Consigliere
Platinum Member
- Sep 9, 2010
- 12,822
- 27,126
Mwenye nchi1: Haya mambo ya nipe nikupe yanatughalimu sana, ona watu wanavyorundikana kwetu, huku wengine wakianza kudai haki sawa, na sisi tupo tukiwaangalia tu. Hata watu wetu sasa hivi wameanza kuwa kama mazobazoba fulani hivi. Wamewaacha kabisa jamaa wabadirisha hadi misingi na tamaduni zetu.
Mwenye Nchi2: Sasa unadhani tutafanya nini kuikabili hali hii, maana katika mazingira ya sasa ni ngumu sana kuwagusa bila kujenga hisia za ubaguzi.
Mwenye Nchi1: Tunahitaji kufanya kitu haraka sana, na ili tufanikiwe tunahitaji mtu ambaye itakua raihisi kuonekana anajifanyia mambo kivyake bila ya kushirikiane na wengine. Mtu ambaye itakua rahisi kumtwisha zigo lote lawama, mtu ambaye si wa kulalamikalalamika.
Mwenye Nchi2: Bado sijakupata hapo, una maanisha nini? Kwa nini tufikie kuhitaji mtu wa aina hiyo?
Mwenye Nchi1: Hapo ndiyo nilikua nakuja. Ni hivi, mtu huyo awe mwenye misimamo mikali, lengo lionekene hizo ni sera zake sababu ya akili zake mbovu. Mtu huyo ni lazima awe maarufu na mwenye nguvu. Lengo kuonekana zigo ni lake mwenyewe. ni ili wananchi wetu waendelee kukubarika huko kwao na kufanya shughuli zao bila ya kubughudhiwa. Hapo hata tukiwafanya nini huku, itaonekana ni huyo jamaa amejikurupukia mwenyewe.
Mwenye Nchi2: Sasa nimekupata vizuri sana mkubwa. Hilo ni bonge la mkakati. Hofu yangu ilikua usalama na kukubarika kwa watu wetu kwenye hizo nchi zao. Ila kwa mkakati huu tutakuwa tumefanikiwa kula na kipofu bila kumgusa mkono. Sasa unadhani ni yupi atatufaa kati ya hawa wote tulio nao?
Mwenye Nchi1: Yule mwenye nywele kama za dhahabu nadhani atakua ni mwafaka kwa hili.
Mwenye Nchi2: Mmhhhh!
Mwenye Nchi1: Vipi mbona unaguna?
Mwenye Nchi2: Yule bwana sidhani kama atatufaa wala sidhani kama atakubali, maana yule Bwana ni mfanyabiashara mkubwa sana, na akishiriki kutoa kauli yoyote kati ya hizi itakua ni kumdondosha kutoka pale alipo na kumfilisi kabisa. Baada ataonekana ni mbaguzi, mbabe hafai n.k. Hapo itakua mwanzo wa kuanguka kwa biashara zake.
Mwenye Nchi1: Kumbe wewe bado hujajifunza namna tunavyoendesha mambo haya. Ni hivi, huyo bwana biashara zake zitaimarika mara tatu zaidi ya sasa. Ukweli ni kwamba. Huyo jamaa tulishaongea naye na alikubali kushiriki katika mkakati huu. Pia asilimia kubwa ya nchi za walaya na watu wenye nguvu ushawishi nchini mwetu wataungana ili kumpinga, yote hayo ni kwa usalama wa watu wa asili yetu popote waendapo. Ingawa huyu mama na wampao kampani wapo serious kuitaka hii nafasi, sisi tutakachohakikisha tunapambana na kuwadhibiti ili wasituharibie mipango yetu. Wao wamejipanga sana kwenye media na kampuni za kura za maoni, lakini sisi tayari tuna mbinu mbadala ambayo sitakuambia kwa sasa kutokana na uchanga wako katika kikosi hiki cha mikakati. Huyu Bwana atapingwa sana, kitakachofuata ni kuyumbisha takwimu ili kuonyesha hali ya uchumi hapa nchini si shwari.
Mwenye Nchi2: Mmh..makubwa haya...halafu!?
Mwenye Nchi1: Baadaya ya kuyumbisha takwimu hizo, hali iyo itaenda na ku impact nchi karibu zote za Walaya. Hapo nchi hizo zitakuwa zimeshapata sababu ya kuacha kupokea wakimbizi na kutengeneza roadmap ya kurudisha wakimbizi makwao, pia kuomba nchi kadhaa za Bara la Giza kukubali kuwapokea wakimbizi hao. Hapo tutakuwa tumedhibiti mfumuko wa wakimbizi kuingia huku kwetu na kwa Walaya. Na lawama na vilio havitakua vikubwa kwa kuwa itaonekana kuwa kila nchi sasa inapambana kurekebisha hali ya uchumi wake. Na kama ujuavyo, tuna wasiwasi sana kuwa wimbi hili la wakimbizi linakuwa cheered na magaidi ili waweze kuingia kwenye ya Walaya na baadaye hapa kwetu kwa lengo la kuanza mashambulizi ndani ya nchi zetu. Hivyo sambamba na kurekebisha uchumi pia tutakua tunadhibiti kirahisi siala hili la wakimbizi, maana lina sura halisi ya kigaidi, unaweza ukaliita kuwa ni blanket la ugaidi.
Mwenye Nchi2: Bado haujaniambia kuhusu biashara ya za huyo bwana zitakuaje salama.
Mwenye Nchi1: Biashara za huyo bwana zitakua salama sana na zaidi zitaimarika kwa kuwa yeye ndiye amekubali kuwa shujaa wetu. Halafu ushahidi unaonyesha kuwa watu wa asili yetu ndiyo wateja wakubwa kwa asilimia zaidi 90 kwenye hizo biashara zake. Ni mtu ambaye tutamtukana na kumshambulia hadharani ila sirini kila mmoja wetu atambue ana jukumu na deni kubwa mbele yake. Ni mtu muhimu sana kuliko umuhimu wenyewe.
Mwenye Nchi2: Daah...kudadadeki, kweli kazi ipo na duniani kuna vichwa. Ina maana kwenye uchaguzi wa safari hii watu wanakwenda kulishwa matango pori!!
Mwenye Nchi1: Hakika, na kwa kuanzia utayaona matokeo. Ila usisahau kwamba 'The wakina mama" (The Mamaz) and the company yupo serious sana, hawapo tayari kupoteza na kitu kizuri tumefanikiwa kuwapandikizia watu katika timu yao ya kampeni na watu hao watahakikisha wanayalaza usingi majimbo ambayo ni ngome zao.
Nadhani nimeshakueleza vya kutosha sasa. Nenda ukampumzike tayari kwa majukumu utakayokabidhiwa...ila ukumbuke kuwa yote hii ni namna nzuri ya kula na Kipofu, pamoja na mambo mengine mengi ikiwemo kuondoa kabisa utawala wa mazoea na yale magenge/familia, tunahitaji kubadili mwelekeo wetu kama taifa na jamii pia kusimama katika misingi ya asili maana huku tuendako sasa siiyo kabisa.