Ukweli kuhusu audio ya Kinana na Nape huu hapa

Inkognito

Member
Feb 13, 2011
86
108
UKWELI KUHUSU AUDIO INAYOSEMEKANA KUWA NI YA KINANA NA NAPE HUU HAPA

Nimesikiliza audio zote mbili zinazoendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinazodaiwa kuwa ni za mazungumzo kati ya Nape na Kinana, kupitia audio hizo yapo mambo ambayo yanatia shaka kama kweli yametoka kwa wahusika wenyewe yaani Nape na Kinana licha ya ukweli kuwa wenyewe hawajakanusha wala kujibu chochote kuhusiana na audio hiyo.

Kwanza ni vema ikaeleweka kuwa siasa ni mchezo, na kwakuwa ni mchezo tukubaliane kwamba matamko yanayotolewa na mtu anayejiita ni mwanaharakati musiba dhidi ya Kinana, Makamba, Nape, Membe pamoja na watu wengine ni sehemu ya michezo ya kisiasa kwasababu zifuatazo.

1. Kwa uzoefu wa Kinana na Nape kwenye siasa za Tanzania ni jambo lisiloingia akilini kwamba wanaweza kupanga,na kutekeleza mipango yao inayohusu masuala nyeti yanayohusu chama na serikali hasa katika jambo kama la kumtuhumu kiongozi mkuu wa nchi na mwenyekiti wao wa chama Mheshimiwa Rais Magufuli, kufanya hivyo ni kuonyesha ni kwa kiasi gani ni wazembe katika kupanga na kutekeleza mambo yanayoweza kuhatarisha maisha yao ya kisiasa. Mambo kama hayo yanaweza kufanywa na watu ambao hawajawahi kuwa kwenye system za uongozi wa chama na serikali. Nape amewahi kuwa waziri, ni mbunge na amewahi kuwa mwenezi wa chama tawala, kama ingekuwa ni suala la kujadiliana kwa njia ya simu masuala nyeti yanayohusu chama au serikali basi audio nyingi zinazowahusu zingekuwa zimeshavuja na kusambaa kitambo, kwanini basi iwe sasa hivi?hapo kuna mchezo.

2. Kiumri, uzoefu, kicheo na kiitifaki Kinana anamzidi Nape kwa mbali sana, lakiniUkisikiliza audio zote mbili huoni uwepo wa nidhamu katika mazungumzo ya Nape kwa Mkuu wake kama Kinana, wanaongea ni kama watu ambao huwa wanakutana kijiweni, au washkaji tu ambao hawana agenda mahsusi, wanahamahama, mara waingize story kuhusu barua, mara hotuba ya jamaa, mara wataje majina ya watu wengine kwenye mpango wao nk, hiyo ni viashiria kwamba watu wao wawili kwenye audio hiyo hawapo siriaz na jambo husika ingawa kwa asili yake ni jambo kubwa.

3. Kwenye audio inaonekana ni kama vile Kinana hajui mkakati uliopo kwa upande wa media, haiwezekani watu wawili mpange jambo kubwa namna hiyo alafu upande mmoja uwe haujui kinachoendelea. Kwa namna jambo lenyewe lilivyo ilipaswa wawe wameshalijadili walipokutana, na sio kulirudia kwenye simu. Huo ushahidi kuwa malengo ya audio hiyo ni ili kuwaaminisha watu kuwa kuna mpango unafanyika kwa njia ya simu.

4. Kiongozi kama Rais mstaafu "Mkapa" sio rahisi sana kuwasiliana na mtu au Kiongozi mwenzake kama Kinana kuhusu masuala makubwa yanayomgusa jamaa kwa njia ya simu ya mkononi. Hii ni kwasababu kiusalama simu za mtu kama Rais mstaafu lazima zinakuwa monitored, hivyo ni rahisi kuvuja kwa siri, vinginevyo wafanye kikao cha siri. Kwa hiyo hoja ya Kinana kuongea na Nape kwenye simu eti akimwambia kuwa ameongea na Mkapa, tena bila aibu anamtaja kwa jina as if ni mshikaji tu wa kijiweni.

5. Kama kweli kuna conspiracy theory kati ya Nape na Kinana, basi suala la Kinana kuongea na Mkapa, au Nape kuongea na Mwandosya yasingefanyika kwenye simu, huo utakuwa ni uzembe wa hali ya juu. Mambo kama hayo kwa wakongwe kama hao hufanywa kupitia vikao vya siri tena huko majumbani mwao na sio kutaja kwa kujiachia hadharani, huko ni kutaka tu kiwaaminisha watu kuwa kuna mazungumzo kati yao.

6. Kinachoonekana kupitia sarakasi za kisiasa ni kwamba Walengwa wanataka kudraw attention kwa watanzania ili wahamie kwenye agenda ya kile kinachojiri ndani ya chama cha mapinduzo, agenda hiyo inaweza kuwafanya wengi waachane na kile kinachoendelea kwenye vyama vingine, mwisho wa siku ccm watakuja kuwa na msimamo mmoja kuingia uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na uchaguzi mkuu. Kanuni inayotumika hapa ni ile ya KABLA YA TUKIO KUNA TUKIO NA BAADA YA TUKIO KUNA TUKIO. Mpaka sasa mbinu hiyo inaonekana kuanza kufanikiwa kwasababu tayari mitandao ya kijamii imeshahamia kwenye mjadala huo. Wapinzani itabidi wasubiri mpaka upepo huo upite kwanza, hizo ndizo siasa.

