Ukomo wa mihula ya ubunge

Ukomo wa mihula ya ubunge

Gia kubwa

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2020
Posts
470
Reaction score
495
Jana Katibu Mkuu wetu alizungumzia sana ukomo wa Urais ila akapitia kwa mbaaali kuzungumzia ukomo wa wabunge ila vijana tuliinasa nikajiuliza hivi kwanini?

1. hakuna ukomo wa ubunge na kuna video clips na picha za wabunge wazee kulala hadi kukoroma bungeni, wengine hawana maajabu wapo wapo tu bungeni hawaongei chochote tangu bunge linaanza hadi linavunjwa hawana cha kuchangia kujenga taifa zaidi ya kuleta mawazo ya kizamani tu!! kwanza wabunge wazee ni mzigo kwa walipakodi, ni watu waliochoka ambao kazi yao kubwa bungeni ni kupasha viti joto tu! ni watu wanahitajika sana kurudi kijijini kucheza na wajukuu,

2. kuna wabunge wazee wanaumwa for five years tangu bunge linaanza hadi linavunjwa ! na wanalipwa kodi za wanyonge tu , halafu kwanza wabunge hawa wazee kina Chenga, Mkono nk ni mzigo kwa kodi za walalahoi bajeti ya matibabu yao nje ya nchi ni kubwa mno wanatibiwa nje bila ulazima wowote watu wenyewe wamejiishia wanaacha Mloganzila ipo for them. Mh Rais huku bungeni kuna hela nyingi ya kuokoa kulipa vibarua wa SGR wabunge wote watibiwe nchini mbona sisi raia wanyonge tunaokupigia kura za kishindo tunatibiwa nchini na hatufi kwa corona na malaria na kuharisha?

3. kuna wabunge watoro bungeni tangu bunge linaanza hadi linavunjwa hawapo bungeni wako na mishe zingine tu za kujiongezea kipato na kule wanalipwa kodi za wanyonge wapi Dr Bashiru unajua hili? Mh Rais hapa ukipewa list na kuwakata wabunge watoro mishahara utapata pesa ya ndani kulipia vibarua wa kujenga Stieglers Gorge dam!! kupanga ni kuchagua!!

4. kuna wabunge wengi hawana sifa za kitaaluma za kuweza kufanya kazi za kibunge, wana elimu ndogo na uwezo mdogo wa kiakili hawawezi kuchambua complex issues kama ripoti ya CAG, bajeti za wizara, ripoti za kamati kama PAC nk nao kazi kubwa wanaropoka kukashifu wenzao , kupiga vijembe na kuleta mipasho tu bungeni na kupiga meza na kuibua mijadala isiyo na tija kwa nchi hii maana they cannot reason!!

5. kwanini sifa ya mbunge iwe kujua kusoma tu na kuandika wakati majukumu ya mbunge tukisimama kwenye ukweli yanahitaji Graduate? mf sheria nyingi ziko kwa kiingereza ndo zinakaa vyema na wabunge hawa vilaza kwanini sasa wawepo jumba linahitaji wasomi?? huwa najiuliza ni mjinga gani aliweka kipengele hiki? kwa mantiki gani? kwa maslahi ya nani?

6. Je mchakato gani utumike kuweka ukomo huu haraka? kwanini Rais tumuwekee kikomo halafu tukubali wabunge wasiwekewe kikomo? nilijiuliza kwanini sisi watu weusi ni watu wajinga na sera zetu nyingi za utawala zinaonesha ujinga wetu na hatukemei?

7. nilijiuliza kwanini kusiwe na ukomo wa umri wa mbunge ili kuwaengua wazee zaidi waliochoka, mfano mbunge awe na miaka 30 hadi miaka 60 na si zaidi ili kupata watu wanaowaza kujenga nchi na si kujilimbikizia mali na kusubiri kufa vifo vya ghafla vinavyotokana na moyo kushindwa kusukuma damu ya mwili wenye tumbo kubwa lililojaa mafuta ya kodi za wanyonge!!

Naomba Dr Bashiru simamia hili ukomo wa ubunge uwe ten years only and Allah will bless you! Kumbuka kila mtu ni mchunga na ataulizwa kwa alichokichunga wabunge wazee wa chama chako wanalibiia taifa nawewe ni mtendaji mkuu msaidizi!!usikubali!!

