Yaani kwa kuwa alishusha viwango vya ufaulu sio?watu wanasema afadhali alipokuwa Kawambwa kwenye hiyo wizara!
Nilitegemea useme hapa na uoneshe kosa alilolifanya Mama Ndalichako.Maamuzi yake na watendaji wake wote katika wizara inayosimamia huduma za elimu nchini ndiyo majibu ya kidato cha NNE ya sasa.Hali si nzuri kabisa tofauti na miaka ya nyuma, walimu hawana ari na kazi, wanaingia darasani ili kuonekana wako makazini tu.
Wengine tulisema kuongoza Wizara ya elimu ni tofauti na kuongoza kitaasisi kidogo kama NECTA ambacho kipo chini ya wizara hiyo.
Hili suala la elimu linahitaji mijadala wa kitaifa kwa maneno ya Mh James Mbatia na sio kuamua haraka haraka tu bila kushirikisha wadau husika kwa kuhisi kua mtangulizi wako aliharibu hapo awali. Tukiendelea hivi baada ya miaka kadhaa tutakua na wasomi wachache nchi ambao kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya awamu ya NNE ambayo ilionekana kubadili hali ya elimu nchini, ni kwamba tunarudi hatua nyingi nyuma kwa maneno ya mzee Jenerali Ulimwengu.
Utakua mzazi wa ajabu na hivyo kama utabaki kumlaumu mwanao uliyemzaa wewe, unatakiwa ubadili mbinu kudeal na mwanao anapokushinda. Ithibiti wa tabia ya mwanao ni wewe mzaziTutawalaumu mawaziri wote, wakati mwingine vijana na wenyewe wako bize sana na mitandao na vitu vingi vya ujanjaujanja huku wazaki wakiwachekea. Hili suala ni la kila mtu katika jamii kushirikiana.
Uko sawa kusema wako bize na mitandao ya jamii ndani yake yupo mzazi ambaye hatizimi wajibu wake ipasavyo.Utakua mzazi wa ajabu na hivyo kama utabaki kumlaumu mwanao uliyemzaa wewe, unatakiwa ubadili mbinu kudeal na mwanao anapokushinda. Ithibiti wa tabia ya mwanao ni wewe mzazi