuwa Mbowe amehongwa sh. bil 12 ili kumpokea EL. Fedha hizi ameziweka kwenye akaunti yake binafsi na amewawia kidogo wale aliowaona wanaweza kumchallenge. baadhi ya watu waliopata mgao ni wajumbe wa kamati kuu ili kuwaziba mdomo. na si wajumbe wote bali wale wachache viherehere. baadhi yao ni Godbless Lema (anadaiwa kupokea milioni 120), Peter Msigwa (mil 135), Tundu Lissu (mil 180), Salum Mwalimu (Mil 180).

Pesa hizi ndizo zinazodaiwa kuwafumba macho kamati kuu na kuamua kumpitisha EL bila kufikiri mara mbili. Kitu cha ajabu kamati kuu imefunga dirisha la kuchukua fomu na kusema eti kamati kuu inamuunga mkono Lowassa tu.

Huu ni ujinga ambao hata CCM haiwezi kuufanya. Kamati kuu inatakiwa kuwa neutral. kamati kuu haitakiwi kuwa na mgombea. kamati kuu haitakiwi kuzuia watu kuchuku fomu. acha wachukue wengi kadri iwezekanavyo halafu wachujwe abaki mmoja.

Kama EL anajiamini yeye ni bora zaidi na ana nguvu zaidi kwanini anaitumia kamati kuu kuzuia watu wasichukue fomu? Siku chache zilizopita watu walilalamikia kamati kuu ya CCM kuwa ilikua na mgombea wake mbona hawaoni hili la kamati kuu ya chadema?

Ikiwa madai haya ya kuhongwa kamati kuu ni ya kweli basi chadema inaelekea ukingoni katika siasa za nchi hii. jambo la ajabu viongozi wanaodaiwa kuhongwa akiwemo Mbowe hawajakanusha habari hizi. halafu wanatuma ujumbe kw Slaa eti wakamsihi asiondoke. wajumbe wote waliotumwa wakaishia getini na hawakufunguliwa mlango. mlitegemea mfunguliwe mlango wakati kuna madai mmehongwa na hamjakanusha? kanusheni kwanza ndio muende kumuona Slaa. Au mnataka mkamhonge na yeye? Kama msipokanusha habari hizo mkienda mtafungiwa tena nje maana nyumbani kwa Slaa hakitaingia chochote kilicho kichafu.

Response ya Chadema. ni kama vile hawajali yanayoendelea. na bahati mbaya zaidi vijana wa chadema wameanzisha movement ya kumtukana Josephine kuwa yeye ndio anamponza mumewe. kwenye mtandao wa jamiiforums, facebook ma magroup ya whatsapp wanamtukana sana.

kwenye group moja la wabunge wa chadema wameanzisha movement iitwayo "Josephine Bring Back our Dr". wengine wanamwita mwanamke mpumbavu, wengine wanasema ana hasira ya kukosa ufirst lady, lakini wengine wamefika mbali na kudai anatumiwa na TISS na CCM.

Kimsingi madai yote hapo juu hayana mashiko. Josephine hatumiwi na TISS wala CCM. Hana uchungu wa kukosa ufirst lady wala nini. anachofanya ni kutetea haki ya mumewe. haki ya kuthaminiwa, haki ya kuheshimiwa, haki ya kutoa mawazo yake na kusikilizwa.

Hivi mumeo anapuuzwa kwenye vikao vikubwa vya maamuzi halafu unaambiwa waliompuuza wamehongwa fedha na hawajakanusha habari hizo, halafu ukimtetea mumeo unaambiwa unatumika na TISS. this is ridiculous.

Hakuna cha TISS wala CCM mchawi wa chadema ni chadema wenyewe na mchawi wa ukawa ni chadema. Hizi porojo za TISS ni mbinu inayotumika ili Slaa akiamua kutangaza msimamo wake ionekane anatumiwa na CCM. Chadema acheni siasa za kitoto. hivi Slaa aliyepigania chadema zaidi ya miaka 20 akitoa sadaka maisha yake kwenu ndio wa kutumika na TISS leo aache kutumika huyo EL aliyekuja jana? this is very interesting. chadema kitaingia katika rekodi za dunia za kuwa chama cha kwanza kumtilia shaka mwanachama wake wa miaka 20 na kumuamini mwanachama wa siku moja.

Nini kifanyike? Jambo linaloweza kufanyika na kusaidia kuiokoa chadema na UKAWA kwa ujumla ni mediation. zitafutwe mbinu nzuri za kukutana na Slaa na kuongea nae. aeleze yanayomhusu na chama kioneshe concern ya kuyatatua.

pia kwa kuwa Josephine anaonekana kuwa na nguvu kubwa sana kwa Slaa hivi sasa ni bora Watafutwe wanawake wenye heshima ndani ya chama wakaongee nae. kwa mfano Mama Regina Lowassa, mama Ntagazwa na mama Mbatia waende kumuona mwanamke mwenzao waongee nae. hii itasaidia kupunguza hasira za huyu mama maana tangu juzi anatukanwa mitandaoni akidaiwa ndiye anayemzuia Slaa.

