TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,845
Habari za weekend ndugu yangu, bila shaka upo katika mapumziko murua kabisa siku ya leo na hata kama upo kazini basi unaifurahia siku hii. Leo ningependa kuzungumzia kuhusu ukoloni mweusi
Ukoloni ni ile hali ya kumtawala mtu au nchi nyingine kimabavu pasipo ridhaa yake ambapo mtu au nchi hiyo huwa chini yako na wewe ndiye unakuwa na mamlaka au maamuzi juu yake.Yamkini wengi wetu tumeishia kusoma shuleni somo la historia ambapo tulielezewa na waalimu wetu ambao nao walifundishwa kuhusu ukoloni ila ni wazee wachache sana ambao wamebaki hai hadi leo walioshuhudia kwa macho yao mateso makali ya ukoloni. Wengi tunaishia kutamka neno 'Ukoloni' na kuliona ni neno tamu sana kulitaja lakini makali yake ni mabaya sana kulinganisha na tunavyofahamu.
Kipindi cha ukoloni nchi nyingi sana zilijitoa kimasomaso kuweza kupambana na wakoloni hao ambapo walisalimu amri na kunyanyua miguu yao au kwa matakwa yao wakaamua kuondoka kwa amani kama walivyofanya waingereza kwa Tanganyika. Shangwe na vigelegele vilikuwa havizuiliki nchi nzima, watu walitembea umbali mrefu kwa furaha kupashana habari namna tulivyopata uhuru na furaha ile haikuwa na kifani.
PICHA LINAANZA
Hivi leo sio jambo la ajabu sana kusikia mauaji ya kila namna yanayoendelea katika baadhi ya nchi zetu za Afrika kama Libya, Kongo, Afrika ya kati, Afrika ya kusini, Msumbiji na kwingineko ambapo ni mapigano ya sisi kwa sisi tukishawishiwa na mataifa makubwa ya nje ambayo yanamezea mate rasilimali zetu. kwani hamkusoma kipengele cha "divide and rule"? yaani "watapanye kisha uwatawale" ndicho tunachofanyiwa sasa hivi. Nina hakika wale wapigania uhuru ambao wamelala udongoni sasa hivi wakipewa nafasi ya pili kurudi tena kwenye uhai watamwaga machozi kwa hiki kinachoendelea sasa. Tumekosea wapi, kwanini hatujifunzi kutokana na historia yetu, kwanini tunatesana wenyewe kwa wenyewe na kuuana bila sababu zaidi ya kugombania mali tu? Angalia kinachoendelea Afrika kusini watu wanauana sababu ya kugombania mali yaani wanawaua na kuwanyanyasa raia wa nchi nyingine simply sababu sio wazawa is it fair? Upendo na utu wetu ule tulioachiwa na babu zetu wapigania uhuru upo wapi? Damu za wapigania uhuru wa Afrika zinalia udongoni kwa usaliti mkubwa unaoendelea katika nchi za Afrika. Inatupasa turudi nyuma na kutubu kwani kuimwaga damu ya Mwafrika mwenzako haikuongezei kitu badala yake unazidi kuwapa nafasi wa mataifa makubwa waje kukutawala waziwazi kama walivyofanyiwa watu wa Libya..Nafasi ni yako sasa kudumisha upendo ule wa kale na ukumbuke sisi sote ni ndugu "Sisi ni Wamoja" nimeikumbuka kauli ya Raleigh 2014. Sabato njema wapendwa
Mtenga Gerald
04/03/2017