Ukraine,Poland na Lithuania zaunda jeshi

Ukraine,Poland na Lithuania zaunda jeshi

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,945
Reaction score
63,725
120306154453_ukraine_soldiers_parad_army_304x171_unian.jpg

Wanajeshi katika gwaride

Ukraine ,Poland na Lithuania zimekubaliana kuunda jeshi la pamoja litakaloshirikisha maelfu ya wanajeshi.


Akizungumza baada ya mataifa hayo matatu kutia sahihi makubaliano hayo mjini Warsaw,rais wa Poland Bronislaw Komorowski amesema kuwa jeshi hilo linatarajiwa kufanya zoezi lake la kwanza la kijeshi mwaka huu na kwamba litashirikisha oparesheni za kulinda amani.

Kitengo hicho cha jeshi kitakuwa na makao yake makuu katika mji wa mashariki mwa Poland Lublin,ikiwa ni kilomita chache kutoka mpaka wa Ukraine.

Mpango wa Jeshi la pamoja ulianzishwa mnamo mwaka 2007 ,na sasa unaonekana kupigwa jeki na wasiwasi uliozushwa na jeshi la Urusi katika eneo hilo.

Chanzo:BBC
 
wacha wajikoki tu..usifanye mchezo kabisa na hiki kitabia cha kuyeyusha ndege kama ice cube kwenye glasi ya vodka..
 
Back
Top Bottom