7. Warioba ni waziri mkuu mstaafu, kiitifaki Kinana hawezi kumtuma Nape akaongee na Warioba kuhusu mpango wao tena kwenye simu, achilia mbali huyo Mzindakaya wanayemtaja kwenye audio. Prof Mwandosya pia sio wa level ya Nape kwenye suala kubwa kama hilo linalohitaji mtu kufunga safari kwenda kukaa kitako na kumwelewesha mtu aukubali mpango huo, sio jambo la kujadili kwenye simu kama vile wanajadili suala la Irene Uwoya kuwamwagia hela waandishi wa habari. Mbaya zaidi mazungumzo na mipango yote inaonekana inafanyika kwa njia ya simu jambo ambalo sio rahisi kufanywa na wanasiasa hao wakongwe.

8. Ukisikiliza kwa makini audio zote mbili utagundua hazina mwanzo mahususi wala haionyeshi zinaishiaje, mazungumzo yameanzia kati. Hiyo ni dalili kuwa aliyetengeneza audio hiyo au wale waliodukua audio hiyo aidha walichelewa kurekodi au hawakujua namna ya kuanza.

9. Katika audio hiyo wanasema jamaa ameanza kuchanganyikiwa wakirejea mazungumzo kati ya jamaa huyo na Rais museven, lakini swali la kujiuliza ni hili, inawezekanaje jamaa akaogopa kurudi Dar?yaani jamaa aweze kwenda huko alikokuwa, aende dodoma alafu aogope kurudi Dar kwenye makazi na ofisi zake? Hapo ni dhahiri kuwa wahusika wa audio hiyo walikosa story yenye mashiko ya kuunganishia matukio.

10. Ukisikiliza Kwenye audio ya kwanza eti Kinana anamtuma Nape akamwelekeze Msekwa jinsi ya kuwajibu waandishi wa habari iwapo ataulizwa kama ameipokea barua, hivi Nape ana uwezo wa kumwelekeza Msekwa kweli? Hivi Kinana ni wa kushindwa kuongea na Msekwa ambaye ndiye katibu wa wastaafu eti mpaka amtume Nape?!!! Je Kinana hana mawasiliano na Msekwa? Hapa watengenezaji wa audio hiyo walichemsha.

11. Kama kweli Kinana na Makamba walipata muda wa kuandika na kuisaini barua yao na kisha kumpatia Nape aipeleke kwa katibu wa wastaafu Msekwa sasa iweje tena Kinana huyohuyo aanze kutoa ufafanuzi kwa Nape kuhusu uwepo wa nembo na saini yake yeye na Makamba kwenye barua hiyo? maana inategemewa kwamba hayo yote wangeweza kumwelekeza Nape wakati anaichukua barua hiyo kuipeleka kwa msekwa.

12. Kitendo cha Kinana wa kwenye audio kurejea mambo yaliyomo kwenye barua hiyo kwa njia ya simu inaonesha kuwa Nape alikuwa hajui barua aliyopewa ina nini ndani yake, na hajui aipeleke saa ngapi kwa huyo msekwa ndio maana kwenye audio eti unasikia Nape akisema ataipeleka barua hiyo saa sita mchana ,alafu Kinana anasema aipeleke saa saba kabisa, yaani badala ya kusisitiza barua iwahi kufika yeye Kinana wa kwenye audio anaichelewesha kwa kumwambia Nape aipeleke barua saa saba, wala hakukuwa na sababu za kwanini barua ipelekwe saa saba badala ya sita, ukweli ni kwamba watu hao hawakujipanga hata namna ya kuipeleka?

13. Ukitaka kuona kwamba suala hili lina mchezo, jaribu tu kutafakari mfuatano wa matukio, alianza Musiba kutoa tamko, wazee wakatoa tamko lako, musiba akajibu, alafu baada ya kujibu imeachiwa audio na kusambazwa kwenye mitandao ikiwafichua Kinana na Nape Hahahahahaha, kwenye siasa usipokuwa makini unaweza kuchezewa akili mpaka ikajamba.

Kwa leo naomba niishie hapa, wakiendelea nitakuja na ushahidi wa simu walizotumia kurekodia na kusambaza hizo audio na majina yao.
 
Nadhani maelezo yako yana - make sense kwa 80%

Binafsi, nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa.....

Kwa sbb kwenye plan nzima, inaonesha kuwa watupia audio hii wanataka audience iamini kuwa Nape is part and parcel of the whole plan....

Lakini wakati huohuo wanashindwa ku - connect maudhui hayo kwa kusikiliza kwa makini ni kana kwamba Nape ameingia katikati na hajui plan ilianza anzaje....!!

Lakini hebu tujibu na swali hili muhimu:

Kuhusu hizo sauti, unadhani ni halisi, ni zao Kinana na Nnape?
 
The cannibalistic fiasco in the sobriquet of "Jakadala"(a strange killer STI) sorrounding Obado's territory(Chato county) is a mortification on the sex monomania among the occupants of Obadolization sphere and the domains beyond. This can lead to a
pusillanimous sexual magnetism within the troubled vicinities and even the rest of the agrestic pro- patria.Therefore,the nation should decipher this problem before it turns into a per-contra cataclysm.
 
Back
Top Bottom