Ukombozi wa nchi yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukombozi wa nchi yetu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kagwina, May 14, 2009.

 1. Kagwina

  Kagwina Member

  #1
  May 14, 2009
  Joined: May 1, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekaa na kutafakari hatima ya nchi yetu yafuatayo yakanijia kichwani kwangu. Kutokana na halia ya sasa na mfumo wa kisiasa, kiuchumi na kijamii, maisha kwa Watanzania wanyonge walio wengi yataendelea kuwa hivi daima. Itatuchukua miaka mingi kubadlisha hali hii hii inatokana na uwezekano kwamba pengine kizazi cha kufanya mabadiliko tunayoyataka hakijazaliwa au ndio kwanza kimezaliwa. Tizama namna viongozi wa kisiasa wa nchi hii wanavyopatika, kichefuchefu kitupu. Wasomi na wenye uwezo wa kuleta mabadiliko wanakimbilia kwenye siasa, vijana wadogo wanaotoka Vyuo vikuu wanakimbilia kwenye siasa, Mathalani vijana wengi waliomaliza UDSM mwaka 2005 wamechukua nafasi nyingi za uongozi CCM, kinachowavuta si uchungu wa nchi hii bali ni kutafuta maisha mazuri. Tusitegemee kupata viongozi tofauti na waliopo sasa kwa kuwa ni matokeo ya mfumo tulionao.

  Serikali iliyopo madarakani imegawanyika kutokana na mgawanyiko katika Chama tawala. Mathalani, Mawaziri karibu wote wapo busy kuhakikisha kuwa kundi lake linaibuka kidedea, katika mazingia haya, watu wapo busy kuwachafua wenzao na kujisafisha badala ya kumsaidia Rais kuongoza nchi na kuwaletea maendeleo wananchi. Dhambi hii itaendelea kututafuna milele kutokana na makovu yaliyoachwa nyuma na wanamtandao wakati wa kuingiza serikali hii madarakani. (Wachambuzi mbalimbali wamelisema hili). Yafuatayo yatatuondoa hapa tulipo;
  1. Kama kweli Rais ana nia ya kutuletea maendeleo na tatizo ni wasaidizi wake basi awafute kazi wote na kuanza upya. Mrisho kasema kuanza upya si ujinga. Atengeneze base yake mpya kabisa na awasahau maswahiba wake wote na kufanya kile ambacho anaamini kuwa kitaisadia nchi hii.
  2. Tuendelee kumuomba Mungu awabadilishe fikra viongozi waliopo ili wageuke na kuturudisha njia panda ili tuchukue njia sahihi kwa kuwa naamini tumepotea kabisa na tunazidi kwenda tusikokujua.
  3.Kundi moja kati ya hayo yanayogombana CCM lijitoe na kuanzisha chama kingine kwa kuwa mbinu zote wanazijua itakuwa ni rahisi kuwadhiti wenzao wakati wa rafu za uchaguzi na hatimaye chama kitakachishinda kitaongoza kwa displine kwa kuwa kuna watu wenye uwezo wapo pembeni wanapiga jaramba.
  4. Tupate Rais kichaa kwa muda wa miaka 10 tu ambaye akipita barabarani mara mbili na kukuta shimo kubwa anamfukuza engineer wa Wilaya on the spot ili kuleta heshima katika utumishi wa Umma. Apunguze posho na mishahara ya wabunge na kuongeza maslahi ya watumishi.
  5. La mwisho ambalo litatokea kama yote haya yatashindikana ni kuchapana ili tuheshimiane.

  Bila hivyo tutaendelea kuimba wimbo wa kupambana na ufisadi kila leo na hakutakuwa na mabadiliko yoyote, tutakufa watakuja wengine watakufa na damu za vizazi vijavyo itakuwa juu yetu.

  Naomba kuwasilisha mawazo haya kwa michango yenu.
   
 2. N

  Nampula JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2009
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mzee hayo mambo 4 yote kutokea ni ngumu lakini hili la tano naona ndio njia iliyobaki.kwa sababu tumekuwa tukihubiriwa amani lakini mie sioni kama tuna amani as long as masikini ya mungu wanakufa kwa maradhi ambayo kwa uoni wangu ni rahisi kutibika.kiufupi nasema tz hatuna amani .Tuna amani vp wakati vifo vya watoto na wanawake vinaongezeka kila kukicha?kuna amani vp wakati 95% ya watz hata huo mmoja kuupata kwa mbinde?tuna amani vp wakati watu wachache tu mafisadi mapapa na manyangumi ndio wanaokula national cake?
   
Loading...