Ukusanyaji wa kodi za majengo : TRA iunde mfumo wa kukata kodi kutoka katika mishahara ya watumish

Binti Msichana

Senior Member
Oct 9, 2016
109
247
Ili kurahisisha ukusanyaji wa kodi ya majengo katika halmashauri nchini, TRA ingeweka mfumo wa kutambua wamiliki wa majengo walioajiriwa ili mishahara yao ikatwe kodi hiyo ya majengo kupitia waajiri wao.

Wamiliki wengi wa majengo nchini ni wafanyakazi hivyo kukata kodi ya majengo kupitia mishahara yao kutarahisisha ukusanyaji wa kodi hii kwa urahisi.

Makusanyo ya kodi hii si ya kuridhisha nchini kwani wamiliki wengi wa nyumba wamekuwa wakaidi kulipa kodi hii.

Hivyo nashauri TRA ipeleke mapendekezo bungeni ili sheria ya kodi ya majengo irekebishwe na makato yapitie kwenye mishahara ya wafanyakazi wenye majengo kote nchini.

Mambo mengi ya maendeleo yamekwama katika halmashauri kwa ukosefu wa makato hivyo ukusanyaji wa kodi hii utaboresha maisha ya wananchi nchini.
 
Vipi kwa ambao hawajaajiriwa, vipi kwa vibarua na waliojiajiri. Zaidi ya nusu ya watanzania siyo waajiriwa na wanamiliki nyumba/ ardhi. Watu wa serikalini wanashida sana wao wanadhani watu wote wameajiriwa na wanauhakika wa kupokea kila mwisho wa mwezi kama wao
 
tenaaaa??????15% tuu imefanya maisha ya watu yaende mrama wewe unataka tuongeze na hiyo utaua watu aseee
 
We Binti Usichana Wako Utumie Vizuri Acha Mambo Ya Kuchongea Watumishi Unataka Tuwe Tunapokea Elfu 10 Mbona Tunalipia Kodi Hicho Unachonunua Dukani Hutuonei Huruma.
 
Back
Top Bottom