Mkyamise
JF-Expert Member
- Apr 14, 2014
- 473
- 607
Hali hii inatishia afya za wagonjwa wanaofika katika hospitali hii. Matarajio ya wengi ni kwamba hospitali ni sehemu ambayo mgojwa hupata huduma za afya. Jambo hili katika hospitali hii ni kinyume kabisa. Kuna vyoo vipo karibu na canteen ya hospitali, hali ni mbaya. watu wanaweka *mizigo* tu halafu choo chenyewe kinahitaji maji. Maji yenyewe hakuna. Vyoo vingine vipo karibu na wodi za wanaume. Vyoo hivi vimejaa sana. Uongozi wa hospitali hii mnasubiri nini kitokee ndiyo mchukue hatua? Hata kama ni ukosefu wa maji je mlitegemea wagonjwa na watu wengine wanaofika hapo hospitali kutumia vyoo vipi? Hatukatai maji yanaweza kuwa ni ya shida lakini kamwe si kwenye vyoo vinavyohudumia wagonjwa na watu wengine na particularly hospitali. Chonde chonde, chukueni hatua.