Uko wapi Udikteta wa Rais Magufuli?

Elimu haina mwisho,kajielimishe kuhusu Udikteta unaopingwa!
Jielimishe kuhusu uendeshaji bunge!
Jielimishe kuhusu haki ya vyama Vya siasa kufanya sasa muda wote kisheria!
Jielimishe kuhusu haki zingine za kuraia.
Magufuli anafanya baadhi ya mambo vizuri,hususani nidhamu kazini na ukusanyaji kodi
UKUTA haipo kwa hayo mambo.Raia tutaijuaje serikali yetu kama vyama Vya upinzani vinazibwa mdomo? Vyama hivi ndio vioo Vya raia juu ya serikali yao.
 
Hao ni wasaka tonge
Hawana hoja mpya
Wameishiwa,
Nshu ya ufisadi imewameza hawana lolote wana tapatapa.
Wacha watikise kibiriti cha Gesi
 
Mr Mpendazoe, tatizo siyo hilo bali tatizo ni Magufuli kuendesha nchi kiimla, kukiuka misingi mingi ya katiba, kuamini kuwa nchi hii kuna CCM pekee na ni lazima kila Mtanzania awe mwana CCM.
Kivipi?madai yako ni ya junla mno fafanua
 
Mpenda zoe, muda huu si wa kuwapinga chadema na ukawa kwa ujumla, ni kujiharibia siku tu maana chadema na ukawa hawajui hata wanajiita ukawa kwa kutaka mabadiliko ya katiba iliyopo kuwa ina mapungufu makubwa! Katiba inaruhusu nchi kuongozwa kijeshi kupitia rais wa nchi huyohuyo na ndio maana yeye ni amiri jeshi mkuu!
 
It's too late Mzee Fred Mpendazoe, sidhani kama una kifua cha kujibizana na UKAWA na hao wafuasi wao wa UKUTA.

Ningekushauri upumzike tu ule pension yako. Nimjuavyo Uncle JPM, na namna yake ya uongozi.... Usitegemee kupata kifuta jasho kwa ''kuwashauri UKAWA" otherwise Le Mutuz kwasasa angekuwa DC au RC.

You don't pose any threat to his regime... Kina Polepole wali"pewa" kwa vile walikuwa hatari. Ila wewe......... Kaa utulie mzee, achana na siasa za mitandaoni!!!!
 
Chakaza,

You have said!

Kuna wakati nilisikitika sana Mpendazoe alipokosa ubunge Segerea. Lakini sikusikitika wananchi wa Kishapu, kule kwao, walipomkataa mapema tu mwaka jana kwa kuwa tayari nilikuwa nimeanza kumwelewa vizuri.

Ukisoma alichokiandika (kama ni kweli kaandika yeye), ni uthibitisho tosha kwamba Chadema walikuwa sahihi kutompa nafasi yoyote nyeti ndani ya chama. Huyu ni mzigo ambao hauwezi kubebeka hata huko ulikorudi na kukatwa mkia!

Mtu makini yoyote ndani ya CCM, kwa maandishi yale atajua wazi kuwa Mpendazoe anajikomba na kujipendekeza kwa kiwango kilichopitiliza! Mwenye access na makala yake ya kumwomba Lowassa amsamehe atuwekee hapa tafadhali!

Na kwa andiko hili Mpendazoe anachafua dhana nzima ya mtu kuamua kuwa mwanasiasa!
 
Mpuuzi pekee ni yule anayeweza kutumia madhaifu ya mwingine kuharalisha maovu yake!!

Mambo ya Lowassa na chadema yao walifanya mambo yao haijarishi ni mazuri au mabaya Kwa sababu hawana effect yeyote kwa utawala uliopo madarakani

Hivi ccm ilimtuma kuongea mambo ya kufatua watoto
Ningewapoteza
Wataishi kama mashetani
V.ilaza wakati mtoto wake yupo udom anasoma?
Ilimtuma akurupuke kuzui sukari?
Kufanya mikutano peke yake wakati wapinzani wakisubiri mpaka 2020
Haaaah kama ccm na baraza la mawaziri walimutuma hivi kwanini hawakumtuma na jk??
 
Njaa imekurudisha CCM tena ulidhani na Chadema kuna pasi fupifupi za kupiga pesa kweli zidumu Fikra za mwenyekiti...yani wewe na Msindai ni kama mapacha
 

Tokea urudi tena Kundini CCM sina tena matatizo na Wewe Mkuu na nakusihi sana endelea kuwaeleza Watanzania athari za kuwa mwana CHADEMA na faida nzuri za kuwa mwana CCM kama Mimi na Wewe. Uliona mbali mno hadi kuamua kurudi CCM na Wana CCM tumekusamehe na tumekupokea bila Kinyongo. Binafsi nilihuzunika sana ulipohamia CHADEMA na nikasema ni Shetani gani alikuhadaa vile? Karibu tena CCM Mkuu.
 
Kama kweli kweli kabisa mheshimiwa rais anafanya maamuzi kwa kufuata ushauri wa taasisi hizo mbili ulizozitaja.....basi nina mashaka na weledi watu waliomo kwenye taasisi hizo na weledi wa mheshimiwa raisi katika kuwatumikia wananchi.....

Mheshimiwa rais anashindwaje kuchanganua baadhi ya mambo anayoshairwa kuwa yana impact kwenye jamii ya sasa iliyojaa werevu......

Mheshimiwa rais kama anapokea hizo shauri bila ya kuzipima kwa mizani yake ya fikra....ni wazi kuwa tumepata kiongozi mkuu wa nchi asiye na busara........

