Ukombozi wa Anunnaki

Ukombozi wa Anunnaki

Joined
Jun 17, 2022
Posts
4
Reaction score
16
ANUNNAKI WATATUKOMBOA KUPITIA NIBIRU.

KUPITIA SOMO HILI UTAJUA UJIO WA YESU HNA MAANISHA NINI HASA.

Kama ambavyo tumeona Nibiru ni chombo ambacho kipo kweli, ambacho pia kinaitwa Meli mama yaani Mothership.

Nibiru ilikuja kwenye mfumo wetu wa Jua wakati wa kuanza kwa Milenia, Milenia 2000. Ilikuja karibu na Dunia yetu kutokana na mpangilio wa kisayari (Planetary alignment). Mpangilio huo au Planetary Conjuction ilisababisha sayari hiyo kuja karibu na Dunia yetu pasina kuathiri au kuharibu mzunguko wa mfumo wetu wa sayari. Kama uki gogo (Google search) kuhusu picha za Satellite za sayari ya NIBIRU utaiona sayari hiyo ikionekana nyuma ya Sayari ya Pluto. Andika "Planet X visible on sky" utapata picha hiyo ambayo ni video ya dakika kama 4 hivi, ambayo itathibitisha Nibiru ni kitu cha kweli na NASA pia wamekiri Nibiru ni kitu cha kweli.
Kwahiyo Nibiru ni Mothership, yaani Meli mama ambayo viumbe weusi wa sayari ya mbali (Melanated Extraterrestrial) Wataitumia kurudi Duniani.

Inachukua miaka 3,600 kwa meli hii mama kuzunguka mfumo wetu wa sayari na mifumo mingine ya Sayari kwakua imeonekana tupo kwenye mfumo pacha wa mfumo wa sayari yaani binary solar system, kwamba galaxy yetu na galaxy ya 19 zimeungana.

Meli hiyo mama ina fuwele yaani "Crystals" nne
Fuwele hizo ni pamoja na Amethyst Crystal ambayo ni ya rangi ya zambarau (Purple) inayowakilisha mlango wa sita wa ufahamu (6th Chakra) Third eye chakra. Kuna fuwele ya Zumaridi yaani, Emarald crystal ambayo ni ya kijani kwa mlango wa nne wa Ufahamu ambayo ni chakra ya moyo (Heart Chakra), chakra ya nne.
Kuna fuwele ta Safira yaani Saphire crystal yenye rangi ya baby blue kwa chakravya koromeo (Throat Chakra) na mwisho ni Fuwele ya Yakuti nyekundu yaani Ruby red Cryatals ambayo ni nyekundu kwa Chakra ya Tano.

Hizo ni fuwele nne ambazo zina kemikali zilizo tumika kutengeneza meli hiyo na kila kitu ambacho meli hiyo inacho. Unaweza kuona meli hiyo ina fuwele za muhimu kabisa ambazo zinapatikana kwenye mwili wa mwanadamu. Hiyo inathibitisha zaidi kwamba tunashiriki jeni sawa na ANUNNAKI wa Nibiru. Kumbuka wanadamu tuna milango saba ya Ufahamu ama chakras kwenye miili yetu ambazo zinajulikana pia kama vituo vya nishati yaani Energy Centers. Somo hilo tutalipata vyema kwenye Ukitoho (African spirituality) na Unajimu (Astrology) ambapo masomo hayo yanafundishwa na mimi mwenyewe kwa mfululizo maalumu hapa na kwenye group letu la KUNDALINI AWAKENJNG IN TANZANIA CENTER. Hakika Nibiru imetengenezwa kwa Teknolojia ya hali ya juu.

Nibiru ama Neb Heru ni jina la kale ambalo lilitajwa na watangulizi wetu (our ancestors) wa Misri ya kale, kumbuka Wamisri walikuwepo kabla ya Caucasians. Neno BC linamaanisha before Caucasians yaani kabla ya Caucasians (Wazungu).

Kumbuka Melanated beings (Watu weusi) walkkuwepo muda mrefu kabla ya Wasumeria na waliwafundisha Wasumeria kwahiyo tunapozungumzia Nibiru, watangulizi wetu waliita Meli hiyo mama Nibiru, kutokana na kanuni asilia za Misri (Egypt's natural laws) au Netars au kanuni asilia (Principle of Nature).

Nibiru inaelezwa kwamba ni muunganiko wa majina ya ki-Afrika, Neftis pia akiitwa Neb het na Horus ama Heru. Ukiunganisha majina hayo ya kiafrika pamoja unapata Nebheru ambayo ndio Nibiru. Neft au Neb het alikua sambamba na mungu mke wa misri, Isis/Auset pamoja na Mungu mme Osiris ambaye pia anaitwa Ausar/Osur, tunajua kwamba Osiris ni Mungu wa Fikra (Mind god), Mungu aliyeenea pote (The omnipresent Entity), Muumbaji wa Fikra Utashi. Neb het ni Mungu wa kutufikisha kwenye uwezo wa Auset inawakilisha utashi wa chini.

