Uko wapi ukweli kuhusu panya road?

BEDUI Jr

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2016
Posts
2,037
Reaction score
2,858
Habari Mabibi na Mabwana wa Jf;

Haya matukio ya Panya Road kwa sasa yamekua yana tatanisha sana.
Mfano Mimi ni mkazi wa Temeke (Tandika) sikuwai kusikia wala kuona Panya Road.

Lakini cha ajabu nikienda kazini maeneo ya Sinza nawasiki watu wanahadisia kua Panya Road wamevamia Temeke (Tandika ).

Basi nabaki najiuliza, mbona mimi nakaa huko na hiyo siku ambayo wanasema Panya Road wamevamia nilishinda uko na nikawa ktk mizunguko mpaka saa 4 Usiku sikusikia wala kuona Panya Road?.

Hii inanifanya nikumbuke story ya Babu yangu, kuhusu Mwizi Maaru hapa jijini Dar alieitwa MAHMOUDU.
Ipo hivi;

Miaka ya nyuma kulitokea Mwizi maarufu kwa jina MAHMOUDU, kipindi hicho Dar yote kituo cha polisi kilikua Msimbazi Police tu ukiondoa makao Mkuu Centre, hii zamani kidogo.

Kesi za wizi zilizokua zikilipotiwa zote mtuhumiwa wao ni MAHMOUDU.

Haijalishi mleta mashtaka katokea wapi iwe Magomeni au Temeke, tena hata kama matukio yalitokea kwa wakati Mmoja.

Police walimtafuta MAHMOUDU na kumuweka ndani, chakushangaza kesi zikawa zinakuja na mtuhumiwa wao ni yuleyule bwana MAHMOUDU.

Sasa hawa Panya Road kweli wapo kama tunavyo Peana taarifa au tunatishana tu na kulikuza hili jambo.
 
Hao watoto huku mtaani kwetu tumejipanga vizuri sana na tunashangaa kwanini hawavamii huku kwetu tuwaonyenyeshe kazi ila tunasikia wanavamia tu huko kwa wachovu wachovu
 
Mkuu sasa ww huoni katika hyo habari ya panya road mpaka watu wanajeruhiwa na picha unaziona mtandaoni.
 
Panya road si mtu ni jina wamepewa wahalifu wa kikundi kimoja wanaovamia eneo moja kwa wakati mmoja kwa lengo la unyanganyi mali. Hivyo inaweza kuwako na vikundi vingi vya panyaroad vikifanya uhalifu kwa wakati mmoja ama tofauti.
Pia mkuu wewe ulikua temeke mtaa gani na hao uliowasikia walipita mtaa gani
 
Tandika kubwa Sana, Ina maana tandika yote uliitembelea usiku huo
Sio kubwa kama unavyozani kiasi litokee tukio la wadudu kama Panya Road alafu usisikie au kuona
 
kuna campaign ya kuwadhalilisha wanaume wa dsm kwa wale wa mkoani.

marpc wote wamepangwa.
 
Wanasema tukio limetokea Tandika sokoni yani mpaka watu wamefunga maduka mapema.
Mimi nipo kalibu na hapo Tandika madukani
 
kuna campaign ya kuwadhalilisha wanaume wa dsm kwa wale wa mkoani.

marpc wote wamepangwa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji114][emoji114]
 
Huyo babu yako kilaza kakuona wewe ni boya ndio maana kakupa story ya uongo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Wanasema tukio limetokea Tandika sokoni yani mpaka watu wamefunga maduka mapema.
Mimi nipo kalibu na hapo Tandika madukani
Next time watakufikia tu mkuu na huwa ni tukio la dakika chache maana wanafanya kazi yao kwa tahadhali kidogo wanachokipata wanatoweka
 
Huyo babu yako kilaza kakuona wewe ni boya ndio maana kakupa story ya uongo [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] story ya kweli Mkuu huyo MAHMOUDU alikua anatokea mkoa Kigoma na baadae walimrudisha kwao na alipigwa marufuku kutoka nje ya Kigoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…