Ukuzaji wa biashara

Ukuzaji wa biashara

Fleax_coinz

Member
Joined
Dec 12, 2013
Posts
13
Reaction score
19
Salaam!

Kama ilivyo kwa kiumbe chochote kiwe hai au kisicho hai inafikia kipindi kinahitaji new energy au mbinu mbadala kuweza kutoka pale kilipo na kusogea sehemu nyingine. Vivo hivyo kwa biashara.

Hivyo basi, Mfanyabiashara hata wa mtaji wa shilingi laki 1 unapaswa uwe na mpango wa muda mfupi na muda mrefu wa ukuzaji wa biashara yako (Business Growth strategy).

Mbinu mojawapo ya ukuzaji wa biashara ni Diversification (Hii ni mbinu ambayo unapaswa uanzishe bidhaa au uanze toa huduma mpya kwa soko jipya (wateja wapya). Kwa mfano kama unauza viatu vya mtumba Dar, unaongeza kuanza kuuza makoti ya mtumba kwa Dar na Dodoma)

Ukiacha mbinu hiyo ya diversification zipo mbinu nyingine kama Market Penetration (Hapa kama unauza viatu, unaongeza nguvu katika kuuza viatu na kwa wateja walewale kama viatu vya kike kwa wanawake, Hii mara nyingi ni njia ambayo hutumika kuingia katika soko.

Njia nyingine ni Market development (Hapa ni kuendelea na bidhaa ile ile ila unabadilisha focus ya soko kama ni kijiographia au aina ya wateja. Kama ulikuwa unafocus na Mkoa mmoja unaweza panua mkoa mwingine.

Njia nyingine ni product development (Kuingiza bidhaa mpya katika soko lako lile lile). Kama ulikuwa unatengeneza unga wa lishe, unaanza tengeneza na siagi).

Hizi njia ni hatua ya ukuaji ambao kila biashara inabidi ipitie kwa wakati fulani kama inataka kusonga mbele, ingawa sio mbinu za kuzikurupukia kwa kuwa ni lazima bidhaa iliyopo sokoni iweze kuwa stable ili uongeze bidhaa nyingine au ni lazima soko uwe umelikamata kwa wewe kwenda katika soko lingine la sivyo unaweza ukajikuta umebadilisha bidhaa au huduma badala ya kutanua wigo.

Lengo kubwa la Diversification ni kukuza faida yako. Katika mbinu zote za ukuzaji wa biashara Diversification ndio njia yenye hatari (risk) zaidi. Lakini risk tunazozungumzia hapa ni Systematic risk mfano market risk nk. Kwa kuwa sifa mojawapo za hizi mbinu za ukuzaji wa biashara ni kuondoa Unsystematic risk kwa mfano risk ya competition from new entrants au new products.

Utajuaje kama biashara yako inahitaji kukuzwa:

Jifunze kuipima biashara yako kwa interval za mwezi, miezi mitati na mwaka kwa kutumia vipimo kama Return on Investment (ROI) ambayo utachukua faida (Net profit-Faida baada ya kutoa gharama zote) uliyoipata tokea biashara ianze na kugawanya kwa Mtaji uliouweka halafu zidisha kwa 100%.

ROI ya 15% hadi 30% ni nzuri kwa biashara yako na unaweza kufikiria kuikuza zaidi ROI ya less than 10% itabidi ukiassess zaidi kwa kufanya Trend Analysis ya faida yako uangalia kwa kila mwezi unaoendelea kifanya biashara Net profit inaongezeka au inapungua au ipo stagnant?

Kikubwa katika biashara yoyote, unapaswa uifanyie hata roughly risk assessment, ubrainstorm kujua primary risks gani zinaweza kutokea na zikitokea utaziondoa au kuzipunguza vipi zisiathiri sana biashara yako. Kwa kuwa muda mwingi ni rahisi kudeal na residual risk than a primary ones.

Sasa Diversification na yenyewe imegawanyika pia kuna less risk (Horizontal) to medium (concentric) to more riskier (Conglomerate and Vertical - This is my favourite ).

Itaendelea...
 
Back
Top Bottom