Ni vizuri mambo haya yafanyike mapema maana taarifa zilizopo ni kuwa kufikia wiki ijayo kama chama kitakua hakijatoa msimamo kuhusu Slaa basi yeye atatangaza msimamo wake wa kujiuzulu wadhifa wake chadema na kuamua kuachana na siasa kabisa. kisa wataondoka nchini yeye na familia yake kwenda Italia ambapo ataishi huko kwa miaka mitano kabla ya kurudi nchini na kumalizia maisha yake Karatu. mipango ya Slaa kwenda kuishi Italia kwa miaka mitano inaratibiwa na shirika mija la kiroho la kanisa katoliki na maandalizi yanaendelea vizuri.

Hivyo basi ni vema kazi hii ikafanywa mapema na kwa umakini ili tusivuruge kazi yote ya kuijenga Ukawa na kuujenga upinzani nchini. ukweli ni kuwa Slaa akiamua kujiuzulu siasa za upinzani zitapoteza uelekeo na tutashindwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu kuanzia udiwani, ubunge hata urais. maana yake ni kuwa kazi yote iliyofanyika kuujenga upinzani inabomolewa siku moja na kuifanya CCM izidi kushamiri. na ikiwa Slaa ataondoka itachukua miska zaidi ya 100 kupata upinzani mwingine wenye nguvu kama huu. hivyo basi juhudi za haraka zinatakiwa.

Mwandishi wa makala haya ni ndugu A.N Chilongola, mwanachama wa chadema na mkurugenzi wa kampuni ya uwakili ya Chilongola &Advocates iliyopo Mabibo
Dar.anchilongola@gmail.com
 
Mwaka huu myanyooka tu wazee wa kijani na njano, mtajiita majina yote, mara watafiti, wanasheria, makada, wachambuzi n.k... Sisi kazi yetu ni moja tu: kuhakikisha CCM inatoka mdarakani.

Waswahili walisema mfamaji, haishi kuandika thread zakutapata Jf...

Tulieni dawa iwaingie taratiibu kabisa...
 
''Josephine hatumiwi na TISS wala CCM. Hana uchungu wa kukosa ufirst lady wala nini''
''
Hivi mumeo anapuuzwa kwenye vikao vikubwa vya maamuzi halafu unaambiwa waliompuuza wamehongwa.....''
''
hii itasaidia kupunguza hasira za huyu mama''

Quotes from a learned Brother!!


 
Duhhhh kwel hii n siasaa... vp mnyika nae..?????
 
Binafsi ninauheshimu sana msimamo wa Dr Slaa; Na sikuwahi kuamini hata siku moja kuwa Mbowe anaweza kumkaribisha EL CDM bila kwanza kuwa na masilahi ya namna fulani. Ni kweli EL ana following kubwa hasa vijijini lakini alipaswa kujisafisha kwanza. hii haraka haraka ya Mbowe and Co. inaleta wasiwasi sana. Yaani tupoteze watu makini ndani ya CDM ili tupate makapi ya CCM!!!!

EL alipaswa kujisafisha kwanza
 
Binafsi ninauheshimu sana msimamo wa Dr Slaa; Na sikuwahi kuamini hata siku moja kuwa Mbowe anaweza kumkaribisha EL CDM bila kwanza kuwa na masilahi ya namna fulani. Ni kweli EL ana following kubwa hasa vijijini lakini alipaswa kujisafisha kwanza. hii haraka haraka ya Mbowe and Co. inaleta wasiwasi sana. Yaani tupoteze watu makini ndani ya CDM ili tupate makapi ya CCM!!!!

EL alipaswa kujisafisha kwanza

Hajisafishe kivip wakat alishasema amechoka kuitwa fisadi mwenye ushaidi aende mahakaman kuna mtu ameenda kumfungulia kesi?
 
Ni mtu mjinga tuu ndio unaweza kumkataa El na naweza sasa kusema Dr. ameonesha ubinafsi wa hali ya juu labda ndio tuaanza kumtambua aina ya viongozi tunaowaamini. Padre anakuwaje na moyo mgumu namna hii kusamehe?
Lakini maamuzi yaliyofanyika ni kidemocrasia maana ni ya wengi lakn namshangaa Slaa kukomalia msimamo wake mwenyewe. Dr. alipokelewa kama lowassa baada ya kukatwa ka alivyokatwa lowassa.

Hii ndio inadhiirisha hakuna aliye juu ya chama wanachama wamesema mpokee lowassa katibu pekee aseme asipokelewe huu msimamo haukubaliki anapaswa abadilike.
 
