Financial Intelligence
Senior Member
- Sep 29, 2023
- 150
- 277
Tunaposema Mama Samia aongezewe miaka mingine mitano ni mambo kama haya tunayatazama,
Haya mambo hayakuwahi kufanyika tangu uhuru wa Taifa hili but why now?
Sasa twende na Mimi kwenye hoja:
1. Benki ya NMB tanzania na Klabu ya Yanga SC wamezindua Kadi Maalum za Wanachama wa Yanga,
2. Huu ukiwa ni ni muendelezo wa ushirikiano kati ya taasisi hizi mbili kubwa nchini za kibiashara.
3. Kwa wasiofahamu, Kadi hii ya NMB Yanga World Debit Mastercard huunganishwa na akaunti na huduma zote za kifedha za Benki ya NMB.
4. Mwanachama atakayejiunga atapata Jezi 6 Kila Msimu, VIP Ticket 10 za Msimu wa NBC VPL
5. Kadi hii pia Kutumika in kwa VIP Lounge katika viwanja vya ndege vya kimataifa bure.
6. Kadi hii pia inakupa Bima za safari ukilipia tiketi ya ndege kutumia kadi hii ikiwemo kulipwa hadi Dola za Kimarekani 3,000 begi likipotea, hadi Dola 300 ndege ikichelewa na kupata mpaka Dola 7,500 kama safari yako ya ndege ikihahirishwa.
7. Hata unapougua NMB itakupa punguzo la kuanzia 10% na kuendelea ukitibiwa katika hospitali zote za Aga Khan nchini.
8. Utapata pia Punguzo la hadi 10% ukifanya malipo kwa Kadi/QR katika maduka, migahawa, vituo vya mafuta na maeneo mengine.
9. Lakini pia, Mwanachama kupata Toleo la kwanza la jezi na vifaa vyote vinavyotambulishwa na Yanga
10. Nzuri zaidi mwanayanga kupata huduma zote za kifedha zinazotolewa na Benki ya NMB ikiwemo mikopo nafuu, huduma ya NMB Mkononi na nyingine nyingi.
11. Mwanachama wa Yanga ataipata kadi hii kwa ada ya Milioni Moja kwa mwaka na kufurahia huduma zote hizi kwa mwaka na Kadi hii inapatikana katika matawi yote ya Benki ya NMB nchi nzima kuanzia leo.
12. Hata mwanachama wa Ihefu ya Yanga anaweza pia kununua kadi hii au hata mwanachama wa Club yeyote ile.
Rais wa Klabu ya Yanga, Eng Hersi Said
Filbert Mponzi, Mkurugenzi wa Biashara na Wateja Binafsi