Ukondoo wa Watanzania Unawafanya Watawala Kufanya Uchafu Wowote Wanaoutaka

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,555
41,064
Kwa namna Tanzania ilivyo na jinsi Watanzania tulivyo, lazima uwe na akili ndogo sana au uwe huna kabisa, ndiyo unaweza kuamini kuwa nchi hii kuna siku itakuja kuendelea kwa kutegemea jinsi tunavyoenda.

Karibia wakati wote, kwa kiasi fulani ukiondoa kipindi cha awamu ya kwanza, wakati mwingine wote, Watanzania wamekuwa katika laana ya kuongozwa na watu majizi, wazembe wasio na huruma kwa wananchi na Taifa kwa ujumla. Ofisi nyingi za umma zimejaa majizi, wafuja pesa, wazembe na uwezo duni wa kiutendaji.

Kila mwaka report ya CAG inakuja na madudu yale yale, wakati wote ni mabilioni na matrilioni yaliyopotea. Safari hii mpaka mamia ya magari yaliyonunuliwa hayaeleweki yameenda wapi.

Ndiyo maana haya majitu hata wakati wa uchaguzi yapo tayari kuiba kura, kuhonga, kupora ushindi wa waliochaguliwa na wananchi ili wapate nafasi ya kwenda kukomba mabilioni wa Watanzania makondoo na wajinga.

Hakuna mtu anayeweza kuiba kura na kuhonga wapiga kura kwa sababu ana uchungu wa kutaka kwenda kuwahudumia wananchi. Wanaiba kura, wanapora ushindi, wengine wanaenda mpaka kuwanga, ili tu wapate mwanya utakaowapeleka kwenda kuiba pesa ya umma.

Uchafu unaotendwa na watendaji wa Serikali kila mwaka, ingekuwa ni nchi ya watu wenye akili timamu wanaojitambua, hakika lazima kuna kitu kingetendeka dhidi ya Serikali.

Ndugu zangu, hata ukianzisha mradi wowote, mafanikio huwa yanategemea zaidi maeneo mawili:

Moja, ni uzalishaji. Hii ndiyo itakayoamua mapato (revenue) utakayoyapa.

Sehemu ya pili ni matumizi.

Mradi wako unaweza kufanikiwa kwa kuhakikisha unaongeza uzalishaji, matumizi yakabakia constant. Au unaweza kubakiza uzalishaji ule ule lakini ukapunguza matumizi.

Ukitaka kufanikiwa zaidi, unaweza kuongeza uzalishaji na pia ukapunguza matumizi wakati mmoja.

Ukweli ni kwamɓa hata ukizalisha kiasi gani, na mapato yakaongezeka, lakini matumizi yakawa nayo yanapaa, mradi wako hauwezi kufanikiwa, na wewe utabakia maskini daima.

Kwa Tanzania, hatuwezi kupata mafanikio yoyote kwa sababu wakati tunahangaika kuongeza mapato, tena kwa kuwakamua hasa wananchi maskini, haya majizi yaliyomo kwenye ofisi za Serikali, yenyewe yanajitahidi kuongeza kufuja na kuiba pesa za umma maradufu.

Lakini haya yote yanatokea kwa sababu ya ujinga wa sisi wananchi. Yanaiba kura, sisi tupo kimya, yanaiba pesa, tupo kimya. Kwa nini yasiongeze kuiba!!

Hivi kama tumeshindwa japo kuandamana kudai tuoneshwe kwa majina, hayo majizi ili tukayakokote kuyaondoa ofisini, kwa nini hata tusigome wote kwa pamoja kulipa kodi mpaka tutakapokuwa na uhakika kodi zetu zinatumika vizuri?

Kwa hali ya wizi, rushwa na uzembe wa watendaji wa Serikali ya Tanzania, kwa kweli si halali kabisa kulipa kodi. Wajibu hauwezi kukaa upande mmoja. Yaani mwananchi alipe kodi, lakini mkusanyaji atapanye kodi kwa anasa na wizi. Hii haikubaliki. Kama anayekusanya hana uwezo wa kuitunza hela inayokusanywa ikawa salama, basi asikusanye mpaka siku atakapokuwa na uwezo wa kuilinda na kuitumia vizuri na kwa umakini kwa manufaa ya walipa kodi.

