Ukuta wa mawe waanguka Msuka Bandarini

Ukuta wa mawe waanguka Msuka Bandarini

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,175
Reaction score
64,552




UKUTA wa Mawe ambao umeangua chini, kufuatia nguvu za maji zinazosababishwa na athari za mabadiliko ya Tabia nchi, ukuta huo ulijengwa na wananchi wa Msuka bandarini, kwa lengo la kuzuwia maji ya bahari kumega eneo la bandari ya msuka, mabadiliko hayo yamemega eneo lenye urefu wa mita 500 la bandari ya msuka.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed, akiangalia athaari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi, katika eneo la msuka bandarini, katika ziara yake Kisiwani Pemba hivi karibuni eneo hilo ambalo ukuta umeangushwa chini na maji ya bahari.


UKUTA wa Mawe ambao umeangua chini, kufuatia nguvu za maji zinazosababishwa na athari za mabadiliko ya Tabia nchi, ukuta huo ulijengwa na wananchi wa Msuka bandarini, kwa lengo la kuzuwia maji ya bahari kumega eneo la bandari ya msuka, mabadiliko hayo yamemega eneo lenye urefu wa mita 500 la bandari ya msuka. (PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 
Ni suala la muda tu visiwa vya Pemba na Unguja vitazama kabisa baharini. Sasa ni wakati wa wapemba na waunguja kuomba muundo mpya wa muungano ili visiwa hivi vipoteze utaifa wao kama ilivyokuwa kwa tanganyika na viwe Mkoa kama mikoa mingine ya bara Mfano Dar es salaam; mwanza au Rukwa. Wakazi wa huko unguja na Pemba Mtakapokuwa kama wakazi wa mikoa ya unguja na Pemba itakuwa rahisi sana kwenu kuhamia wote bara bila kikwazo chochote pindi bahari ikianza kuwameza, itakuwa kama vile mchaga anavyotoka moshi na kwenda kuishi mwanza na kuendelea na maisha bila bugudha ya pasport, kibali au maombi ya kuhamia. Leo hii wapemba na waunguja wazo langu mtalidharau lakini nawahakikishieni kadri mabadiliko ya tabia nchi yanavyoendelea visiwa hivi vitazama na bila mabadiliko ya muundo wa muungano basi kama sio kizazi hiki cha wapemba na waunguja basi vizazi vyao vijavyo vitapata tabu sana!!! Labda kama mtaamua kuishi baharini!![emoji15]
 
Back
Top Bottom