Ukweli huu ukiuzingatia utafika mbali sana kwenye biashara yako

Lazaro Samwel

Member
Apr 27, 2019
33
26
Sijui kama utanielewa leo maana nina jambo kwaajili yako ambalo unaweza kulibeba kwa shingo upande.

Umeshawahi kujikuta katika hali ya kusema maneno mengi ya namna unavyotaka kufika mbali na biashara yako alafu kwenye kufanya vitu vya kukufikisha huko unakuwa mzito?

Unasema “Yaani mwaka huu nataka mwishoni niwe nimefungua ofisi yangu nyingine xxxxx”

Au “Nataka mpaka mwisho wa mwaka biashara yangu iwe ya mtaji wa mil 10.”

Siku zingine pia utasema “Nataka kila wiki niwe naingiza 100,000/=- 500,000/= kwenye biashara yangu.”

Baada ya hapa unakaa kwenye biashara yako ukisubiri wateja waje.

Utafunga jioni biashara yako alafu asubuhi utafungua ofisi yako,baada yahapo unaingia kwenye mitandao ya kijamii kufuatilia page za udaku na kuchati mambo ambayo hayana umuhimu wowote na marafiki ambao nao pia hawakusaidii kwa chochote kwenye shughuli zako.

Tukisema ukweli kabisaa,hapa nani wa kulaumiwa?

Je ni biashara yako,marafiki zako na hali ya uchumi au nini ndugu?

Je mwaka unapoisha na haujatimiza kitu hata kimoja unadhani tatizo ni nani hapa au nani ni wa kulaumiwa?

Sijakwambia ukasirike ndugu kwasababu unajua jibu ni NINI.

Ukweli ni kwamba wewe ni wa kulaumiwa.

Nisikilize kwa umakini.

Katika biashara yoyote maendeleo yake huwa yanakuja kwa kuweka malengo na mikakati thabiti ya kujua mbinu na njia ambazo zitakusaidia kuongeza mauzo kwenye biashara yako.

Hii inasema nini nasi?

Kama mfanyabiashara ni muhimu sana kuhakikisha elimu ya mauzo unakuwa nayo na unaitumia ipasavyo kwenye biashara yako kusudi uweze kufika mbali kwa vitendo na sio kwa maneno tuu.

Inabidi uweze kuwa na mifumo thabiti ya kuongeza SALES CHANNELS kwenye biashara yako lakini pia lazima uweze kuhakikisha unaongeza DISTRIBUTION CHANNELS kwenye baishara yako.

Utasema Coach unaongea nini mbona sikuelewi.

Nachomaanisha ni kwamba hakikisha UNAONGEZA NJIA ZA UUZAJI WA BIDHAA/HUDUMA YAKO usitegemee njia moja tuu kuuza bidhaa au huduma yako utafeli.

Kama hautumii mitandao ya kijamii au kama ulikuwa hautumii
mitandao ya kijamii jifunze namna ya kuitumia uuze bidhaa zako.

Kama unaona wateja wako pia wanapenda kufanya manunuzi kwenye website basi angalia ni kwenye website gani ili uweze kuitumia kama channel nyingine ya kuongeza mauzo ya bidhaa zako.

Pia ongeza mianya ya usambazaji wa bidhaa zako kufikia wateja wako katika maeneo mbalimbali mfano mzuri angalia Azam wanachokifanya kwa sasa,wameajiri mawakala mbalimbali wa bidhaa zao kuhakikisha wateja wanafuatwa kila pande kupata bidhaa zao.

Wewe utawafikiaje wateja wako kwa mwaka huu kuhakikisha wanapata bidhaa zako kwa urahisi?

Changamsha AKILI hapa sio mpaka nikwambie kila kitu.

Kukaa kwenye biashara na kusubiri wateja wako waje haitakusaidia kitu haswa kama ndo umeanza biashara na hauna BRAND yenye nguvu sokoni.

Kujisemesha maneno ya hamasa bila kuwa na mikakati ya kuyatimiza pia ni kazi bure.

Lazima kama mfanyabiashara uweze kuwa na utaratibu maalumu ambao utakusaidia ndani na nje ya biashara yako kuhakikisha unasogea sehemu.

Hata aina ya marafiki ambao utakuwa unatumia muda wako mwingi nao hakikisha ni watu ambao kwa namna moja ama nyingine watachangia kuzidi kusogea sehemu flani katika utimizaji wa malengo yako ya kibiashara.

Sio unakuwa na marafiki ambao kusupport biashara yako ni ngumu lakini kuchat na wewe masaa 2 au zaidi sio shughuli.

Au kuwa na marafiki ambao ku-support biashara yako ni shughuli lakini maswala ya kukukopa kwako ni kawaida tena haohao marafiki zako wanakuwa maarufu kwa kuchelewesha kurudisha hela yako.

Hawa wakimbie watakuchelewesha sana kutumiza kile unachotaka kutimiza kwenye biashara yako.

Sijui kama utakuwa unanielewa lakini maana ni mambo ambayo inawezekama umezoea kuyafanya na yanaathiri sana biashara yako.

Kitu kingine hakikisha unakuwa makini na matumizi ya fedha zako kutoka kwenye biashara yako.

Kile ambacho kinapatikana kipe jukumu la kuendeleza ujenzi na kuimarisha misingi ya biashara yako na sio misuli ya tumbo lako tuu.

Naimani umenielewa mpaka hapa.

Weka COMMENT yako hapa chini ya kitu ambacho umejifunza.

Ongea Na Coach Kupitia namba hizi +255678010334

Lazaro Samwel
Author | Sales And Marketing Expert | Professional Copywriter
#akiliyaushindi
 
Ushauri mzuri, ukiufuata bila shaka utafanikiwa katika biashara yako.
 
Nauza kiwanja mkoa wa pwani wilaya ya mafia mji wa kilindoni Chenye ukubwa wa mita 25x30 bei ni milioni mbili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom