Ukuu wa mkoa na hapo hapo ni mbunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukuu wa mkoa na hapo hapo ni mbunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkombozi, Aug 26, 2009.

 1. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2009
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Wakuu nilikua najiuliza inakuwaje unakuta mtu ni Mbunge halafu hapo hapo ni mkuu wa Mkoa? Je kati ya watu million 40 hamna mtu mwenye uwezo wa kushika cheo komojawapo? Je inakuaje kuhusu haya

  •Je analipwa mara ngapi? Anachukua mshahara wa kibunge na hapo hapo wa ukuu wa mkoa?

  •Je anatenganisha vipi kazi za kibunge na za ukuu wa mkoa?

  •Kama bunge linapitisha maamuzi yanayohusu mkoa wake atasimama upande gani? Conflict of Interest hapo.

  •Je akisafiri kutoka jimboni au mkoani kwenda mkoani au jimboni anatumia rasilimali zipi? Anawezaje kutofautisha?

  •Je kazi za kibunge na za kimkoa anazifanyaje?

  •Je wakati wa kipindi cha bunge na anatakiwa pia afanye kazi za ukuu wa mkoa, je anazigawaje?

  •PCCB wana msimamo gani kuhusu ajira mbili?

  •Je Employment and Labour Act inasemaje kuhusu ajira mbili kwa wakati mmoka?

  •Je anawaongozaje wananchi wanaotoka jimboni kwake wanaoishi mkoani kwake?

  •Je anawaongozaje wanaotoka mkoani kwake wanaoishi jimboni mwake?

  Naomba tuchangine mjadala kwa nguvu za hoja
   
 2. Magpie

  Magpie Member

  #2
  Aug 26, 2009
  Joined: Aug 26, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mimi hata jamani hata la uwaziri na ubunge hapo hapo linanikera na kunichefua...its high time now to have a clear separation of power....
   
 3. H

  Heri JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2009
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 242
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Utendaji kazi wa Mkuu wa Mkoa ambaye ni mbunge unakuwa mbaya na pia huongeza expenses kwa umma.
  Mkuu wa Mkoa inabidi kuhudhuria vikao vya bunge kama sikosei ni mara nne kwa mwaka. Inampasa vilevile kutembelea jimbo lake la uchaguzi. Hivyo basi mkoa una umia kwa sababu kusimamia na kufuatilia matatizo/maendeleo una kuwa haupo.
  Hapohapo anatumia gari na dreva wa serikali akienda kwenye vikao vya bunge na jimboni.
  Wakati umefika kuwepo kwa sheria (iliyopitishwa na bunge) kudefine nani anaweza kuwa appointed na idadi ya wilaya , mikoa na wizara .
  Position nyingine nyeti , appointees wawe vetted na bunge.
   
Loading...