Kuna wabunge wazee wengi wameiba vya kutosha pesa ya umma kwa miaka mingi na wamejimilikisha ubunge kwenye majimbo yao kwa kutumia pesa na majina yao (influence) na hawaleti maendeleo yoyote majimboni kwao!!

Jana nilikusikiliza vizuri kwenye mdahalo wako na Tido mwanzo mwisho nikakuona ni Kondoo umevaa ngozi ya Chui, wewe Dr Bashiru ni Mzalendo wa kweli kama Mh Magufuli nanyi mmejificha ndani ya genge bovu la wasafi na wengine Manyang’au!!
 
Kwa taarifa yako huyo Bashiru baada ya kupewa madaraka ndio unafiki wake umekaa hadharani. Anajua fika kuna rasimu ya Warioba iliyokuwa na maoni ya wananchi, na wananchi walitaka kikomo cha ubunge kiwe miaka 10, lakini chama chake kulipinga maoni hayo kwa faida yao.

Hapo alipo anajua ili aweze kubaki ni kufanya unafiki wa kiwango cha juu, vinginevyo anajua atapoteza hii boom aliyoipata uzeeni.
 
Kama bunge lijalo litapendekeza urais wa milele, basi ukomo wa ubunge hauna maana, ni bora na wabunge wawe wa milele tuondokane na gharama za uchaguzi. Ukiwa na rais wa milele ukimletea wabunge wasio wa milele unaweza kujikuta unamleteawabunge wa kumpinga na hivyo akashindwa kutimiza malengo yake!
 
Kwa taarifa yako huyo Bashiru baada ya kupewa madaraka ndio unafiki wake umekaa hadharani. Anajua fika kuna rasimu ya Warioba iliyokuwa na maoni ya wananchi, na wananchi walitaka kikomo cha ubunge kiwe miaka 10, lakini chama chake kulipinga maoni hayo kwa faida yao.

Hapo alipo anajua ili aweze kubaki ni kufanya unafiki wa kiwango cha juu, vinginevyo anajua atapoteza hii boom aliyoipata uzeeni.
Nadhani mngeanza na Katiba ya CHADEMA kwanza, kipengele cha Ukomo wa Mwenyekiti kilichoondolewa kinyemela ili abakie madarakani milele kirejeshwe. Halafu sasa ndo mpate uhalali wa kujadili ukomo wa mbunge.
 
Gia kubwa,
Lakini mkuu, hao uliowataja wote hapo juu si wanachaguliwa na wananchi wenyewe, hawayajui hayo?
 
Nadhani mngeanza na Katiba ya CHADEMA kwanza, kipengele cha Ukomo wa Mwenyekiti kilichoondolewa kinyemela ili abakie madarakani milele kirejeshwe. Halafu sasa ndo mpate uhalali wa kujadili ukomo wa mbunge.

Tafuta popote mimi ninapounga mkono kiongozi yoyote yule kukaa madarakani zaidi ya miaka kumi. Na hapo ndio utajua kuwa mimi sio muumini wa Mbowe, au kiongozi yoyote yule kukaa madarakani zaidi ya miaka 10. Isitoshe mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, bali shabiki wa nguvu wa cdm, hivyo sina maamuzi yoyote, ndani ya chama chochote cha siasa.
 
Nashukuru sana. Ila unatakiwa kuionyesha wazi, wenzako wanapotetea huo upuuzi wa mbowe kukaa zaidi ya miaka 20 madarakani.

Hata hivyo, kwenye maelezo yako umesema wewe ni ushabiki wa CDM, nimeshindwa kutofautisha kati ya mtu kuwa shabiki na kuwa mwanachama wa chama fulani. Hebu tudadavulie
 
Tafuta popote mimi ninapounga mkono kiongozi yoyote yule kukaa madarakani zaidi ya miaka kumi. Na hapo ndio utajua kuwa mimi sio muumini wa Mbowe, au kiongozi yoyote yule kukaa madarakani zaidi ya miaka 10. Isitoshe mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, bali shabiki wa nguvu wa cdm, hivyo sina maamuzi yoyote, ndani ya chama chochote cha siasa.