Kama hao wanaomshauri ndio wanaona hizi ndio shauri zinazomfaa mheshimiwa raisi basi naweza kusema kuwa moja kwa moja hizo taasisi hazimtakii mema mkuu wa kaya.......
Kwa hivyo mheshimiwa rais kama anania ya dhati ya kutaka kuirudisha hii nchi kwenye mstari....basi watu wa kwanza kabisa anaotakiwa kudeal nao ni hao hao anaowaita washauri wake.....

Maana tangu waanze kumshauri sijaona jambo lolote la maana wanalomshauri zaidi ya kuzua taharuki kwenye jamii......

Kwa mfano kama ndio hao hao waliomshauri kuzuia sukari ya nje kuingia nchin ili hali bado hakujaandaliwa mazingira ya viwanda vyetu kukidhi mahitaji ya ndani...je watu hao wana uhalali gani wa kuendelea kumshauri rais...!!!??

Kama ndio hao hao waliomshauri kuwa mbinu nzuri ya kuuzima upinzani ni kuzuia shughuli za kisiasa kwa vyama upinzani bila ya kujali kuwa wanasigina katiba ambayo mheshimiwa aliapa kuilinda na kuitetea....bado wana uhalali wa kuendelea kuwa washauri wa raisi......

Kwa hapa taifa lilipofikia mheshimiwa rais ndipo anatakiwa apime weledi wa washauri wake......
 
Kwa hiyo Ndugu uliekua Mheshimiwa Rais kukataza mikutano huoni ni kinyume na katiba aliyoapa kuisimamia?
Lkn...ni kweli mikutano imekatazwa?
...mbona tunapata taarifa mikutano inayoendelea?
...hata sasa CUF wako kwenye mikutano yao mchakato wa kujichagulia viongozi wa vyama vyao....CDM na CCM pia tumepata taarifa za mikutano yao!
.....lazima tujielimishe, tukishafundishwa, ili tuijue kweli na tusimame nayo!
 
Wewe naamini ubongo wako utakua umeliwa na mchwaa maana ulitakiwa ujadili yanayowafanya waandamane sio kujalibu kutafuta tu point uchwara za kutetea chama chako labda ungetoa ufafanuzi juu ya Kupiga marufuku mikutano ya kisiasa angali wao wanaFanya na safe zao za kijan afu wana singizia mkutano wa serikali wakat had I wana siasa jukwaa wana kweaa

Pili kuhusu kuzimwa kwa matangazo ya bunge hapo VIP?

Vip uteuzi wa baadhi ya makada kua madas na ma DC

Ennh VIP kuhusu ukuta??? Rais kama taasisi yenye washaur wenye busara basis wange tafuta namna ya kushughulikia hili swala kama wana amin no uvunjifu wa a man lakin wana tumia mda mwingi kuwatishia ukawa kwa kichapo cha polisi this is non sense what I know mfamaji haishi ....... Lakin so vibaya kudunduliza point za kuteteana walumumba
 

Uko sahihi ila hujasema kuzuia mikutano ya kisiasa ni sahihi??
 
Njia bora ya kukanusha udikteta anaosingiziwa ni kuruhusu maandamano ya amani yaliyo kwa mujibu wa sheria ili madai yao yaonekane hayana mashiko. Hilo lina ugumu gani?
Lkn, sheria iliyopo sio ya kuruhusu maandamano tu, ipo na nyingine ya kuzuia maandamano, kama kuna sababu ya kufanya hivyo!
...polisi wamesema hawawezi,kutoa/kusimamia usalama ktk maandamano ya nchi nzima kwa wakati mmoja!
...kumbuka na asli ya aina yenyewe ya maandamano..."kenge, wanangojea fursa ya maandamano ya heri, waingie msafarani ili wafanye mambo ya kikenge, kimakwelikweli".....
...
 
Heeeee! Mungu wanguuuuu! Hivi huyu ndiye Mpendazoe nimjuaye? Jamani! Mbona alikuwa na akili nzuri tu kwani sasa nini kimemtokea? Hata kuandika Kiswahili hawezi siku hizi! Eti upotodhaji! Ndio nini hiki? Hivi hii ni njaa ya Ukurugenzi? Ukuu wa Wilaya? U-Katibu tawala? CCM na serikali yake mhurumieni huyu, mpeni cheo kabla mambo hayajaharibika zaidi. Kuna ndugu yangu mmoja alianza mambo yenye mwelekeo huu huu baadaye akaanza kuweka mavazi begani. Kumbe akili yake ilianza kushindwa kufanya kazi yake vizuri. I cannot believe that this is a person whom I know.
 
Fred, ni wewe kweli?? Siamini hata kidogo! Inakuwaje - huoni ubabe ambao utatugharimu dakika yeyote sasa? Au unafikiri bado uko salama kama hawa wakubwa (CCM na CHADEMA) wakipambana mtaani?

Unajiaminisha nini kuhusu JMP pamoja na kauli za uwazi za kuzuia demokrasia. Ni vizuri tukawa pamoja ili Rais aone hatari inayotusogelea. Lakini wewe umesukumwa na nini? Ukanda labda. lakini wewe huna silika hii ya ubaguzi, kuna nini kimekutokea???

Kumbuka una nafasi katika kuleta amani ndani ya taifa- wanapogambana ndugu usiongeze uchochezi bali tafuta jinsi ya kuwaletea njiwa mweupe! Ubishi na ubisho hautavusha taifa hili salama. Hata wewe!!!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…