mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,580
- 9,821
Leo nimejaribu kupita katika vichochoro vingi vya jiji la DSM. Lengo langu likiwa haswa ni kujaribu kujenga shahuku juu ya kupata taswira halisi ya uwepo wa wingi wa biashara ambazo ndogo na tena si rasmi. Nikiwa na maana ya kwamba hazitambuliwi na mamlaka husika za Kodi.
Jicho la langu limeshuhudia wingi wa pilikapilika za wachuuzi na wanunuzi. Misongamano ikiwa ni mingi, yenye changamoto ktk kuzifikia na hata ubora wa bidhaa nyingi ukiwa ni duni mno, na tena bei za bidhaa zikiwa ni za chini mno.
Jicho langu la udadisi lilizidi kunikita zaidi ndani uwezekano wa wahusika kujumuishwa ktk "common tax net" kama vile mbavyo inaaininishwa ktk makabrasha ya TRA. Kusema ukweli, licha ya udogo wa mitaji na uduni wa biashara hizi, lkn nimeweza kuona kuwa kuna "potential taxable income" kama itakuwa ni kuwafikia "in their aggregate".
Natambua ilivyokuwa ngumu kwa afisa nadhifu wa TRA kuja huku Uswazi kukusanya kwa kufukuzana na wadau wao wa kodi, tena kwa mmoja mmoja wao. "Cost of collection" itakuwa ni kubwa sana "per individual taxpayer".
Natambua ili kufanikisha kukusanya kodi iliyojifisha, inapaswa kuwepo "alternative approach" ya kuweza kufanikisha hilo. Ni "approach" kama vile ifanyikavyo ktk "market segmentation" ndivyo ambavyo tunaweza kuwaweka wafanyabiashara hawa katika makundi mbalimbali ya kikodi, tena yakiwa na ukadiriaji mdogo wa kodi kuendana vipato na mitaji yao.
TRA inaweza kutetengeza "collection centres" tena kupitia vyama vya wafanyabiashara hawa. Vile kama ambavyo taasisi za mikopo midogo midogo wafanyavyo ktk VICOBA ama SACCOS. "Similar rules of the gamep" inaweza pia kutumika. "An autonomous department, solely dedicated" kwa wadau hawa muhimu wa kodi wanaweza kuwatenga ktk makundi tofauti ya kikodi "different tax baskets"
Wauzaji wa mboga mboga kundi lao, hali kadhalika mama ntilie wa sehemu husika, mathalani Mbagala ama Gongolamboto, wanawekwa kundi moja. Wachoma mahindi, mafundi wa viatu wachuuzi pweza na ugwadu wote wanawekwa katika makundi husika, ambapo utaratibu utawekwa wa kuweza kuwa kadiria zao na kukusanywa kupitia ktk vikundi vyao vya kikodi vinavyohusika.
Nimejaribu kukadiria, eneo la Mbagala peke yake zinaweza kupatikana "tax buskets" kama 100 na kila "busket" ina "taxpayer" kama 10 hivi. Piga hesabu hata kama wakikadiriwa kodi ya shilingi 2,000/- kwa wiki, achilia mbalimbali uhalisia wake wote. Utapata hesabu ya haraka ambapo zingeweza kukabidhiwa kwa halmashauri husika kwa maendeleo yake.
Ulipaji wa kodi upo kisheria, haijalishi urasmi ama udogo wa biashara. Kila mtu mwenye kujiingizia kipato halali (mimi nashauri hapa hata kisichokuwa halali lkn tu iwe "ncome" imekuwa "justified and realized") kuguswa na wajibu huu.