Mzee mmoja alikuwa akiwapa stori madogo flani wa kitaa..
"Siku moja nilisafiri kwenda Australia basi nikaona Kondoo mkubwa kama Land rover (Gari)"
Dogo mmoja nae akaongezea "Mimi baba yangu hutengeneza Masufuria,basi ametengeneza Sufuria kubwa kama Land rover..!!"
Yule mzee akarukia "wewe ni muongo Sufuria kubwa lote hilo ni lanini?"
Dogo akamjibu "Si la kumpikia yule Kondoo uliyemuona Australia..!!"