Kama tusingekuwa na majitu majizi kwenye ofisi za Serikali na taasisi zake, ingewezekana vipi shirika kama TANESCO, lisilo na mshindani, linalopewa mpaka na ruzuku na Serikali, lingeweza kupata hasara?

Ni mradi gani wa Serikali au CCM uliwahi kufanikiwa? TBL walifeli, TANESCO wamefeli, viwanda vya bidhaa mbalimbali walifeli, SUKITA ya CCM ilifeli, Shule za wazazi za CCM zilifeli, maduka ya TRC yalifeli, ATCL wamefeli, TTCL wamefeli, kila kitu wamefeli. Hata reli watafeli tu. Kwa sababu hawa watu hakuna wanachofikiria zaidi ya kuiba

Ukweli ni kwamba kila inapowezekana kukwepa kulipa kodi ni aheri kufanya hivyo. Maana hata ukilipa, kuna majitu yanaenda kuichezea pesa yako wakati wewe umejibana, umeiacha familia yako ikijibana na kuteseka, lakini huko kuna mijitu inaenda kuichezea pesa yako kama haina mwenyewe.
 
Middle class wa kitanzania hawajitambui,push back hawana na wanaishia kulalama humu, moja ya miji ya Ulaya ina sanamu ya mwanamke, aliyejuu ya farasi na yupo uchi(naked)huu ni ukumbusho wa kweli wa push back kutoka kwa KE huyu kupinga ongezeko la kodi kwa raia, raia wengi kiuchumi hali zao zilikua hoi, pia kuna ukumbusho wa mwingine wa KE aliye risks maisha na kufanikiwa kuokoa zaidi ya watoto 25k wa ki Jewish waliokua hatarini kufa, (kosa hili angekamatwa lingekuwa punished kwa grave!)hii ni mifano miwili ya push back ya mtu mmoja mmoja ili kudai na kutetea haki za wengi, kwetu tuendelee kulalama kwenye social networks
 
Ukikaa na raia wa Mali leo hii, wanaifurahia sana serikali iliyoko madarakani. Hakuna wizi wa pesa za umma wala miradi kukwama. Ingawa si vizuri, lakini natamani hata sisi tungepata serikali ya aina hiyo. Watumishi wetu wa umma hawana wasi wasi kabisa na ripoti ya CAG maana wameizoea na wanajua hakuna kitakachowatokea.
 
,
JamiiForums-1066041085.jpg

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kwa namna Tanzania ilivyo na jinsi Watanzania tulivyo, lazima uwe na akili ndogo sana au uwe huna kabisa, ndiyo unaweza kuamini kuwa nchi hii kuna siku itakuja kuendelea kwa kutegemea jinsi tunavyoenda.

we umejibana, umeiacha familia yako ikijibana na kuteseka, lakini huko kuna mijitu inaenda kuichezea pesa yako kama haina mwenyewe.
That is correct by 💯 percent
 
Ukikaa na raia wa Mali leo hii, wanaifurahia sana serikali iliyoko madarakani. Hakuna wizi wa pesa za umma wala miradi kukwama. Ingawa si vizuri, lakini natamani hata sisi tungepata serikali ya aina hiyo. Watumishi wetu wa umma hawana wasi wasi kabisa na ripoti ya CAG maana wameizoea na wanajua hakuna kitakachowatokea.
Nimeishi Mali. Hakiks ile nchi kuna maadili ya hali ya juu. Nilishangaa kuona watu wanaacha vitu vyao kwenye magari, mengine milango haijawa locked. Simu, laptop vimeachwa ndani ya magari. Na baadhi ya magari watu wametoka, milango hawajafunga, funguo wameacha ndani ya gari. Kwenye baadhi ya hotel, watu wanaebda chooni, kuonesha kwenye hiyo meza kuna mtu, anaacha simu mezani.

Usiku mmoja, nilipoenda kwa mara ya kwanza Mali, nimefika siku hotelini nikaambiwa hawapokei dola, wanataka nibadilishe kwanza. Na ni saa 2 usiku, bank gani iliyo wazi? Wakaniambia kuwa kuna watu, ni kama machinga, pia wanabadilisha. Tukaenda mitaa ya sokoni pale Bamako. Jamaa ana bag lenye dola, na bag lenye pesa ya mali. Kakaa tu kwenye veranda, na ni saa 3 usiku, anabadilisha pesa. Hana hata mlinzi, na sijui anafunga saa ngapi. Nikafikiria kama ingekuwa Dar, huyo siku inayofuata asingeiona.
 
Middle class wa kitanzania hawajitambui,push back hawana na wanaishia kulalama humu, moja ya miji ya Ulaya ina sanamu ya mwanamke, aliyejuu ya farasi na yupo uchi(naked)huu ni ukumbusho wa kweli wa push back kutoka kwa KE huyu kupinga ongezeko la kodi kwa raia, raia wengi kiuchumi hali zao zilikua hoi, pia kuna ukumbusho wa mwingine wa KE aliye risks maisha na kufanikiwa kuokoa zaidi ya watoto 25k wa ki Jewish waliokua hatarini kufa, (kosa hili angekamatwa lingekuwa punished kwa grave!)hii ni mifano miwili ya push back ya mtu mmoja mmoja ili kudai na kutetea haki za wengi, kwetu tuendelee kulalama kwenye social networks
Kwa kwaida ni wananchi ndio wanatakiwa kui-shape Serikali. Sisi tunasubiria watendaji wa Serikali wawe malaika. Haitatokea.

Nchi yetu ni kama wananchi wake wote akili zilikwishakufa. Tunatoa pesa zetu kwa hiari ili watu wakaibe na kufanyia starehe.
 
Ukweli mchungu bado tunategemea akina Zito, Mbowe, Lissu etc etc watupiganie wakati sisi tumebaki miamba ya kulalama kwenye key boards, it's craze
 
Ukikaa na raia wa Mali leo hii, wanaifurahia sana serikali iliyoko madarakani. Hakuna wizi wa pesa za umma wala miradi kukwama. Ingawa si vizuri, lakini natamani hata sisi tungepata serikali ya aina hiyo. Watumishi wetu wa umma hawana wasi wasi kabisa na ripoti ya CAG maana wameizoea na wanajua hakuna kitakachowatokea.
Na bila shaka baada ya kuambiwa stupid, walicheka na cheeeeers ikafuata ya Meerust Rubicon!
 
Kwa namna Tanzania ilivyo na jinsi Watanzania tulivyo, lazima uwe na akili ndogo sana au uwe huna kabisa, ndiyo unaweza kuamini kuwa nchi hii kuna siku itakuja kuendelea kwa kutegemea jinsi tunavyoenda.
Tuamke watanzania nchi inatafunwa kama kitumbua!
 
Ukikaa na raia wa Mali leo hii, wanaifurahia sana serikali iliyoko madarakani. Hakuna wizi wa pesa za umma wala miradi kukwama. Ingawa si vizuri, lakini natamani hata sisi tungepata serikali ya aina hiyo. Watumishi wetu wa umma hawana wasi wasi kabisa na ripoti ya CAG maana wameizoea na wanajua hakuna kitakachowatokea.
oya angalia convo kuna ujumbe wako
 
Umemaliza kila kitu, hii nchi imejaa wajinga wengi zaidi 90% na ndio ntaji wa watawala, uliona wap report ya CAG itoke mwezi watu alafu kuijadili bungeni mpaka mwezi wa 11.. yaan unampa mwezi miezi nane ya kujipanga na raia wala hawana habari wao ni yanga na simba..
 
Ongezea na diamond wema
Alikiba zari wanafanya nini

Ova
 
Back
Top Bottom