Shida vijana hawajitambui huku wakati wao ukipita.... Vijana hao hao ndio wapambe wa hao wazee...
 
Tatizo sio ukomo wa ubunge, bali ni malipo wayapatao hao wabunge. Ilitakiwa mshahara wa mbunge uwe sawa na mwalimu. Hii kazi iwe ni wito wa kuwakilisha wananchi. Halafu tuona mrejesho wake upoje.
 
umenena vyema! uanzishwe mjadala wa kitaifa!
 
Kwa taarifa yako huyo Bashiru baada ya kupewa madaraka ndio unafiki wake umekaa hadharani. Anajua fika kuna rasimu ya Warioba iliyokuwa na maoni ya wananchi, na wananchi walitaka kikomo cha ubunge kiwe miaka 10, lakini chama chake kulipinga maoni hayo kwa faida yao.

Hapo alipo anajua ili aweze kubaki ni kufanya unafiki wa kiwango cha juu, vinginevyo anajua atapoteza hii boom aliyoipata uzeeni.
Kama wewe na Chadema wenzio ni waumini wa ukomo wa mbunge wa miaka 10 anzeni ku practice kuonyesha wazi kuwa mnaunga mkono kwa vitendo .Wabunge wote waliokaa miaka kumi waje hadharani watamke wazi kuwa sisi tunaunga mkono rasimu ya Warioba hatutagombea tena miaka kumi inatosha.Wananchi wangewashangilia sana kuwa you mean what you say.Lakini kama wabunge wenu walikaa miaka kumi watarudi tena kugombea it means upinzani hamko serious kwenye vitu mnavyoongea Na watu watawachukulia na nyie ni madomo kaya tu hamna lolote
 
Wabunge kwenye kipengele cha elimu walisema ili mradi ajue kusoma na kuandika.

Ila dreva wa Mbunge anatakiwa awe amemaliza kidato cha 4 na kuendelea, hapo utajua nani mtunga sheria.
Sheria zinatungwa na mamalaya ya kisiasa unategemea nini mkuu?. Ndiyo Upumbavu Kama huo.
 
Kama wewe na Chadema wenzio ni waumini wa ukomo wa mbunge wa miaka 10 anzeni ku practice kuonyesha wazi kuwa mnaunga mkono kwa vitendo .Wabunge wote waliokaa miaka kumi waje hadharani watamke wazi kuwa sisi tunaunga mkono rasimu ya Warioba hatutagombea tena miaka kumi inatosha.Wananchi wangewashangilia sana kuwa you mean what you say.Lakini kama wabunge wenu walikaa miaka kumi watarudi tena kugombea it means upinzani hamko serious kwenye vitu mnavyoongea Na watu watawachukulia na nyie ni madomo kaya tu hamna lolote

Mimi sio mbunge wala mwanachama wa cdm, wala sio msemaji wao, bali shabiki wa cdm. Ninasimamia ninachoamini, sio wanachoamini wabunge wa cdm. Sasa unapotaka mimi, sijui na wabunge wa cdm tutoke tuseme utakacho unategemea nini? Mimi maoni yangu kwenye rasimu ya Warioba nilipendekeza mwisho wa ubunge iwe miaka 10, maoni yangu hayo hayakujali wabunge wa cdm wanataka au wanaamini nini.
 
Jana Katibu Mkuu wetu alizungumzia sana ukomo wa Urais ila akapitia kwa mbaaali kuzungumzia ukomo wa wabunge ila vijana tuliinasa nikajiuliza hivi kwanini?

