Ukweli kinachoendelea Uwekaji wa Bikoni Loliondo

Jun 4, 2022
68
184
Pori Tengefu Loliondo lilianzishwa Mwaka 1951 chini ya Sheria ya Kuhifadhi Wanyama Sura 302, na kuendelea kutambuliwa na Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na.12 ya Mwaka 1974 kupitia Tangazo la Serikali Na.269 la tarehe 08/11/1974 likiwa na ukubwa wa kilometa za mraba 4,000. Baadae Eneo hilo lilivamiwa na shughuli za kibinadamu.

Kwa kuzingatia hilo na kutambua umuhimu wa shughuli za wananchi, Serikali imeamua kuligawa eneo hilo ambapo kilometa za mraba 2,500 zimeachwa kwa wananchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo Makazi, ufugaji na kilimo.

Aidha, eneo linalobaki lenye ukubwa wa kilometa za mraba 1,500 limetengwa kwa ajili ya shughuli za uhifadhi.

Kufuatia mgawanyo huo, Serikali imeamua kuweka mpaka wa vigingi ili kutenganisha maeneo hayo mawili na zoezi linaanza hivi karibuni.

Zoezi hili linatarajiwa kufanyika kwa amani na utulivu pasipo kuleta taharuki kwa wananchi hasa ikizingatiwa lengo ni kuwapatia wananchi maeneo ya kufanya shughuli zao bila bughudha. Hivyo, tunawasihi wananchi wawe watulivu na kutoa ushirikiano kwa Serikali katika kufanikisha zoezi hilo.
 
Enyi wamasai hameni Kwa hiari angalau muambulie hata posho za fidia , msifkr kuna mtu atawatetea mtakaojibakisha mtakuja ondolewa bila hata fidia
 
Serikali ikidhamiria jambo lake, hakuna wa kuizuia!
Serikali ni dubwasha Fulani, dude la ajabu, jinamizi halionekani!

Huwa nawashauri wengi, tusipende malumbano ya wazi na hilo likitu libaloitwa serikali kumbuka ndilo linalipa mshahara Hadi wa raisi!
 
Back
Top Bottom