Ukweli juu ya kuoa

Ukweli juu ya kuoa

moyafricatz

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2015
Posts
2,905
Reaction score
4,928
1:Usioe kwa sababu umechoka kula kwa mama lishe >>Mke sio mpishi kama umechoka kula kwa mama lishe jifunze kupika.

2:Usioe kwa sababu umechoka kufua na kupika >>Mke sio housemaid, kama umechoka kufua ajiri mtu akufulie.

3:Usioe kwa sababu rafiki zako wote wameoa >>Mke sio mashindano maana hataishi na marafiki zako wala sio zawadi kwa wazazi wako bali wewe ndiwe utakayeishi naye.

4:Usioe kwa sababu unataka kufungua kanisa sasa unatafuta mama mchungaji

5:Usioe kwa sababu wazazi wanakulazimisha maana dada zako wote wameshaolewa.

6:Usioe kwa sababu mpenzi au mchumba amepata mimba yako.

7:Usioe kwa sababu unataka kumuonyesha msichana aliyekuacha kuwa bado upo juu.

8:Usioe kwa sababu unamhurumia msichana uliyenaye ukimuacha atachanganyikiwa.

9:Usioe kwa sababu wazazi wako wanampenda na kumkubali msichana huyo.

10:Kuliko kumuoa msichana kwa kumhurumia na si kumpenda itapelekea kuteseka moyoni maisha yenu yote ni afadhali umwambie ukweli kungali mapema

11:Kuoa ili kujionyesha kuwa ume-move on baada ya kuachwa ni kujikomoa mwenyewe.

Oa ukiwa na uhakika kuwa huyo ndiye chaguo lako pekee na upo tayari kuishi naye katika hali zote, ndio mpango wa Mungu katika maisha yako na ndiye unayempenda kwa moyo wako wote.

Unauonaje ushauri huu wewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuongezea tu...
Adjustments.JPG



sf
 
Sitakuja kufunga ndoa kanisani au mahakaman........nikiona nimemridhia nilie mpata kuwa mke wangu basi atakuwa mke wangu mpaka mwisho ila sio kwenda kwnye maharusi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom