😀😀😀😀😀😀
Watu 80 wauawa kati ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya waislam wa madhehebu ya Shia na Sunni karibu na mpaka wa Afghanistan na Pakistan. Mapigano hayo yalianza alhamis ambapo wanamghambo waislamu Sunni wenye silaha za moto walipovamia msafara wa waislam wa madhehebu ya Shia ambao...
www.jamiiforums.com
Hao watu wana hesabu zao mbele ya mungu kama utayokuwa nayo wewe na mimi .
Wokovu
Wakristo mnasema kwamba “MUNGU AMEMTOA” mwanawe wa pekee ili kutuokoa sisi”. Je, Mungu alimtoa Yesu kumpa nani wakati yeye Mungu ndiye mmiliki wa ulimwengu wote?
Ikiwa ilikubalika kwa utukufu wa Mungu kuwa awe na watoto, basi angeumba mamilioni ya watoto kama Yesu. Sasa kuna jambo gani kubwa kumhusu huyu mtoto wa pekee?
Kwa nini Biblia inasema kwamba Yesu alitaka kufa msalabani, huku yule mtu aliyesulubiwa pale msalabani alikuwa anapiga kelele “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” kwa mujibu wa Matayo 27:45 na Marko 15:33?
Ikiwa Mungu alitaka kutuokoa, Je, angeshindwa kutuokoa bila kumtoa muhanga Yesu?
Mungu yeye mwenyewe ni haki, na haki inataka kusiwepo na mtu anayepaswa kuadhibiwa kwa madhambi ya wengine, vile vile haipaswi kuadhibiwa watu wengine kwa kuwaokoa wengine: Je! Dai la kwamba Mungu amemtoa muhanga Yesu ili kutuokoa haliteti mkanganyiko kama kweli Mungu ni mpenda haki? Je, Dai hilo halitofautiani na maana halisi ya haki?
Watu wanatoa muhanga vitu vyao ili kupata vitu vingine wasivyokuwa navyo ikiwa haiwezekani kuwa navyo vyote viwili kwa wakati mmoja. Wakristo wanasema kwamba “Mungu alimtoa muhanga mtoto wake wa pekee ili kutuokoa; Tunajua kwamba Mungu ni Mwenye nguvu; Mungu alimtoa Muhanga Yesu kwa nani?
Kutoa muhanga kitu maana yake ni kwamba huwezi kukipata tena kile ulichokitoa; sasa kuna siri gani katika kutolewa Muhanga Yesu wakati Mungu aliweza kumrudisha Yesu baada ya kusulubiwa (kwa mujibu wa maneno ya Wakristo)?
Ikiwa Wakristo nyote mumeokoka kwa kupitia Yesu na mnakwenda Peponi (kwenye uzima wa milele) bila kujali matendo yenu, kwa hiyo mafundisho ya Yesu hayana umuhimu wowote na maana ya maneno “uovu” au “wema” hayana umuhimu wowote. Ikiwa hali sivyo hivyo, kwa hiyo wale Wakristo ambao wanamwamini Yesu lakini hawafuati mafundisho yake wala hawajatubu watakwenda motoni?
Vipi Wakristo mnayachukulia matendo kama kitu kisicho na umuhimu baada ya kuwa kitu kimoja wakati Yesu aliposema katika Matayo 12:36; “Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.”?
Wakristo mnasema kwamba watu wanakwenda Peponi kwa kupitia Yesu tu! Wakati Paulo anasema katika 1 Wakorintho 7:8-16 kwamba Mume asieamini anakubalika kwa Mungu kwa sababu anaunganishwa na mke wake na kinyume chake, na watoto wao wasio na dini vile vile wanakubalika kwa Mungu. Kwa hivyo kumbe watu wanaweza kwenda Peponi bila ya kumwamini Yesu; kutokana na maneno hayo.
Vipi Biblia inasema kwamba Waisraeli wote wameokoka ingawa hawamwamini Yesu? Je, Hili halipingani na dai la Biblia ya kuwa njia ya pekee ya kwenda Peponi ni kwa kupitia Yesu tu?
Kwa mujibu wa Wakristo, wale wote ambao hawakubatizwa watakwenda motoni. Kwa hivyo hata watoto wachanga nao watakwenda motoni kwa vile walikufa kabla ya kubatizwa; kwa vile walizaliwa na dhambi la asili la kurithi? Je, hili halipingani na maana ya neno haki; kwanini Mungu awaadhibu watu kwa madhambi wasiyoyatenda?