Ukubwa dawa

UrbanGentleman

JF-Expert Member
Jun 19, 2016
2,585
1,885
Mpaka Leo nimeshindwa Kuelewa Kwanini vijana wengi wa sikuhizi wanaishi maisha ya kutafuta attention ata katika mambo ambayo kimsingi hayaitaji sifa wala mijadala ya kubuguzi wengine mfano unakuta kijana anakuja na wazo la maisha ya ndani hasa chumbani kwake juu ya ambavyo mke wake Hajui kupika au mke wake ni gogo kitandan au mke wake mchafu sasa mbna tunajidharaulisha wenyewe wakati maisha tulichaguwa wenyewe,mwengine anajisifia kua na mchepuko na kuweka bandiko mkewe mchovu sasa mpaka kufikia umri huo bado unashindwa kuelewa kwanini hauwezi kwenda na mkeo askari monument kutembeza dushe kwa mkeo?? Duuh poleni ila badilikeni
 
Naona mipasho kutoka kwa wanaume na wanawake kila siku hapa jf. Mke anamsema Mme na Mme anamsema Mke.
 
Kutokana na hali ya utandawazi ulioweka wazi kila kitu hata kile ambacho hakikutakiwa kuwa wazi....matokeo yake vijana wanajikuta wamejiingiza kwenye mambo ambayo ukubwa wake yanaizidi akili yake ambayo ni changa.....
Hususani katika masuala ya mahusiano...haya ni moja ya masuala ambayo vijana hujikuta tu wamejitumbukiza huko kwa matakwa ya matamanio yao na wala sio kwa utashi wao.....na ndio maana humu haziishi nyuzi za malalamiko kuhusiana na hayo mambo.....
yao ya kingono....
Kimsingi ni kwamba vijana ni kama wameacha kabisa matumizi ya akili zao na wameamua kuenenda kama wendawazimu....kwa kuendekeza matakwa ya nafsi zao......

Na kibaya zaidi hawashauriki....kila utakalowaambia litakalopingana na matakwa yao....utapewa tusi ambalo pengine tangu kuzaliwa hujawahi kulisikia na kuitwa mmbeya kwa kufuatilia maisha ya watu......mambo yakiwa magumu huko chumbani kwao....anakuja tena huku huku kwa wambea na wanaomfuatilia maisha yake kuja kuomba ushauri.....hapo tena amekuwa mdogo kiasi kwamba unaweza hata kumpitisha kwenye tundu ya sindano..........na sisi kwa kuwa tunajua kulea vijana...tunajitahidi kuwashauri kwa kadri ya uwezo wetu......kwani kuishi kwingi ndio kuona mengi.....

Ujana ni maji ya moto......
Maisha ya ujana ni nusu ya uwendawazimu.....

Ukipiga picha vituko unavyovifanya kwenye ujana wako unaweza usiamini kuwa ni wewe uliyekuwa ukiyafanya hayo pindi uitwapo babu....
 
Ni kweli mkuu, tena nyuzi nyingi ni zile ambazo kwa namna flan zinahalalisha uchepukaji na zingine ni mambo ya tigo tigo tu.

Yaani unakuta mtu analalamika kuudhiwa na mchepuko au anaomba ushauri namna ya kulala na mchepuko bila kujulikana sio hata mke.

Mh...maisha haya.
 
Kutokana na hali ya utandawazi ulioweka wazi kila kitu hata kile ambacho hakikutakiwa kuwa wazi....matokeo yake vijana wanajikuta wamejiingiza kwenye mambo ambayo ukubwa wake yanaizidi akili yake ambayo ni changa.....
Hususani katika masuala ya mahusiano...haya ni moja ya masuala ambayo vijana hujikuta tu wamejitumbukiza huko kwa matakwa ya matamanio yao na wala sio kwa utashi wao.....na ndio maana humu haziishi nyuzi za malalamiko kuhusiana na hayo mambo.....
yao ya kingono....
Kimsingi ni kwamba vijana ni kama wameacha kabisa matumizi ya akili zao na wameamua kuenenda kama wendawazimu....kwa kuendekeza matakwa ya nafsi zao......

Na kibaya zaidi hawashauriki....kila utakalowaambia litakalopingana na matakwa yao....utapewa tusi ambalo pengine tangu kuzaliwa hujawahi kulisikia na kuitwa mmbeya kwa kufuatilia maisha ya watu......mambo yakiwa magumu huko chumbani kwao....anakuja tena huku huku kwa wambea na wanaomfuatilia maisha yake kuja kuomba ushauri.....hapo tena amekuwa mdogo kiasi kwamba unaweza hata kumpitisha kwenye tundu ya sindano..........na sisi kwa kuwa tunajua kulea vijana...tunajitahidi kuwashauri kwa kadri ya uwezo wetu......kwani kuishi kwingi ndio kuona mengi.....

Ujana ni maji ya moto......
Maisha ya ujana ni nusu ya uwendawazimu.....

Ukipiga picha vituko unavyovifanya kwenye ujana wako unaweza usiamini kuwa ni wewe uliyekuwa ukiyafanya hayo pindi uitwapo babu....
utakuwa mchambuz wa maswala haya bla shaka!!!
 
Back
Top Bottom