Ukweli katika nukuu hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli katika nukuu hii

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by IKUKATITI, Oct 4, 2012.

 1. I

  IKUKATITI Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Miaka kumi iliyopita mwanahabari mmoja aliwahi kuandika hivi:
  “Kuepusha fedheha kwa nchi mskini, kwanza lazima nchi msikini zitafute njia bora za kuleta maendeleo kwa wananchi wao Kwa kutumia vema rasilimali walizonazo.
  Nchi masikini hazijiamini ziko legelege mno jambo dogo tu laweza kuonekana tusi, waite ombaomba, watataka waende mahakama ya kimataifa kutaka uwalipe fidia, hata kama wakati wakurejea toka The Hague watapita Ufaransa kidogo kuomba.
  Kushindwa kwa nchi hizi kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa watu wao ni jambo la hatari sana. Matatizo ya umasikini katika nchi hizi husababisha watu wakapata UVIKU yaani Ukosefu wa Viini vya Kufikiri.
  Akitokea kiongozi akasema anafikiri kwa niaba yao, anaweza kuwaamuru kila mmoja achimbe kaburi kisha ajizike humo nao waka mtii.
  Miaka 20 ijayo au zaidi mapinduzi hayatafanywa na wanajeshi tena, yatafanywa jeshi la vijana wasio na kazi amabao hawatakubali kuona wachache wananeemeka kila siku wakati wao wanaogelea katika dimbwi la dhiki.
  Vijana na raia wasio na kazi katika nchi masikini leo wako tayari kuingia mitaani wamalize hasira zao kupitia vurugu za maandamano, hata kama sababu inayompeleka huko ni kudai katiba mpya. Achilia mbali hata kama wengi wao wanakuwa hawajui katiba ni nini.
  Kuna uwezekano akitokea kiongozi akawashawishi kwamba kuna kazi sayari ya Mars na nchi nyingine zinapeleka vijana wao huko, basi wataandamana kudai pasi ili waende huko achilia mbali huo usafiri wa kwenda huko utapatikana wapi

  Wanajamvi nimeikumbuka sehemu ya makala kutokana na ukweli kwamba kipindi mwanahabari huyu anaandika makala hii ilikuwa ni Novemba 2002 na sasa ni miaka 10 mambo aliyoyazungumza yana tokea hata kabla ya kipindi alichotabiri angalia mifano:
  Vijana na raia wasio na kazi walivyo sababisha mapinduzi Tunisia, Libya, Misri,Harakati za wafanyakazi wa migodi S. Afrika, Migogoro ya wafanyakazi na serikali Kenya, Tanzania, DRC.
  Vurugu za raia wa Mali waliodiriki Kuingia ikulu na kumpiga mkuu wao wa Nchi, Vikundi vya harakati huko Nigeri mpaka Somalia.
  Sikiliza radio zetu akitokea mtu anazungumzia suala la Freemasons Vijana wengi huwa wanaulizia namna ya kujiunga wakiamini kuna utajiri wa haraka, na mengine mengi unaweza kuongezea.
   
Loading...