Ukiwa na Mchumba au Mpenzi Mwanachuo jipange haswa...!

Jenerali Ambamba

JF-Expert Member
Sep 8, 2014
3,344
2,535
Leo ni weekend, kama kawaida hupenda kwenda "kijiweni" kupumzika na wenzangu na kubadilishana mawazo juu ya mambo mbali mbali baada ya u-busy wa kazi wiki nzima.

Mmoja wetu tukiwa tumekaa SMS inaingia kwenye simu yake, namuona "amestuka sana" na kubadilika usoni, Mara anapiga simu na kuanza kumfokea huyo MTU ambaye kwa wakati huo hatukuwa tumemjua....

"yaani wewe juzi tu nimekutumia pesa kwa ajili ya birthday yako, ukaniomba tena pesa ya " kununulia simu" nikakutumia juzi, Leo tena unaniomba pesa ya "kusukia" hivi mm Nina kiwanda cha pesa? (Amesikia akifoka sana huyu jamaa).

Sasa ndo akaanza kutusimulia kwamba..

Ana mpenzi wake ambaye wamepanga kuoana lakini huyu mpenzi wake kila Mara amekuwa akiomba-omba pesa mpaka anapata mashaka juu yake na anajutia kuwa naye.

Ni wiki mbili tu huyu binti alimuomba pesa afanye birthday, jamaa akamtumia, baada ya birthday kuisha, demu akampigia jamaa simu kwamba..."simu yake iliibiwa usiku wa birthday, alikuwa ameziacha ndani ya mkoba wa rafiki yake na kuiacha kwa rafiki yake na wao kwenda kwenye birthday, wezi wakaja wakabenua madilisha ya grill na kuloa na kutoa simu na vitu vilivyokuwemo na wezi hao wakatoa line na kuwaachia hivyo wao wakachukua simu tu, jamaa akaamua atume pesa ili demu anunue simu nyingine, pesa hizo katuma wiki hii tu jumatatu, Leo tena demu kampigia jamaa anamuomba pesa ya kusukia, ndipo jamaa akahamaki sana na kumfokea sana.

Sasa wadau pale nikasikia wanampa ushauri mbali mbali, wengine wakisema, huyo demu hakupendi na hana huruma kabisa, wakati huo huo, kumbe jamaa anajenga nyumba, hapo hapo kwao jamaa nao wanamtegemea mshikaji, sasa nikaona nilete hapa ili kuwashirikisha mkasa huu.

Kwa wanaojua mazingira ya vyuo watakubaliana nami kuwa, ukiwa na demu, au mchumba au mke ni lazima ujipange sana maana yaliyopo vyuoni ni makubwa sana.

Unakuta binti ana boyfriend 3, mmoja ndiye aliyemuacha huku mtaani, mwingine ni mwanachuo au lecturer, wa TATU ni mjamaa tu wa huko huko chuo kilipo lakini ni wa mtaani, so ni lazima wanaume tuwe makini sana na viumbe hawa.

Ni hayo tu...
 
Ulikua hujui??? Vipi bint unaish wap?? Mimi mwachuo hiki kigezo ndo kinamfanya binti awe jeur na kujua kua ulimwengu ndo upo uko
 
Uwiiii uwiiii uwiii uwiii uwie yeuwiii
 
1455389847424.jpg
 
hii kali aise,inabidi uwe unatembea dawa za presha muda wote kwa kweli arifuuu....
 
hapo hakuna real love, mbona wapo wengi waliomaliza chuo na wapo maofisin tayari wanasubiri mume mwema tu,kwanini asitafute mchumba huko kuliko kung'ang'ana na mwanachuo? mwanachuo km hajasimama na Mungu lazima atajitumbukiza kwenye maisha ya anasa kwa kuwaiga wenzake pengine waliotoka familia bora au wenye wapenzi walio kula fedha za escrow.
 
Huyo hakuibiwa simu, anamchuma tu. Kama anahofu bora akimbie sasa hivi na labda demu ataisechi nafsi yake kuhitambua tabia yake ya tamaa. Kwa sasa no malavi
 
Hivi haujasikia track la Ney alivyowadis wanachuo..
“Dada unafanya kazi gani?”
“Mi mwanafunzi wa chuo”
“Kila siku uko batani!”
“Ndo maisha yetu wanachuo”-Ney
 
Back
Top Bottom