Bandiko lako kwa kiasi kikubwa linatoa picha kamili na majawabu ya kutuvusha, mengine ya kuhongwa nakuachia wewe mimi simo ila ushauri ulioutoa nimeupenda inshallah na iwe hivyo.
 
Makubwa haya. LINCOLINMTZA hivi kumbe Dr. Slaa ana MKE? makubwa haya! Mwaka 2010 alikuwa "kaiba mke wa mtu" mwaka 2015 "mke wa mtu" kawa mke duh! Ama kweli LOWASSA kawachanganya wazee wa Lumumba. ...wadhamini tu tena wenye BVR karibia milioni mbili je October 25 itakuwaje?. Kazi mnayo mwaka huu.
 
Last edited by a moderator:
Hajisafishe kivip wakat alishasema amechoka kuitwa fisadi mwenye ushaidi aende mahakaman kuna mtu ameenda kumfungulia kesi?
Ule ushahidi waliosema wakina Mbowe na Dk Slaa umeyeyuka ghafla au ulikuwa ni wa uongo.....maana wao ndio walizunguka nchi nzima kwa kumtangazia jamaa kuwa ni fisadi....huku wakisema wana ushahidi mkononi.....sasa iweje leo ushahidi wao waufiche alafu waombe ushahidi mwingine.....au ushahidi wao una walakini........
 
Ni mtu mjinga tuu ndio unaweza kumkataa El na naweza sasa kusema Dr. ameonesha ubinafsi wa hali ya juu labda ndio tuaanza kumtambua aina ya viongozi tunaowaamini. Padre anakuwaje na moyo mgumu namna hii kusamehe?
Lakini maamuzi yaliyofanyika ni kidemocrasia maana ni ya wengi lakn namshangaa Slaa kukomalia msimamo wake mwenyewe. Dr. alipokelewa kama lowassa baada ya kukatwa ka alivyokatwa lowassa.

Hii ndio inadhiirisha hakuna aliye juu ya chama wanachama wamesema mpokee lowassa katibu pekee aseme asipokelewe huu msimamo haukubaliki anapaswa abadilike.

Naona umeongea kama mwanachama wa ukawa(kishabiki),weka mihemko pemben kisha usome tena unaweza kuelewa alichokiandika mkuu hapo juu
 
''Josephine hatumiwi na TISS wala CCM. Hana uchungu wa kukosa ufirst lady wala nini''
''
Hivi mumeo anapuuzwa kwenye vikao vikubwa vya maamuzi halafu unaambiwa waliompuuza wamehongwa.....''
''
hii itasaidia kupunguza hasira za huyu mama''

Quotes from a learned Brother!!



1. Hao wanaoeda kumuona hawafungulii sasa watamediate saa ngapi?

2. CHADEMA sio kitengo cha maaskofu wa katoliki hivyo hizo jitihada za kumpeleka Italy zinakihusu vipi Chadema?

3. Hivi mnajua maana ya wengi wape? Sasa mtu anapogeuka mungu mtu ndipo anapopuuzwa

4. Na sasa rangi halisi ya huyo mnaemwita mchumba/mke ndipo inapoonekana kama Mumewe angekuwa Rais kuna siku angemfungia ndani hivyo hivyo muanze kutafuta wanawake wa kwenda kumshauri mke ali aongee na mumewe

5. Hivi aliyesotea chama ni yeye peke yake?

6.Wale waliopata kusikia habari za vita wakati mwingine askari akiwa vitani anapojeruhiwa na kutoonesha matumaini ya kupona huwa anauliwa sio kwa sababu hakuwa na mchango bali ni kwa mstakabali wa kushinda vita

7. Ifike mwisho tusiendekeze miungu watu. Wengi wape ndio utaratibu katika kufikia mwafaka wa makundi
 
Nimependa umeandika kwa makini kwa kadri ulivyoweza! ila sasa Slaa akijiuzulu sawa bora kujiuzulu kuliko kwenda CCM maana tsunami itamkuta huko huko
 
wazo la el kujisafisha naliunga mkono. lkn km kweli anakipenda chama na taifa y ajitoe???? kuna ubaya gan el akigombea? as long as hata yy alitoka ccm na akapewa nafac agombee. ooooh siasa. upuuuz mtupu..... nampenda sla bt kura yangu kwa ukawa ipo palepale. wananch tushakubaliana na hiyo hali viongoz msituvuruge. i wish slaa angekua mgombea mwenza.
 
Dah,
Lizaboni kaja na wasifu mwingine; eti mwasheria na kada wa mda mrefu wa Chadema. Lowasa atawatesa sana watu wa Lumumba. Nawashauri muanzishe tredi za Magufu maana atapotea hevi hivi kwenye media.
.
 
Back
Top Bottom