1. hakuna ukomo wa ubunge na kuna video clips na picha za wabunge wazee kulala hadi kukoroma bungeni, wengine hawana maajabu wapo wapo tu bungeni hawaongei chochote tangu bunge linaanza hadi linavunjwa hawana cha kuchangia kujenga taifa zaidi ya kuleta mawazo ya kizamani tu!! kwanza wabunge wazee ni mzigo kwa walipakodi, ni watu waliochoka ambao kazi yao kubwa bungeni ni kupasha viti joto tu! ni watu wanahitajika sana kurudi kijijini kucheza na wajukuu,

2. kuna wabunge wazee wanaumwa for five years tangu bunge linaanza hadi linavunjwa ! na wanalipwa kodi za wanyonge tu , halafu kwanza wabunge hawa wazee kina Chenga, Mkono nk ni mzigo kwa kodi za walalahoi bajeti ya matibabu yao nje ya nchi ni kubwa mno wanatibiwa nje bila ulazima wowote watu wenyewe wamejiishia wanaacha Mloganzila ipo for them. Mh Rais huku bungeni kuna hela nyingi ya kuokoa kulipa vibarua wa SGR wabunge wote watibiwe nchini mbona sisi raia wanyonge tunaokupigia kura za kishindo tunatibiwa nchini na hatufi kwa corona na malaria na kuharisha?

3. kuna wabunge watoro bungeni tangu bunge linaanza hadi linavunjwa hawapo bungeni wako na mishe zingine tu za kujiongezea kipato na kule wanalipwa kodi za wanyonge wapi Dr Bashiru unajua hili? Mh Rais hapa ukipewa list na kuwakata wabunge watoro mishahara utapata pesa ya ndani kulipia vibarua wa kujenga Stieglers Gorge dam!! kupanga ni kuchagua!!

4. kuna wabunge wengi hawana sifa za kitaaluma za kuweza kufanya kazi za kibunge, wana elimu ndogo na uwezo mdogo wa kiakili hawawezi kuchambua complex issues kama ripoti ya CAG, bajeti za wizara, ripoti za kamati kama PAC nk nao kazi kubwa wanaropoka kukashifu wenzao , kupiga vijembe na kuleta mipasho tu bungeni na kupiga meza na kuibua mijadala isiyo na tija kwa nchi hii maana they cannot reason!!

5. kwanini sifa ya mbunge iwe kujua kusoma tu na kuandika wakati majukumu ya mbunge tukisimama kwenye ukweli yanahitaji Graduate? mf sheria nyingi ziko kwa kiingereza ndo zinakaa vyema na wabunge hawa vilaza kwanini sasa wawepo jumba linahitaji wasomi?? huwa najiuliza ni mjinga gani aliweka kipengele hiki? kwa mantiki gani? kwa maslahi ya nani?

6. Je mchakato gani utumike kuweka ukomo huu haraka? kwanini Rais tumuwekee kikomo halafu tukubali wabunge wasiwekewe kikomo? nilijiuliza kwanini sisi watu weusi ni watu wajinga na sera zetu nyingi za utawala zinaonesha ujinga wetu na hatukemei?

7. nilijiuliza kwanini kusiwe na ukomo wa umri wa mbunge ili kuwaengua wazee zaidi waliochoka, mfano mbunge awe na miaka 30 hadi miaka 60 na si zaidi ili kupata watu wanaowaza kujenga nchi na si kujilimbikizia mali na kusubiri kufa vifo vya ghafla vinavyotokana na moyo kushindwa kusukuma damu ya mwili wenye tumbo kubwa lililojaa mafuta ya kodi za wanyonge!!

Naomba Dr Bashiru simamia hili ukomo wa ubunge uwe ten years only and Allah will bless you! Kumbuka kila mtu ni mchunga na ataulizwa kwa alichokichunga wabunge wazee wa chama chako wanalibiia taifa nawewe ni mtendaji mkuu msaidizi!!usikubali!!

Kuna wabunge wazee wengi wameiba vya kutosha pesa ya umma kwa miaka mingi na wamejimilikisha ubunge kwenye majimbo yao kwa kutumia pesa na majina yao (influence) na hawaleti maendeleo yoyote majimboni kwao!!

Jana nilikusikiliza vizuri kwenye mdahalo wako na Tido mwanzo mwisho nikakuona ni Kondoo umevaa ngozi ya Chui, wewe Dr Bashiru ni Mzalendo wa kweli kama Mh Magufuli nanyi mmejificha ndani ya genge bovu la wasafi na wengine Manyang’au!!
Ubunge ni ajira mkuu kustaafu kwake ni kifo kwa Tanzania sahau hao wazee ndio wapitisha miswaada yenye tija kwa watu fulani
 
Back
Top Bottom