Kwahiyo kurudi kwa sayari ya Nibiru, kiishara ndiyo kurejea kwa Neb het, kwamba ni Ishara ya zama za Aquarius (Aquarian age) ambayo itakua ni zama za kuamsha Fikra kutoka kwenye miaka 6,000 ya kipindi cha kutokua na haki (Unrighteousness) ambacho tumekipitia kwenye mzunguko wa Zodiaki wa anga. Kwa miaka 6,000 tumeishi kwenye kipindi cha utashi wa chini unaowakilishwa na Auset na sasa tunakwenda kuishinda hali hiyo kupitia ujio wa zama za Aquarius (Aquarian Age) ambayo ni Uamsho wa Fikra (awaking of the Mind).

Tunajua Jua linachoma vkkali na kama hauna Carbon asilia au kiumbe usiye na Carbon asilia utakwenda kuungua (Incinirated) kama Caucasians (Wazungu). Kwahiyo tunafahamu watangulizi wetu waliwekewa hatua tatu za Hekima ya ulimwengu ambazo walizifanya. Hatua hizo ni Alchemy, turning Lead to gold, yaani sayansi ya Alkemia ya kubadili metali zisizo na thamani kama risasi kuwa metali za thamani kama dhahabu, hatua ya pili ni Astrology ambayo ni Elimu ya vitu vya angani na namna vinavyo ingiliana nasi na tatu ni Theurgy, ambayo ni tambiko (Ritual).

Kwahiyo watangulizi wetu waliowekewa sayansi hizo waliipa jina Nibiru meli hiyo Mama ili kutupa maana halisi, wakati meli hiyo itakapo rudi. Kwamba wakati meli hiyo itakua ikirudi inamaana tutapata uamsho mpya wa Fikra kutokea kwa Ausetvambaye ni utashi wa chini kutokana na kuwezeshwa (Activate) kwa wema/haki (Righteousness). Hii ni sawa na kuamshwa kwa DNA zetu wakati huu wa zama za Aquarius. Kwahiyo ujio wa planet X yaani Nibiru, kunamaanisha ama ni ishara ya kurudishwa kwa heshima ya mtu mweusi . Ni wakati wa kurudi kwenye kiti chetu cha utawala na kurudi kwenye haki kutoka kwenye utashi wa chini kupitia uamsho wa Fikra zetu.

Huu ni wakati wa kurudi kwa jua (Horus/Jesus), kuja kuchoma kwa upendeleo wetu kwamba kitu chochote ambacho sio asilia kwenye sayari hii kitaangamizwa kwa kuunguzwa. Kwahiyo, hiyo ndiyo maana ya Nibiru. Nibiru ni kubwa mara nne ya dunia hivyo nchi zingine tofauti na bara la Afrika zitaathiriwa na nguvu ya mvutano wa usumaku (Gravitational Electromagnetic Field). Inaelezwa kwamba, hivi sasa athari ya sayari hiyo Nibiru, imeanza kuonekana ambapo viwango vya maji kwenye bahari vimeanza kubadilika na vina vya bahari vinaongezeka. Rejea maelezo ya Ujio wa Anunnaki na ujenzi wa mapiramid kwenye nakala za nyuma.

Kama ukiangalia unaweza kuona kwanini wazungu wananunua ardhi ya kutosha Afrika. Kwasababu ukiangalia mazingira ya kijiolojia ya Afrika, yaani Landscape, Afrika inaonekana kwenda Juu kama mlima ndio maana upepo wa mto Nile Misri unaonekana ukivuma upande tofauti kwasababu unapoelekea Afrika kaskazini kutokea kusini ni kama kuna mwinuko kutoka usawa wa Ardhi kuelekea usawa wa bahari, kwahiyo sayari itakapo anza kufurika kutokana na kurejea kwa Nibiru na vilevile kupata joto kali kutokana na Jua kali, Afrika itakua mbingu salama kwetu sisi ambao ni watu asilia (Original People). Kwa hiyo caucasians watajaribu tu kwenda chini ya ardhi kukimbia majanga hayo ndio maana wanatumia mbinu za uzazi wa mpango kupunguza idadi ya watu Afrika ili kupunguza mtafaruku wa kugombea ardhi mama ya Afrika.

Nibiru ndiyo iliwaleta viumbe kutoka sayari ya nje ya dunia (Extraterrestrials) duniani, kipindi cha nyuma ambao walikua na nasaba za watu weusi., ndio maana damu ya watu weusi jna asili ya nje ya dunia kutokana na ANUNNAKI. Wandugu hii ni kwa mujibu wa watafiti wa masuala ya sayarivya Nibiru na ukombozi wa mtu nweusi.

ITAENDELEA

NI MIMI NDUGU YENU JAMES LORDY KASHIRINA MTAFITI NGULI WA VIUMBE KUTOKA NJE YA SAYARI YA DUNIA.
 
Nimependa umegusia hizo Chakra! Binafsi huwa nafanya Cleasing, healing na balancing kila ninapoona mambo si mambo, big up!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom